MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 10,115
- 15,057
Hivi uwanja wa ndege wa "Kimataifa" wa Mbeya umeshawekwa taa
Wapi Butiama, Msoga, Masasi International Airport? Mwalimu Nyerere RIP hakika ulikuwa kiongozi Wa Tanzania yote. Ulitumia elimu, uwezo, utajiri Na talents za makabila yote kuendeleza Tanzania tena kipindi cha Anologia.Toeni raisi na nyie mpate advantages
Umemjibu vema, hapa tunaongelea masuala ya muhim analeta utani, ishu ni kwamba je anajua kuwa tunakumbushia ahadi ya omukajungutiWapi Butiama, Msoga, Masasi International Airport? Mwalimu Nyerere RIP hakika ulikuwa kiongozi Wa Tanzania yote. Ulitumia elimu, uwezo, utajiri Na talents za makabila yote kuendeleza Tanzania tena kipindi cha Anologia.
Kwani vyuo vilivyopo kilimanjaro vimejengwa na serikali nani kakuambia chuo cha Ushirika kilijengwa na serikali na si Ushirika (KNCU) wenyewe? tafuta historia ya chuo kile na si kuongea uongo! sioni umuhimu wa uwanja wa kimataifa Kagera wakati wa Kigoma na Mwanza upo na pia wa Bukoba umetoka kuwa modernized! hai-make sense! Ni kama anachofanya unayemlalamikia!Hapana mkuu jangwani hapatanisaidia lakin kagera Imetelekezwa sana
Muanze kuonyesha mfano kujenga kwenu barabara na uwanja wa ndege vipo sasa?Bukoba hatuna chuo kikubwa cha serikali, Bukoba hakuna hadhi ya kuitwa manispaa mji umechoka sana hakuna juhudi za serikali za kuuendeleza kama miji mingine
Bukoba imekuwa kisiwa Biashara imekuwa hatari sana hakuna namna ya kufanya na wenzetu
Acha usenge. Kwani lazima ufananishe na moshi?ukabila haupo ni wajinga wachache ndio wanaochochea, wakazi wa mwanza ni kama wakazi wa Dar wamechanganyikana, tofauti na moshi 98% ni wachagga na ndio wanadhani kila mahali ni ukabila tu, wajinga sana.
Mpaka naleta Uzi uu hapa ujue kuna mantiki,Kwani vyuo vilivyopo kilimanjaro vimejengwa na serikali? sioni umuhimu wa uwanja wa kimataifa Kagera wakati wa Kigoma na Mwanza upo na pia wa Bukoba umetoka kuwa modernized! hai-make sense! Ni kama anachofanya unayemlalamikia!
Ule ulikuwa utani na uhadaaji wa wanabukoba, hakuna mpango kama uo na ni un attainableUle mpango wa Bukoba kuipuku Dubai kwa miundombinu kufikia 2017 umeishia wapi?
MwambieAcha usenge. Kwani lazima ufananishe na moshi?
Kujenga nchi kunahitaji support ya serikali
Pumbavu sana huyo. Tena ni LOFA wa hali ya juu. Yaani badala ya kutoa hoja anahara tu km bata...Mwambie
Na hii hawamu ikipita hakuna kilichofanyika itanibidi niandike kitabu dhidi ya assassination iliyofanywa na serikali dhidi ya baadhi ya mikoa hapa Tz. Sijawahi kuona mzazi anashiriki kumuangamiza mwanae wa kumzaa kama huyo mzazi si mchawi. Na sijuhi ni kwanini ilionekana kuhujumu huu mkoa kutoka mikoa mitatu kimaendeleo mpaka kuwa wa mwisho. Ni hajabu sana kuelewa hili somo lakini naamini maendeleo yaliyokuwepo hapo hawali yalikuwa ni maendeleo kwa njia za haki kabisa, sikuwahi kusikia kwamba wahaya waliingia serikalini wakaiba mali za umma ili kuendeleza kwao, ila najiuliza ilikuwaje serikali ikaamua kuhujumu maendeleo harari ya watu wake. Na mpaka leo naamini wahaya ni kati ya kabila lililotoa mchango mkubwa sana kiasi chake katika kuinua na kuendeleza hata makabila mengine. Walifungua mashule ili watoto wa wengine wasome, walikuwa waalimu na malecture wa watoto wa wengine, walipewa dhamana ya uongozi mpaka leo wakaongoza bila kuiba mali za watanzania lakini yoote hayo leo hawa watu wameharibiwa kuanzia kwa walichokuwa nacho na kuonekana maadui wa kila kundi, hata waliopitia mikononi mwao leo wanawaita maadui kwao. Any way, naamini kwa staili hii kweli hawa watu hawakustahili kuwa Tz. Kuna mambo mengi sana na historia inasema, kuwa sehemu ya Tz ni kwa bahati mbaya. Laiti ingekuwa inawezekana leo unaulizwa uzaliwe wapi ningeomba kuzaliwa ilikotokea historia yangu. Haingii akilini kuzaliwa kwa wazazi wasiokupenda, wanaokutenga na kukubagua na kukuhujumu ili ushindwe, ni bora ukazaliwa porini ukajua haukuumbwa na ndugu.Umeona hee
Dah kumbe kagera imeingizwa matatizon hivyo sasa mi naona tuwe na umoja thabiti wa kuinuanaKwani unafikiri hilo hawalijui? Wanajisemea tu kwa kutoa hoja za kipuuzi na unafiki.
