Na ndivyo jinsi madikteta wenye akili wanavyofanya hata kama ni walafi, basi wanawakumbuka na wanyonge... Familia ya Gaddafi enzi za uhai wake walikula sana Bata, watoto walijichotea sana mihela lakini pia baba yao w
aliboresha maisha ya wanainchi wa Libya.
Sasa viongozi wa CCM wanashindwa nini kufanya hivyo?
Kwa rasilimali zilizopo hapa nchini viongozi wa serikali ya CCM Wana uwezo wa kukwapua mabilioni ya pesa kadri watakavyo, wakati huo pia wanaboresha maisha ya Kila mtanzania kiasi Cha watanzania hao kutowaabugudhi kabisa watawala hao wa CCM.... Ila wanachofanya ni kufisadi mchinkwa sana huku wakizidi kuongeza ugumu wa maisha kwa watanzania, sababu ni nini hasa? Ni kukosa maarifa ya kiongozi au??