Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Sawa
 
Mkuu, nataka kuzamia China nipe mbinu.
Nenda Guangzhou kachukue mzigo wa kuja kuuza.

Nb: Sio rahisi kuzamia China tena kwa raia wa kiafrika ambao ambao hamna nchi iliyopakana na China kidogo wakorea huwa wanazamia japo nao wakinaswa wanarudishwa kwao.
 
Asante kwa kuweka marekebisho, kwa hiyo tunakubaliana kwamba hiyo demokrasia haiwezi kuwa main driving factor ya maendeleo tukitumia hii hii ya reference ya China?

Na pia kama Xi Hana maajabu ni nini kilimfanya mpaka wabunge wa chini karibu wote 2000 wakampigia kura ya ndio siku walivyokuwa wanaondo ukomo wa muhura na kumtaka awe raisi wa kudumu? Kwanini jambo kama Hilo wasingelifanya kwa mtu Kam Dieng Xioaping ambaye ndio anaaminika alikuwa genius kuliko hata watangulizi wake na alirekebisha makosa mengi yalioachwa na Mao na kisha kuja na mipango yake ambayo ndio imeifanya China kuwa hivi tunavyoiona leo?
 
Deng Xiaoping namfahamu japo bila hata Deng kuna watu wengi tu China wangeboresha mawazo ya Mao na kuleta mabadiliko.

Bila foundation ya Mao naye Deng asingeweza kufanikiwa katika mambo mengi sana.
 
Wachina wengi wanakimbilia kuishi na kuwa wakazi Marekani lakini ni nadra kukuta Mmarekani anaenda kuweka makazi ya kudumu China. Raia wengi wa Iran, Urusi, Uarabuni na Africa wanakimbilia Marekani na Ulaya.
Hii peke yake haitoshi kuwa sababu kwamba eti demokrasia ni Bora kuliko mifumo mingine ya kiutawala.

Hata Mimi ninaweza nikakwambia raia wa Qatar wanaishi maisha matamu sana kuliko wamarekani na hawajui hata hiyo demokrasia inafananaje.
 
GLF ilileta majanga China ni moja ya historia mbaya ya chama cha kikomunisti huwa hawapendi kuizungumzia sana
 
 
Upingwaji ulikuwepo hawa wakina Deng walikuwa na faction yao ilikuwa labelled capitalist roaders walishughulikiwa haswa
 
Nenda Guangzhou kachukue mzigo wa kuja kuuza.

Nb: Sio rahisi kuzamia China tena kwa raia wa kiafrika ambao ambao hamna nchi iliyopakana na China kidogo wakorea huwa wanazamia japo nao wakinaswa wanarudishwa kwao.

Sitaki kufanya uchuuzi. Kila mtu anachukua mizigo China kuja kuuza TZ in an already saturated market kwa watu wenye vipato finyu. GSM hadi mtu wa kawaida wote wanauza nguo toka China kweli! Me nataka nizamie huko niishi zangu freely kama mtu akizamia nchi za Magharibi bongo nirudi kuzikwa tu.
 
China wana age limit na term limit kwenye positions mbalimbali suala kubadilishana madaraka wanalo.

Xi Jinping sio raisi wa kudumu walichofanya ni kuondoa term limits jambo la kawaida mataifa mengi wanafanya.
 
Deng Xiaoping hakuwa na nafasi yoyote kubwa ila alikuwa na nguvu ambayo Xi hana na sina hakika kama atakuwa nayo maana Deng hakuwa katibu wa chama cha kikomunisti wala Rais wa China
 
Upingwaji ulikuwepo hawa wakina Deng walikuwa na faction yao ilikuwa labelled capitalist roaders walishughulikiwa haswa
Kwa jinsi GLF ilivyoleta athari wapingaji hawakukosekana, lakini je walikuwa na impact yenye uzito kiasi gani? maana Mao haku retreat hata pale alipoona mamilioni kwa malioni ya watu wakipoteza maisha sababu ya njaa na kukosa makazi.....
 
Deng Xiaoping hakuwa na nafasi yoyote kubwa ila alikuwa na nguvu ambayo Xi hana na sina hakika kama atakuwa nayo maana Deng hakuwa katibu wa chama cha kikomunisti wala Rais wa China
Kwa mtindo wao wa uongozi wa China nafasi aliyokuwa nayo Dieng Xioaping (Paramount leader) ni sawa na raisi tu, kwani baada ya kuondoka kwa Mao yeye ndio alikuwa mbeba maono.

Naona mnanchukulia poa sana Xi ila wachina wanajua ni kwanini wameona yeye ndio anawafaa kuwaongoza kwa maisha yake yote hasa kwenye hizi nyakati ngumu ambapo Kuna battle kubwa sana ya kiuchumi kati yao na Marekani
 
Udikteta ndio uliofanya Xi abadilishe katiba kwa kupata kura za wajumbe wote wa mkutano mkuu/congress(bunge). Mbunge katika bunge la Marekani anaweza kumtukana hata Biden na asifanywe chochote , Elon Musk anamtukana Biden na chama chake Marekani mara nyingi bila kufanywa chochote. Hakuna Mbunge anaweza kumpinga Xi China bila mkakati mpana na wa muda mrefu. Jack Ma aliyekuwa bilionea namba 1 China alijaribu kukosoa kwa mbali tu CCP wakomunisti wakamchukua wakamficha kwa muda aliporudi akawa anaimba Xi anaupiga mwingi na utajiri wake wakautikisa sasa hivi amepoa na kunywea kabisa.

Deng Xioaping hakubadilisha kwa sababu hakutaka na wakati huo kulikuwa na watu watata sana katika siasa za China kuliko walivyo leo hii. Hata Deng kuyapata madaraka ya China na kuwa mtawala kamili ilikuwa mtiti sio wa kitoto na palichimbika haswa ndani ya chama cha CCP hadi kuwazidi wengine.
 
Hakujawahi kuwa na battle kubwa ya uchumi kati ya China na Marekani kama ilivyokuwa enzi za Cultural Revolution na Cold war.
 
Kwa jinsi GLF ilivyoleta athari wapingaji hawakukosekana, lakini je walikuwa na impact yenye uzito kiasi gani? maana Mao haku retreat hata pale alipoona mamilioni kwa malioni ya watu wakipoteza maisha sababu ya njaa na kukosa makazi.....
Impacts ilikuwepo Deng alipewa jukumu la kufanya policy reforms baada ya GLF kuleta madhara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…