Mleta mada umetoa vielelezo vinavyo onyesha kanda na Mikoa inayo pewa kipa umbele na Serikali katika masuala ya kusaidia/leta maendeleo - narudia SERIKALI hii inayo tutoza kodi alafu bila aibu inaleta upendeleo wa wazi wazi kwa kususia Mkoa wa Kagera kimaendeleo, wanaweza kutao kisingingzio gani? Watwambie kama kuna a hidden agenda ya muda mrefu ya kuudhofisha Mkoa wa Kagera - sisemi mambo ya kubuni - hapa ntatoa mifano michache ya kuonyesha uonevu uliyo pitiliza mipaka tangu tupate uhuru:
1) Kampein za kisiri siri za kudhoofisha Mkoa wa Kagera zilianza muda mrefu baada ya kupata uhuru, waanga wa kwanza ni wanafunzi wa darasa la saba - Mkoa wa Kagera uliwekewa pass mark ya 150 kwenda Sekondari wakati mikoa mengine ukipata alama 45 unakwenda Sekondari - yaani Mkoa ukuwa victimised kutokana na juhudi za wanafunzi na wazazi wao kujali elimu, yaani badala ya Serikali ya awamu ya kwanza kuwaleta walimu na baadhi ya wanafunzi kutoka Mikoa mingine kuja Mkoa wa Kagera kujifunza mbinu zinazo tumika kuwawezesha wanafunzi wengi kwenda Sekondari, wao wanabuni mbinu ya kufanya Mkoa umark time kwenye masuala ya elimu.
2) Ukatiri wa kuvunja chama cha Ushirika cha wakulima wa Kahawa, kutaifisha mali na fedha zote zilizo kuwa zimewekwa kwenye Benki ya NBC, chama hiki ndicho kilikuwa kimbilio la watu wanyonge, kilisadia sana katika masuala ya Elimu, waligharimia kila kitu mpaka wanafunzi waliokuwa wanasoma nje ya nchi. Walijenga mashule na kuweka vitega uchumi sehemu nyingi tu - kwa kifupi kilikuwa ni kichocheo kikubwa katika maendeleo ya Mkoa wa Kagera, Viongozi wa nchi wakabuni mbinu za kukisambaratisha wakati wanajua fika kwamba si chama cha SIASA, kwa nini walikuwa na wasi wasi na vyama vya Ushirika, vyama vya wafanyakazi na vyama vya Waislaam wakati ndivyo vilitoa mchango mkubwa katika harakati za kupigania uhuru!!
3) Juhudi za Mkoa wa Kagera kujiletea maendeleo zilianza muda mrefu, si watu wengi wanao lijua hilo - juhudi hizo zilikuja kuzimwa na Serikali ya awamu ya kwanza kwa kutoa visingizio mbali mbali mfano: Ni hii Project kubwa iliyokuwa itekekezwe katika mto NGONO, Serikali ya Sweden alitaka kugharimia mradi huo wa kujenga DAM karibu na daraja la Karebe - maji yangetumika kuzalisha umeme, kumwagilia commercial farms za mpunga, horticulture zikiwemo Alizeti, hiriki, vanilla na maua ya kwenda kuuzwa Ulaya - ulikuwa ni mradi mkubwa na wa maana ambao ungechochea maendeleo katika nyanja za kilimo, viwanda vidogo na vya kati kutokana na umeme wa kuaminika -wasimamizi wa mradi walikuwa ni marehemu Askofu Josiah Kibila na wenzake, hao ndio walikwenda kuomba msaada Sweden - baada ya Serikali ya awamu ya kwanza kupewa taarifa, Waziri Mkuu Edward Sokoine kaenda Bungeni na kusema Serikali ya awamu ya kwanza inajali sana Mkoa wa Kagera itagharimia mradi huo - kauli yake ndiyo ikawa mwanzo wa kauliwa mradi mzima kistaarabu - atuwezi kusema mradi ulikufa kwa bahati mbaya.
