La hasha tofali za kuchoma sio za kimasikini ,ni uelewa mdogo tu wa wabongo.Kibongo bongo inaonekana ni cheap kutumia hizo tofali ,lakini kiukweli hawafuati utalaamu sahihi wa kujenga hizo tofali na ndio maana majengo yanayojengwa na wabongo kwa kutumia bricks hayawezi kudumu kulinganisha na majengo ya bricks ya wazungu.
Mbongo anajenga bricks kama anavyojenga blocks wakati kikawaida bricks ni nyembamba kuliko blocks.Kitalaamu ukuta wa bricks unatakiwa uwe na line mbili ya bricks au bricks zijengwe kwenye mfumo wa header bond yaani ubavuni wa ukuta uwe unaona kichwa cha tofali na sio ubavu wa tofali.