Kwanini Chato International Airport na si Omukajunguti international Airport? Kagera inaonewa sana

Kwanini Chato International Airport na si Omukajunguti international Airport? Kagera inaonewa sana

Mkuu umeongea jambo la msingi sana sana ila umeharibu sana kitu kimoja, kuutaja mkoa wa Kagera. Ukiutaja mkoa huu utashambuliwa na hata yule asiye na meno. Yawezekana tulipata bahati mbaya kuwa watanzania, naamini huu mkoa ungekuwa Uganda ingekuwa ni jambo jema zaidi kuliko ilivyo leo, ubaguzi ni mkubwa sana hapa Tz dhidi ya mkoa huu.i
Samahani mkuu, sidhani kama kuna mkoa wenye watu wabaguzi kama mkoa wa Kagera. Wao wanaona fahari kubagua wengine lakini wakiona wanabaguliwa wanalalamika. Kagera mpaka stendi wapiga debe wanauga debe kihaya tena stendi ya mkoa. Kila sehemu ukiingia ni kihaya, ukiwa na lafudhi tofauti na kihaya unapandishiwa gharama ya vitu madukani na hata bodaboda/sekido. Ukiwa Kagera huwezi kutofautisha mjini na kijijini.Mnaweza kuwa makabila mawili au matatu bado jamaa wakaendelea kuchapa kilugha chao bila kujali,mbaya zaidi wakijua kuwa husikii kihaya watakusema mpaka basi. Kwa ubaguzi badilikeni. Kuhusu maendeleo wilaya zenu zote zimeunganishwa kwa lami, mna maji,mna uwanja wa ndege mzuri tu.
 
Sadoku inawezekana kana suala MV Bukoba isiwe ishu ila Suala la Vita ya Kagera ilipiganwa wapi, battle field ilikuwa Kagera ilikuwa na direct impact katika uchumi wa Kagera, suala la Ukimwi ni janga la Kitaifa na kidunia na kwakuwa lilichukua nguvu kazi kubwa ya watu wa huko huwezi kupuuza kwa madai kwamba si serikali tena eti ukitukana. Hapa hoja ni majanga yaliyoikumba Kagera. Nakumbuka Risala ya Mzee Philip Mangula kwa Mkapa wakati huo akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera haya mawili yalikuwa kati ya majanga aliyataja. Ni kweli pia zao la Kahawa limeshuka bei sana na wananchi wa Kagera walizuiwa kuuza Uganda ambako kuna soko zuri, migomba imekumbwa na Ugonjwa wa Mnyauko hakuna tena ndizi zilizojulikana kama ndizi za Bukoba, Mihogo kwa upande wa mkoa huu umekumbwa na ugonjwa wa Bato Bato mihogo inaharibika kabla hata haijaweka mzizi ndani. Hivyo si sahihi kutumia lugha uliyoitumia na nadhani umeongozwa na ushabiki labda wa kisiasa tu. Na mimi niseme kabisa matatizo ya Kagera si kukosa uwanja wa ndege, hapana kuna matatizo ambayo nimeyataja hapo juu ambayo serikali inapaswa kuwasaidia wananchi wa mkoa huu.
 
Ni kweli mkoa wa kagera ni kama umetengwa kagera kuna kila kitu kizuri aridhi yenye lutuba, hali ya hewa nzuri, umeme wa uhakika, na watu wake wameelimika sana, na katika dini wapo vizuri (kuna wakati makanisa makubwa hapa TZ yaani RC na KKKT kwa wakati mmoja yoote yalikuwa yanaongozwa na wahaya)Rugambwa na Dr Mushemba, lkn cha kushangaza ulianzishwa mchakato wa kumtangaza kiongozi wa kisiasa kuwa mwenyeheri akaachwa karidinali wa kwanza mwausi........
Hili ndilo linalowaangusha,la kutaka kujiinua. Ardhi nzuri lakini wakazi wake wengi ni wavivu hata wa kulima mchicha. Utofauti ni Karagwe tu ambapo watu ni wachapa kazi na hulima mpaka kwenye mawe.
 
