Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Kwani hao viongozi walioko juu wanatoka mbinguni mkuu?siwanatoka miongoni mwa jamii yetu?

Tatizo la waafrica Sio uongozi bali ni mfumo wa kifkira kwenye jamii yetu ,na ndio maana mtu utamkuta anapiga kelele kuhusu ufisadi lakini akipewa nafasi ya uongozi badala ya kuondoa huo ufisadi alio kuwa anaupigia kelele yeye ndo anaenda kuwa fisadi mara 10 ya aliye mtangulia.
Sasa hivi mfano chadema akachukua nchi nakuhakikishia hakuna chochote kitakacho badilika ndani ya nchi hii.
Ni kweli, kubadilika lazma tubadilishe mfumo wa utoaji haki. Adhabu zikiwa kali hamna mtu atasogelea rushwa.
 
Uongo hakuna kitu kama hicho.....!! Kwa watu ambao tayari mko brainwashed na western ideologies ndio mtaamini hivyo
Kila binadamu mwenye akili timamu anataka freedom of speech, mahakama huru, uhuru wa imani na kuchagua watu wa kumuongoza katika uchaguzi uhuru.
Hata wewe unapenda haya kama una akili timamu.
 
Kuna udikteta wa kichama na hapo ndipo China alipo Xi anaweza asiwe na nguvu yoyote lakini chama cha kikomunisti kikawa kimehodhi nguvu zote
same as US, state department na Pentagon wamehodhi nguvu zote,..... au tuseme MIC wamehodhi nguvu zote kiasi raisi wa nchi hana kauli kwao!

kifupi kila nchi ina aina yake ya utawala ambapo ukichunguza utagundua kuna elements za udikteta!
 
Unaelewa majukumu ya State Department na Pentagon?
Unaelewa majukumu ya chama cha Kikomunisti cha China(CCP)??
 
China walipata bahati ya kumpata mzee mmoja anaitwa Deng Xiaoping. Huyo ndio chanzo HALISI cha mafanikio ya China. Hayo mengine ni mengineyo. Bila huyo mzee, China ingekuwa nchi maskini kama nchi zingine.

Kamgugo Deng Xiaoping
Huyo mzee ndio alisuka kila kitu China wanamuita the Architect of modern China. Marais Baada yake walifuata njia yake, alifuata Jiang Zemin akaboresha kisha akafuaya Hu Jintao na sasa hivi Xi Jinping.
 
Kwa ufupi tu China waliligundua hili miaka mingi sana kuwa demokrasia sio kichocheo halisi Cha maendeleo hususani kwa taifa ambalo Bado linajitafuta.

Miaka ya 1950s mpaka 1970s mzee Mao alikuja na campaign maalimu ya GLF(Great Leap Forward) ambayo ililenga kuitrasnform China kutoka kwenye agrian economy na kuipeleka kwenye uchumi wa viwanda, campaign ambayo iligharimu mamilioni ya maisha wa wachina, watu walikufa sana na njaa na Mao alipata wapingaji wengi sana. Lakin wapingaji hao hawakuwa na nguvu sababu hapakuwepo na demokrasia ya kimagharibi.

Kwa kipindi chote hicho hawakuendekeza siasa za kidemokrasia uchwara, ilikuwa ni mwendo wa KUPIGA kazi tu, muda wa kupigana majungu na kukosoana kukosoana kiholela mara sijui purukushani za uchaguzi haukuwepo, waliamini katika maono ya Mao Zedong na baadae kupokelewa kijiti na Dieng Xiaoping. Mpaka leo hii wamefika hapo waliopo ni vision na uwajibikaji na Wala sio siasa za demokrasia.

Wachina hawaamini Kwenye utawala wa kubadilisha badilisha viongozi kuwa eti ndio chachu ya kupata maendeleo kwa haraka, wao wanaamini kwenye utawala Bora unaozingatia katiba ambayo inaweza ikamuwajibisha mtu yoyote pale anapoikiuka.

Na ndio maana leo hii wameamua kumfanya Xi Jinping kuwa raisi wa kudumu, sababu Wanaamini katika maono yake na pia hawana wasi wowote kuhusu yeye maana katiba yao ni Bora na ipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya China.
 
Kila binadamu mwenye akili timamu anataka freedom of speech, mahakama huru, uhuru wa imani na kuchagua watu wa kumuongoza katika uchaguzi uhuru.
Hata wewe unapenda haya kama una akili timamu.
Kila binadamu mwenye akili timamu anapenda maendeleo kwa maana ya upatikanaji wa huduma zote za msingi kwanzia yeye mwenyewe na vizazi vijavyo.

Na hili kuwezekana sio lazima uishi kwenye demokrasia.

Na Zaid ya hapo mwenye akili timamu hapendi kabisa political Chaos ya aina yoyote, na of course mara nyingi political chaos utaikuta Zaid kwa waendelekeza demokrasia.
 
