Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Kwanini China nchi ya kidikteta ina maendeleo makubwa kuliko Kenya na Zambia?

Na ndivyo jinsi madikteta wenye akili wanavyofanya hata kama ni walafi, basi wanawakumbuka na wanyonge... Familia ya Gaddafi enzi za uhai wake walikula sana Bata, watoto walijichotea sana mihela lakini pia baba yao w
aliboresha maisha ya wanainchi wa Libya.

Sasa viongozi wa CCM wanashindwa nini kufanya hivyo?

Kwa rasilimali zilizopo hapa nchini viongozi wa serikali ya CCM Wana uwezo wa kukwapua mabilioni ya pesa kadri watakavyo, wakati huo pia wanaboresha maisha ya Kila mtanzania kiasi Cha watanzania hao kutowaabugudhi kabisa watawala hao wa CCM.... Ila wanachofanya ni kufisadi mchinkwa sana huku wakizidi kuongeza ugumu wa maisha kwa watanzania, sababu ni nini hasa? Ni kukosa maarifa ya kiongozi au??
Lakini pia maisha bora ya Libya chini ya Qadaffi yalitiwa chumvi sana.

Tulisikia 'Libia ukioa unalipiwa mahari na unapewa nyumba''.

Niliongea na mtu aliekuwa anaishi Libya anasema sio kweli.

Ni kweli Gadafi alijitahidi, lakini sifa nyingi zilikuwa propaganda za uwongo, kama ilivyo kwa Paulo Kagame.
 
Libya ni mfano wa matokeo ya Udikteta na sio demokrasia, udikteta wa Gaddafi ndio uliosababisha vurugu zote za Libya na taifa kusambaratika. Libya haijawahi kuwa na demokrasia.
Baada ya Gaddafi kuondolewa hawakuchagua viongozi kidemokrasia???

Na kwanini wameshindwa kurejea kwenye Hali ya utulivu na kujenga uchumi imara kuliko kipindi Cha Gaddafi maana Sasa hivi wako huru Zaid?
 
OK OK OK kwa hiyo Kenya na Zambia zinaokoteza tu matapeli
Siyo system ya utawala peke yake inayoleta maendeleo, commitments, fulfilling obligations and responsibilities inapaswa kuanzia kwenye grassroots. Asilimia kubwa ya raia wakiwa na ile drive ya kusukuma maendeleo kila mmoja katika eneo lake slowly but surely nchi lazima inyanyuke kiuchumi.
Waafrika ni wachache mno wenye nia ya dhati na kuiishi nia hiyo kwa vitendo ya kuhakikisha nchi zao zinakua kiuchumi na akili pia tukibali tukatae hatuko sawa na wenzetu, kama kungekuwa hakujawahi kutokea muingiliano kati yetu na watu kutoka mabara mengine then all of a sudden ndiyo wangeibuka karne hii naamini jamii nyingi zingekuwa bado zinaishi maporini bila mavazi. Hata haya tunayajidili pasina kujuana kwa sababu ya akili za watu kutoka nje ya Afrika.
 
Wachina wengi wanakimbilia kuishi na kuwa wakazi Marekani lakini ni nadra kukuta Mmarekani anaenda kuweka makazi ya kudumu China. Raia wengi wa Iran, Urusi, Uarabuni na Africa wanakimbilia Marekani na Ulaya.
Hiyo hoja ya watu kukimbilia kwenye mataifa ya Magharibi huwa ni moja wapo ya hoja za kipumbavu na sijui ni kwann huwa mnaiendekeza.
Yaani utadhani nchi za Magharibi tu ndo zina wahamiaji tu hapa duniani.

Suala la mtu kutoka nchi moja kwenda nyingine mara nyingi huwa nitafuta furusa hasa za kiuchumi kwani wachina wako Marekani na Ulaya tu? Wachina siwametapakaa mpaka ndani ya nchi yetu?

Mbona Ufilipino na India ni mataifa yanayo jiita ni ya kidemokirasia lakini mamilioni ya raia wake wamejazana mashariki ya kati ambapo mataifa yote yanaongozwa kidkiteta?
 
Libya ni mfano wa matokeo ya Udikteta na sio demokrasia, udikteta wa Gaddafi ndio uliosababisha vurugu zote za Libya na taifa kusambaratika. Libya haijawahi kuwa na demokrasia.
Kama tumekubaliana ya kuwa democracy pekee haiwezi kukuletea maendeleo, basi kila nchi iwe huru kuchagua ni mfumo gani utakao faa kuliongoza taifa lao la msingi huo mfumo uwawezeshe raia wa nchi husika kuishi maisha mazuri.
 