Umeielewa sana post yangu? Background ya matatizo ya mbeya na kagera ni tofauti
Mbeya kuliwahi kutwishwa mzigo wa vita wa taifa zima?
Mbeya kuliwahi kuwa kimbilio la wakimbizi tena ambao wamekuja na silaha Kali? Na kuanza uporaji? Mbeya iliwahi kukandamizwa na serikali kama ambavyo kagera wanakandamizwa? Najiuliza vipi mwaka 1963 makatibu wakuu wahaya 24 waliopigwa chini wakabaki watatu makusudi?

Hapa ni makosa yalifanyika inabidu ukweli tuukubali kabisa.
Mkuu wahaya wangejazana maofisini wao tu na kuacha makabila mengine yakisota nje. Hospitali za Kagera zimejaa Wahaya, Ofisi za Kagera zimejaa wahaya na 'Lingua Franca" yao ni Kihaya tu. Jifunze kuitetea Tanzania na sio kutetea ukabila.
 
Unaposema Mwanza unamaanisha nani kajenga ule mji? Wasukuma?. Hebu acha kuchekesha Sadoku, Wakinga waliojenga Bwiru na Kapripointi ni ya nao ni wenyeji wa Mwanza?, Sema kwingine si Mwanza, tumenunua maeneo ya wasukuma kwa wingi wao wakikimbia mji, sasa unaowasema wamejenga jiji ni kina nani hao
 
Maendeleo mengine ya mikos umeijumuisha kikanda.. Ila unataka Kagera ipewe kipaumbele kama mkoa na siyo kama sehemu ya kanda ya ziwa. Acha ubinafsi
 
Najua ulichomaanisha ila mi nakumbushia OMUMAJUNGUTI INTERNATIONAL AIRPORT, Nakumbushia kwanini hakuna mikakati ya kuendeleza mkoa kagera, kwanini hakuna uwekezaji wa serikali, AU BADO MNABALANCE EQUATION KWA KUWAVUTA CHINI WAHAYA LABDA
Mkuu hizo ndege za kwenda huko zitatoka wapi maana Bukoba Airpot ni nzuri lakini haiko busy?.
 
Nchi hii upendeleo wa kieneo upo sana na inanishangaza sana. Hebu fikiria Duka kubwa la Dawa la MSD limejengwa karibu na Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa katika jimbo la Waziri Mkuu kisha tunaambiwa kwamba Hospitali ya Rufaa ya Mtwara itakuwa inafuata dawa Ruangwa na Waziri Mkuu anasema limejengwa huko sababu ndiko katikati baina ya Lindi Manispaa, Mtwara Manispaa, Newala, nk. Kuna hatari sana kwa nchi kuongozwa kwa kujipendelea. Hata bandari ya Bagamoyo jk alichelewa kuanzisha ujenzi wake tu ni bahati mbaya kwa watu wa bagamoyo.
Hehehehehehe[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Samahani mkuu, sidhani kama kuna mkoa wenye watu wabaguzi kama mkoa wa Kagera. Wao wanaona fahari kubagua wengine lakini wakiona wanabaguliwa wanalalamika. Kagera mpaka stendi wapiga debe wanauga debe kihaya tena stendi ya mkoa. Kila sehemu ukiingia ni kihaya, ukiwa na lafudhi tofauti na kihaya unapandishiwa gharama ya vitu madukani na hata bodaboda/sekido. Ukiwa Kagera huwezi kutofautisha mjini na kijijini.Mnaweza kuwa makabila mawili au matatu bado jamaa wakaendelea kuchapa kilugha chao bila kujali,mbaya zaidi wakijua kuwa husikii kihaya watakusema mpaka basi. Kwa ubaguzi badilikeni. Kuhusu maendeleo wilaya zenu zote zimeunganishwa kwa lami, mna maji,mna uwanja wa ndege mzuri tu.
Wewe unaonekana hutembei upo labda Dar au wapi sijui. Ngoja nikwambie Mimi nilikwenda kufundisha Chuo Kimoja MTWARA, nilipofika pale nikaenda kununua Feni na vifaa vya ndani, feni niliyoambiwa ni elfu sabini, alipokuja mtu mwenye lafudhi ya N badala ya M nikaona anaibeba kwa 35,000/ kumwambia nipunguzie, nikaambiwa kanunue na wewe uje uuze ili upunguze bei. Nikadhani ni hapo tu, nikaenda kununua samaki pwani/ Ferry nikapigwa bei hatari, nikapewa ujanja kwamba samaki uliyemnunua elfu kumi wewe mpe mtu wa mtwara elfu tano tu atakuja nayo bila shida. Sikuishia hapo nikaenda kumtembelea rafiki yangu anafanyakazi benki Newala. Kufika kule nikakuta analia ubaguzi wa hivyo hivyo, kiasi kwamba alipotaka kufungua duka la nguo ilibidi amtumie rafiki yake mwenyeji wa huko ili ionekane anaandaa ile fremu ili akiweka nguo zile ziweze kununuliwa. Hali hii niliikuta Ruangwa pia kwa Hakimu mmoja niliyekutana naye huko yeye akiwa mtu wa mbeya, alilalamikia hali hii. Inawezekana na Bukoba kuna ubaguzi lakini sidhani kama ni wa kiasi cha Mtwara na Lindi.
 