4)Mengi ya kweli kuhusu matatizo ya Mkoa wa Kagera yamekwisha zungumzwa na wenzangu labda mimi nigusie kidogo kuhusu usafiri - inashangaza kidogo kuona reli ya kati zitajengwa branch za kwenda Mpanda, Kaliua/Katavi, Rwanda, Burundi na Uganda -kwenye Project nzima Wizara ya Uchukuzi haikiwekea maanani/kumbuka Mkoa wa Kagera - awasemi chochote zaidi ya kuzungumzia reli ya Mtwara nk - Mkoa wa Kagera tutasahulika mpaka lini, wakati wa utawala wa Wajerumani walitaka kutandaza reli kwenda Bukoba sisi tunashindwa nini?
Mpango wa omukajunguti ni wa Siku nyingi
Je mnatambua kuwa serikali imeshiriki katika kuudumaza mkoa kagera?
Hivi ndivyo mkoa kagera umeachwa yatima na serikali ya Tanzania,
Tulivyopata Uhuru kagera ilikuwa miongoni mwa mikoa mitatu yenye uchumi imara,
1. Dar es salaam
2. Kagera
3. Kilimanjaro
Lakin ukweli usiopingika kagera imetelekezwa na serikali vya kutosha bila kujali majanga yaliyoikuta au michango ambayo kagera imetoa kwa watanzania.
Kila MTU kutokea kagera atakuwa anakumbukumbu zinazomfanya kusononeka sana,
SABABU MUHIMU ZILIZO SABABISHA KAGERA KURUDI NYUMA KIMAENDELEO
1. VITA YA KAGERA, 1978/79
Vita ya nchi nzima ilipuganwa kwenye mkoa mmoja na kuharibu miundombinu vya kutosha , na ule ndo ulikuwa uwanja qa vita hasa, lakin hakuna sehem yeyote kuna strategy za kuujenga upya mkoa, tunaishia kusikia maneno ya kashfa tu tena toka kwa viongozi wakubwa kwa wanakagera eti mmeshindwa kujenga hata chuo kikuu kimoja? Aliuliza kikwete lakin kasahau kuwa yeye kama mkuu qa serikali hajajenga hata chuo cha kutoa cheti,
2. JANGA LA UKIMWI 1983,
Kama inavyojulikana kagera iko mpakani mwa Uganda, na UKIMWI umeanzia Uganda, na kwakuwa wana Kagera wanautaratibu wa kufanya Biashara na Uganda , haikukwepeka kupata UKIMWI, nguvu Kazi kubwa ilipotea sana miaka hiyo na kusababisha uchumi kurudi nyuma,
3. AJALI YA MV BUKOBA
janga LA pili ambalo linafanya kudhoofisha mkoa wa kagera ni kuwa , watoto wengi yatima wameongezeka , nguvu kazi imepungua kutokana na ajari ile,
4.1998 EL NINO
Hii wengi mnaelewa kuwa imekumba sana ukanda wa kanda ya ziwa kuliko kanda yeyote ile hapa nchini , imeharibu miundombinu na kupoteza wazalishaji Mali,
5. KUSHUKA KWA BEI YA KAHAWA 1998 KWA UZEMBE WA SERIKALI.
Inajulikana kagera ilitegemea sana Kahawa kama kitega uchumi , kwa uzembe wa serikali hakukuwepo utaratibu wa kuhakikisha Kahawa inabaki na bei ya kuridhisha badala yake ikapuuza mpaka wananchi wakakata mibuni maana haikuwa na maana tena,
6. UBAGUZI ULIOJIFICHA TOKA KWA VIONGOZI ( INDIRECT DISCRIMINATION TOWARDS HAYA TRIBE)
Miaka ya nyuma hakuna ambaye hajui kuwa wahaya waliwekewa mizengwe katika baadhi ya sekta, hata kwenye elimu , walipandishiwa alama za ufauru ili wachache waendelee na elimu ya juu maana walionekana kuwa wao ndo wanafauru na kujaza madarasa mengine, lakin ili kuitamka sentensi hii (INAHITAJI UJIFANYE MWENDA WAZIMU KIDOGO)
7. KUTENGWA NA NCHI KIJIOGRAFIA
kagera iko kaskazini magharibi mwa Tanzania, waliowahi kufika uko ndio wanaelewa namaanisha nini, Kagera imekuwa kama kisiwa maana jinsi ya kufika kule inabidi ukatishe kilometer kadhaa za msitu, ili uingie kagera, au upite ziwani kwa meli ndo uende mikoa mingineyo ambayo ni ya Tanzania, hivyo basi wana Kagera walikuwa na urahisi wa kufanya Biashara na Uganda kuliko mikoa mingine ya Tanzania, lakin serikali ilikataza biashara hiyo , wakajikuta wamebaki kama kisiwa ndani ya nchi yao wenyewe,
8.KAGERA KIMBILIO LA WAKIMBIZI MAUAJI YA KIMBALI YA RWANDA 1994 NA MACHAFUKO TANAYOENDELEA UKANDA ULE.