Kwa ufupi tu China waliligundua hili miaka mingi sana kuwa demokrasia sio kichocheo halisi Cha maendeleo hususani kwa taifa ambalo Bado linajitafuta.

Miaka ya 1950s mpaka 1970s mzee Mao alikuja na campaign maalimu ya GLF(Great Leap Forward) ambayo ililenga kuitrasnform China kutoka kwenye agrian economy na kuipeleka kwenye uchumi wa viwanda, campaign ambayo iligharimu mamilioni ya maisha wa wachina, watu walikufa sana na njaa na Mao alipata wapingaji wengi sana. Lakin wapingaji hao hawakuwa na nguvu sababu hapakuwepo na demokrasia ya kimagharibi.

Kwa kipindi chote hicho hawakuendekeza siasa za kidemokrasia uchwara, ilikuwa ni mwendo wa KUPIGA kazi tu, muda wa kupigana majungu na kukosoana kukosoana kiholela mara sijui purukushani za uchaguzi haukuwepo, waliamini katika maono ya Mao Zedong.

Wachina hawaamini Kwenye utawala wa kubadilisha badilisha viongozi kuwa eti ndio chachu ya kupata maendeleo kwa haraka, wao wanaamini kwenye utawala Bora unaozingatia katiba ambayo inaweza ikamuwajibisha mtu yoyote pale anapoikiuka.

Na ndio maana leo hii wameamua kumfanya Xi Jinping kuwa raisi wa kudumu, sababu Wanaamini katika maono yake na pia hawana wasi wowote kuhusu yeye maana katiba yao ni Bora na ipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya China.
Wachina hawajawahi kugundua miaka mingi kwamba demokrasia sio kichocheo cha maendeleo, China haijawahi kufikiria hata suala la demokrasia. Kwa miaka 2000 mpaka mwaka 1912 China ilikuwa inatawaliwa na Emperors, baada ya utawala wa emperors kuanguka ikaanza kutawaliwa kama jamuhuri chini ya mtawala wa kijeshi, mwaka 1959 Wakomunisti ndipo wakauipindua utawala uliokuwepo baada ya vita vya muda mrefu.

Pamoja na kutokuwa nchi ya kidemokrasia baada ya Mao China imekuwa ikibadilisha viongozi mara kwa mara na katiba yao waliweka ukomo wa miaka 10 japo ni chini ya chama kimoja. Maendeleo makubwa China iliyopata na kuweka msingi wa sasa wa uchumi ni wakati wa Deng Xiaoping. Huyu Xi amekuta uchumi wa China tayari unafanya vizuri sana akajijengea umaarufu halafu juu ya ule udikteta wa kichama akijitengenezea cult of personality. Viongozi waliomtangulia walikitanguliza mbele zaidi chama ndio maana hawakuwa maarufu kama yeye ila sio kwamba eti yeye ana miujiza kuliko wengine waliomtangulia.
 
Kila binadamu mwenye akili timamu anapenda maendeleo kwa maana ya upatikanaji wa huduma zote za msingi kwanzia yeye mwenyewe na vizazi vijavyo.

Na hili kuwezekana sio lazima uishi kwenye demokrasia.

Na Zaid ya hapo mwenye akili timamu hapendi kabisa political Chaos ya aina yoyote, na of course mara nyingi political chaos utaikuta Zaid kwa waendelekeza demokrasia.
Wachina wengi wanakimbilia kuishi na kuwa wakazi Marekani lakini ni nadra kukuta Mmarekani anaenda kuweka makazi ya kudumu China. Raia wengi wa Iran, Urusi, Uarabuni na Africa wanakimbilia Marekani na Ulaya.
 
Mfano rahisi ni hapo Libya tu.

Ajaribu kuwauliza walibya kwamba tangu utawala wa Gaddafi umeangushwa na wao kuletewa hiyo demokrasia Kuna mabadiliko gani ya maana waliyonayo mpaka sasa
Mabadiliko yapo, ile ni VERY NEGATIVE KWAO..!!
Umeme ulikuwa bure, sasa ipoje?
Matibabu ilikuwa bure, je sasa?!!
Elimu ilikuwa bure, saa hii je?
etc

DEMOKRASIA NI ADUI WA MAENDELEO...!!!
 
Mfano rahisi ni hapo Libya tu.

Ajaribu kuwauliza walibya kwamba tangu utawala wa Gaddafi umeangushwa na wao kuletewa hiyo demokrasia Kuna mabadiliko gani ya maana waliyonayo mpaka sasa
Libya ni mfano wa matokeo ya Udikteta na sio demokrasia, udikteta wa Gaddafi ndio uliosababisha vurugu zote za Libya na taifa kusambaratika. Libya haijawahi kuwa na demokrasia.
 
Back
Top Bottom