Umenikumbusha mbali aise nifkiria nyumban nahis choz linadondoka
 
Unakuja kulialia hapa eli ninyo ilinyesha kwenu tu?ukimwi nao ni serikali?mv bukoba iliua watu lakhi ngap toka kagera?ninyi ni wapuuzi sana.si ndo huwa mnajisifu ujinga?kwenu hamjengi na hamkai mnakaa kujifu sifa za kijinga. Angalieni kwa wenzenu mbeya,arusha,knjaro na mwanza.

Ninyi mnakaa kujisifia sifa za kijinga wakati mkoa wenu ni mmoja ya mikoa iliyochoka.mnasema ninyi wasomi na mna pesa.haya mnajenga wapi sasa.
Namsaidia mleta mada MV bukoba iliua 80% ya wakazi wa Bukoba ambao ukienda mnalan majina yapo japo mengine ya ambao hawakupatikana hayapo,
Hivyo madhara yake ni haya
1. Wazakishaji walipungua
2. Wameacha watoto wengi yatima ambao wanahitaji kulelewa
3. Meli ile kama kitega uchumi, haipo tena, hawana kifaa kama kile tena
Hivyo ukae ukijua kuwa meli ile INA impact kubwa

Suala LA ukimwi, monster, kilikuwa ni jambo geni na serikali ilikuwa haijaingilia sana kudhibiti maana ulikuwa haujapatikana popote pale, mwaka 1983 hospital ya ndolage ndo ya kwanza kupima MTU MWENYE ukimwi na hawakujua nini , sasa kwanza watu wengi walioathirika na janga ili mwanzon na kuacha yatima wengi ni kagera, ukimwi ukaja kusambaa kwingine serikali imeshajidhatiti,
 
Mpango wa omukajunguti ni wa Siku nyingi

Je mnatambua kuwa serikali imeshiriki katika kuudumaza mkoa kagera?
Hivi ndivyo mkoa kagera umeachwa yatima na serikali ya Tanzania,
Tulivyopata Uhuru kagera ilikuwa miongoni mwa mikoa mitatu yenye uchumi imara,

1. Dar es salaam
2. Kagera
3. Kilimanjaro

Lakin ukweli usiopingika kagera imetelekezwa na serikali vya kutosha bila kujali majanga yaliyoikuta au michango ambayo kagera imetoa kwa watanzania.