Lakini pia maisha bora ya Libya chini ya Qadaffi yalitiwa chumvi sana.

Tulisikia 'Libia ukioa unalipiwa mahari na unapewa nyumba''.

Niliongea na mtu aliekuwa anaishi Libya anasema sio kweli.

Ni kweli Gadafi alijitahidi, lakini sifa nyingi zilikuwa propaganda za uwongo, kama ilivyo kwa Paulo Kagame.
Unalosema ni kweli, yapo mambo mengine ambayo hayakuwepo ila watu waliongeza chumvi... Lakini yapo mengi sana ambayo ni ya kweli kama vile wanainchi wa Libya kutokulipa bills za umeme na maji, elimu Bure kwa ngazi zote, matibabu Bure na endapo kama Kuna ulazima wa kwenda kutibiwa nje basi serikali ndio iligharamia na wanainchi kupewa nyumba za kuishi hasa wale waliokuwa hawana uwezo.... Haya yote yalifanyika japo ni katika substandard.

Kwanza kitendo tu Cha Gaddafi kuendesha nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo Libya bila kutegemea msaada wa aina yoyote ni jambo la kishujaa sana na anastahili maua yake maana viongozi wengi wa kiafrika wameshindwa.
 
Umesah

umesahau pointi moja muhimu sana. Uchumi wa Afrika unasimamiwa na mabepari. Nchi ikienda speed kimaendeleo, itapigwa tukio ili kuipunguza kasi.

Hii ndiyo sababu kubwa ya umaskini wa nchi zetu.
Cheap excuse, hakuna nchi ya Afrika iliyopigwa tukio eti kwa sababu uchumi wake unakua kwa kasi.
 
Watu wengi hawaelewei hili, wanafikiria udikteta wa watawala wa nchi zenye mafuta uarabuni ndio umezisaidia sana hizo nchi.
Kinachozibeba familia za Kifalme uarabuni ni kwamba pesa wanazopata za mafuta na gesi ni nyingi sana kiasi kwamba wanajichotea za kwao kuwafanya mabilionea na bado zinabaki nyingi tu za kufanya maendeleo kwa raia.
Vipi kuhusu Nigeria na Angola zote si zina mafuta kama waarabu?
 
Demokrasia haileti maendeleo..
Nchi za kiarabu wana demokrasia? Lakini angalia walipo... Qatar unaionaje?
Demokrasia ni neno pana. Wengi wanahusisha demokrasia na uchaguzi au vyama vingi jambo ambalo ni kosa. Na pia: demokrasia bila uwajibikaji ni bure. Unakuwa na demokrasia ya corruption utegemee maendeleo?
 
Mabadiliko yapo, ile ni VERY NEGATIVE KWAO..!!
Umeme ulikuwa bure, sasa ipoje?
Matibabu ilikuwa bure, je sasa?!!
Elimu ilikuwa bure, saa hii je?
etc

DEMOKRASIA NI ADUI WA MAENDELEA...!!!
Demokrasia pekee ilete maendeleo? Au udiktekta pekee ulilete maendeleo? Maendeleo yanaletwa na uwajibikaji.
 
Kama tumekubaliana ya kuwa democracy pekee haiwezi kukuletea maendeleo, basi kila nchi iwe huru kuchagua ni mfumo gani utakao faa kuliongoza taifa lao la msingi huo mfumo uwawezeshe raia wa nchi husika kuishi maisha mazuri.
Sahihi kabisa... Kila mtu ajiongoze kwa mfumo ambao anaona una mfaa, maswala ya kupangiana pangiana Kila mtu afuate mfumo Fulani ndio udikteta wenyewe
 
Mbona gambia ina watu wachache kuliko Qtaar na bado ni masikini bora hata Tz ?
Na vipi Saudia yenye watu wengi mbona ni tajiri?
Mbona Gambia ni ndogo kama Qatar na iliongozwa na dikteta na hakuna maendeleo? Nimekwambia Afrika tunatakiwa kuishi kienyeji bila maserikali. Si udikteta, wala demokrasia, unaotufaa.
 
Baada ya Gaddafi kuondolewa hawakuchagua viongozi kidemokrasia???

Na kwanini wameshindwa kurejea kwenye Hali ya utulivu na kujenga uchumi imara kuliko kipindi Cha Gaddafi maana Sasa hivi wako huru Zaid?
Hawakuchagua viongozi, wamekuwa wanapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe. Dikteta Gaddafi aliacha ombwe kubwa la uongozi nyuma yake lililojazwa na warlords wengi.
 
Back
Top Bottom