Wanyarwanda wameiteka kagera hasa wilaya ya Karagwe na Muleba na kujichukulia ardhi , pia wamekuwa watekaji wa magari na kudhalilisha wana kagera , kitu amabacho kimerudisha nyuma uchumi wa mkoa, kwa kasi, majambazi wametamalaki na kufanya uharamia ambao umefanya kusiwepo hali ya utulivu na kujenga uchumi, serikali imechelewa kuchukua hatua,
9. KUTOJUMUISHWA KATIKA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO KIKANDA
kila kanda imetengwa katika kanda fulan ya mkakati wa maendeleo lakin kanda ya ziwa ambayo ndipo kuna mkoa Kagera hakuna ilipoainishwa katika mpango wa maendeleo.
Kagera Umekuwa ni mkoa wa kujitegemea kwa kila kitu utasikia
Ukumbi wa mkutano unajengwa arusha, sijui chuo cha utalii dar, chuo cha ufugaji Tabora.
Chuo cha reli tabora, chuo cha science cha nelson Mandela arusha,
Chuo cha serikari cha ugavi
Chuo cha ushirika Moshi Mara..
Chuo cha mbao iringa, kwanini kagera hakuna mipango endelevu, sasa upo wapi uwanja wa mukajunguti wa ndege na ulishaahidiwa kuwa wa kimataifa n kutengewa bajet kipindi cha mkapa?,Rais Magufuli halioni ilo?
Kagera wanekuwa wa kupandia kama daraja, kikwete kaenda bukoba katoa ahadi ambayo imerudiwa na Magufuli sana, eti ntawapa meli ,mbona hata mtumbwi haujaweka,
We unayesoma hapa nitajie chuo chochote kilichojengwa na serikali kuazia cheti mpaka degree, imekjwa vipaumbele kujenga Dodoma na mnasahau kuna deni kagera inadai kwa taifa Ili,
Kilichosaidia kagera ni vishirika vya wazungu tu kama partage, world vision, gses, yaan serikali haijatenda haki uko,
SOMA HII SASA SERIKALI INA KITU KINAITWA SUBJECTIVE AND OBJECTIVE PLANNINGS,(BIG FOUR REGIONS) IKO HIVI
1.KANDA YA KUSINI AU NYANDA ZA JUU KUSINI
Imetengwa kama kanda ya kilimo hapa kuna mikoa
Njombe
Mbeya
Katavi
Ruvuma
Na Iringa .
2.KANDA NYINGINE KANDA YA KASKAZINI
Hii imeahinishwa na kupewa kipaumbele kama kanda ya utalii,
Mikoa ni
Arusha,
Kilimanjaro na Manyara,
3.NYINGINE NI KANDA YA KATI ,
Taasisi za siasa na Elimu ya juu
Mikoa ni
Morogoro,
Dodoma,
Singida,
4. KANDA YA MASHARIKI INEPEWA Kanda ya viwanda na Biashara, mikoa ni
Dar es salaam,
Mtwara
Lindi
Pwani
Tanga
KANDA YA ZIWA ANBAYO KUNA KAGERA IKO WAPI, ?
Sasa inafika hatua tunapaswa kuusema ukweli ,
Mheshimiwa rais huu ulikuwa ninwakati wa Kujenga MUKAJUNGUTI INTERNATIONAL AIRPORT SIYO CHATO. TUNGEPOZWA ANGALAU NA UWANJA UO MAANA TUMESUBIRI NEEMA KWA MIAKA MINGI LAKIN WAPI
Wengi watasema umejenga uko kwakuwa ni kwenu, lakini pia hata KAGERA KARAGWE NI KWENU KWA MZEE MACHALILA, NA JINA LAKO LA KIHAYA NI KATO (wengi hawajui hii), sasa kama ndo sababu ya kujenga nyumbani anza nyumbani ambapo pako kwenye mipango ya Siku nyingi,
Kajunguti International Airport - Wikipedia, the free encyclopedia
Acha uongo, wamekafuta lini wakati wamebadili jina na kuita CARUMUCO. Nipo Kagera na chuo kipo hai.Hako ka tawi wamekafuta