Kila MTU kutokea kagera atakuwa anakumbukumbu zinazomfanya kusononeka sana,

SABABU MUHIMU ZILIZO SABABISHA KAGERA KURUDI NYUMA KIMAENDELEO

1. VITA YA KAGERA, 1978/79
Vita ya nchi nzima ilipuganwa kwenye mkoa mmoja na kuharibu miundombinu vya kutosha , na ule ndo ulikuwa uwanja qa vita hasa, lakin hakuna sehem yeyote kuna strategy za kuujenga upya mkoa, tunaishia kusikia maneno ya kashfa tu tena toka kwa viongozi wakubwa kwa wanakagera eti mmeshindwa kujenga hata chuo kikuu kimoja? Aliuliza kikwete lakin kasahau kuwa yeye kama mkuu qa serikali hajajenga hata chuo cha kutoa cheti,

2. JANGA LA UKIMWI 1983,
Kama inavyojulikana kagera iko mpakani mwa Uganda, na UKIMWI umeanzia Uganda, na kwakuwa wana Kagera wanautaratibu wa kufanya Biashara na Uganda , haikukwepeka kupata UKIMWI, nguvu Kazi kubwa ilipotea sana miaka hiyo na kusababisha uchumi kurudi nyuma,

3. AJALI YA MV BUKOBA
janga LA pili ambalo linafanya kudhoofisha mkoa wa kagera ni kuwa , watoto wengi yatima wameongezeka , nguvu kazi imepungua kutokana na ajari ile,

4.1998 EL NINO
Hii wengi mnaelewa kuwa imekumba sana ukanda wa kanda ya ziwa kuliko kanda yeyote ile hapa nchini , imeharibu miundombinu na kupoteza wazalishaji Mali,

5. KUSHUKA KWA BEI YA KAHAWA 1998 KWA UZEMBE WA SERIKALI.
Inajulikana kagera ilitegemea sana Kahawa kama kitega uchumi , kwa uzembe wa serikali hakukuwepo utaratibu wa kuhakikisha Kahawa inabaki na bei ya kuridhisha badala yake ikapuuza mpaka wananchi wakakata mibuni maana haikuwa na maana tena,

6. UBAGUZI ULIOJIFICHA TOKA KWA VIONGOZI ( INDIRECT DISCRIMINATION TOWARDS HAYA TRIBE)
Miaka ya nyuma hakuna ambaye hajui kuwa wahaya waliwekewa mizengwe katika baadhi ya sekta, hata kwenye elimu , walipandishiwa alama za ufauru ili wachache waendelee na elimu ya juu maana walionekana kuwa wao ndo wanafauru na kujaza madarasa mengine, lakin ili kuitamka sentensi hii (INAHITAJI UJIFANYE MWENDA WAZIMU KIDOGO)

7. KUTENGWA NA NCHI KIJIOGRAFIA
kagera iko kaskazini magharibi mwa Tanzania, waliowahi kufika uko ndio wanaelewa namaanisha nini, Kagera imekuwa kama kisiwa maana jinsi ya kufika kule inabidi ukatishe kilometer kadhaa za msitu, ili uingie kagera, au upite ziwani kwa meli ndo uende mikoa mingineyo ambayo ni ya Tanzania, hivyo basi wana Kagera walikuwa na urahisi wa kufanya Biashara na Uganda kuliko mikoa mingine ya Tanzania, lakin serikali ilikataza biashara hiyo , wakajikuta wamebaki kama kisiwa ndani ya nchi yao wenyewe,

8.KAGERA KIMBILIO LA WAKIMBIZI MAUAJI YA KIMBALI YA RWANDA 1994 NA MACHAFUKO TANAYOENDELEA UKANDA ULE.
Wanyarwanda wameiteka kagera hasa wilaya ya Karagwe na Muleba na kujichukulia ardhi , pia wamekuwa watekaji wa magari na kudhalilisha wana kagera , kitu amabacho kimerudisha nyuma uchumi wa mkoa, kwa kasi, majambazi wametamalaki na kufanya uharamia ambao umefanya kusiwepo hali ya utulivu na kujenga uchumi, serikali imechelewa kuchukua hatua,

9. KUTOJUMUISHWA KATIKA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO KIKANDA
kila kanda imetengwa katika kanda fulan ya mkakati wa maendeleo lakin kanda ya ziwa ambayo ndipo kuna mkoa Kagera hakuna ilipoainishwa katika mpango wa maendeleo.
Kagera Umekuwa ni mkoa wa kujitegemea kwa kila kitu utasikia

Ukumbi wa mkutano unajengwa arusha, sijui chuo cha utalii dar, chuo cha ufugaji Tabora.

Chuo cha reli tabora, chuo cha science cha nelson Mandela arusha,
Chuo cha serikari cha ugavi
Chuo cha ushirika Moshi Mara..

Chuo cha mbao iringa, kwanini kagera hakuna mipango endelevu, sasa upo wapi uwanja wa mukajunguti wa ndege na ulishaahidiwa kuwa wa kimataifa n kutengewa bajet kipindi cha mkapa?,Rais Magufuli halioni ilo?

Kagera wanekuwa wa kupandia kama daraja, kikwete kaenda bukoba katoa ahadi ambayo imerudiwa na Magufuli sana, eti ntawapa meli ,mbona hata mtumbwi haujaweka,

We unayesoma hapa nitajie chuo chochote kilichojengwa na serikali kuazia cheti mpaka degree, imekjwa vipaumbele kujenga Dodoma na mnasahau kuna deni kagera inadai kwa taifa Ili,

Kilichosaidia kagera ni vishirika vya wazungu tu kama partage, world vision, gses, yaan serikali haijatenda haki uko,

SOMA HII SASA SERIKALI INA KITU KINAITWA SUBJECTIVE AND OBJECTIVE PLANNINGS,(BIG FOUR REGIONS) IKO HIVI

1.KANDA YA KUSINI AU NYANDA ZA JUU KUSINI
Imetengwa kama kanda ya kilimo hapa kuna mikoa
Njombe
Mbeya
Katavi
Ruvuma
Na Iringa .

2.KANDA NYINGINE KANDA YA KASKAZINI
Hii imeahinishwa na kupewa kipaumbele kama kanda ya utalii,
Mikoa ni
Arusha,
Kilimanjaro na Manyara,

3.NYINGINE NI KANDA YA KATI ,
Taasisi za siasa na Elimu ya juu
Mikoa ni
Morogoro,
Dodoma,
Singida,

4. KANDA YA MASHARIKI INEPEWA Kanda ya viwanda na Biashara, mikoa ni
Dar es salaam,
Mtwara
Lindi
Pwani
Tanga

KANDA YA ZIWA ANBAYO KUNA KAGERA IKO WAPI, ?
Sasa inafika hatua tunapaswa kuusema ukweli ,

Mheshimiwa rais huu ulikuwa ninwakati wa Kujenga MUKAJUNGUTI INTERNATIONAL AIRPORT SIYO CHATO. TUNGEPOZWA ANGALAU NA UWANJA UO MAANA TUMESUBIRI NEEMA KWA MIAKA MINGI LAKIN WAPI

Wengi watasema umejenga uko kwakuwa ni kwenu, lakini pia hata KAGERA KARAGWE NI KWENU KWA MZEE MACHALILA, NA JINA LAKO LA KIHAYA NI KATO (wengi hawajui hii), sasa kama ndo sababu ya kujenga nyumbani anza nyumbani ambapo pako kwenye mipango ya Siku nyingi,
Kajunguti International Airport - Wikipedia, the free encyclopedia
Pole sana kwasababu watu wa mikoa mingine wataona umeongea pumba tu.
 
Wewe unaonekana hutembei upo labda Dar au wapi sijui. Ngoja nikwambie Mimi nilikwenda kufundisha Chuo Kimoja MTWARA, nilipofika pale nikaenda kununua Feni na vifaa vya ndani, feni niliyoambiwa ni elfu sabini, alipokuja mtu mwenye lafudhi ya N badala ya M nikaona anaibeba kwa 35,000/ kumwambia nipunguzie, nikaambiwa kanunue na wewe uje uuze ili upunguze bei. Nikadhani ni hapo tu, nikaenda kununua samaki pwani/ Ferry nikapigwa bei hatari, nikapewa ujanja kwamba samaki uliyemnunua elfu kumi wewe mpe mtu wa mtwara elfu tano tu atakuja nayo bila shida. Sikuishia hapo nikaenda kumtembelea rafiki yangu anafanyakazi benki Newala. Kufika kule nikakuta analia ubaguzi wa hivyo hivyo, kiasi kwamba alipotaka kufungua duka la nguo ilibidi amtumie rafiki yake mwenyeji wa huko ili ionekane anaandaa ile fremu ili akiweka nguo zile ziweze kununuliwa. Hali hii niliikuta Ruangwa pia kwa Hakimu mmoja niliyekutana naye huko yeye akiwa mtu wa mbeya, alilalamikia hali hii. Inawezekana na Bukoba kuna ubaguzi lakini sidhani kama ni wa kiasi cha Mtwara na Lindi.
Mkuu Kagera nimeitembea sehemu kubwa, sipo Dar kama unavyofikiria. Binafsi sijawahi kufika Mtwara ila niliambiwa issue ga ubaguzi ipo kama ilivy kwa Kagera. Pole kwa yaliyokukuta Mtwara mkuu. Karibu sana Bunazi, Rugu, Muleba, Kagondo, Omurushaka nk.
 
Namsaidia mleta mada MV bukoba iliua 80% ya wakazi wa Bukoba ambao ukienda mnalan majina yapo japo mengine ya ambao hawakupatikana hayapo,
Hivyo madhara yake ni haya
1. Wazakishaji walipungua
2. Wameacha watoto wengi yatima ambao wanahitaji kulelewa
3. Meli ile kama kitega uchumi, haipo tena, hawana kifaa kama kile tena
Hivyo ukae ukijua kuwa meli ile INA impact kubwa

Suala LA ukimwi, monster, kilikuwa ni jambo geni na serikali ilikuwa haijaingilia sana kudhibiti maana ulikuwa haujapatikana popote pale, mwaka 1983 hospital ya ndolage ndo ya kwanza kupima MTU MWENYE ukimwi na hawakujua nini , sasa kwanza watu wengi walioathirika na janga ili mwanzon na kuacha yatima wengi ni kagera, ukimwi ukaja kusambaa kwingine serikali imeshajidhatiti,
Mkuu,hivi MV Bukoba iliua watu wangapi mpaka irudishe nyuma maendeleo ya Kagera kwa miaka 20? Majanga mengine nakubali lakini hili hapana.
 
Mpaka naleta Uzi uu hapa ujue kuna mantiki,
Angalia hivyo vya Kilimanjaro vimejengwaje na kwanini,
Je una fununu zozote juu ya kuanzishwa kwa UNIVERSITY OF BUKOBA? mwaka 1995 na unajua nini kilivuruga mpango uo? Fanya research za kutosha
tatizo huongei ukweli chuo cha Ushirika hakikuanzishwa na serikali!
 
Mwenye macho ahambiwi tazama kupitia michango ya baadhi ya watu hapa unapata kuona watu wanavyozidisha chuki dhidi ya wahaya bila kujibu hoja, mleta mada ameainisha kero za msingi zinazochangia mkoa Wa Kagera kurudi nyuma kimaendeleo na akionyesha tatizo lilipo katika vipaumbele vya serikali kwa baadhi ya Kanda.

Na huu ndio ukweli mtupu, serikali inatakiwa kijitafakari kuhusi ukanda huu.
 
Hapo umenena
 
Mkuu,hivi MV Bukoba iliua watu wangapi mpaka irudishe nyuma maendeleo ya Kagera kwa miaka 20? Majanga mengine nakubali lakini hili hapana.
Watu mianane na zaidi, na wafanya Biashara, kwanza MV Bukoba usiiangalie katika ufinyu angalia madhara kwa ujumla
Athari za watoto yatima unazijua?
Athari za kukosekana kwa MV Bukoba kiuchumi unazijua?
 
Back
Top Bottom