Kwanini Dar es Salaam magari binafsi aina ya Landcruiser V8 yako mengi sana?

Kwanini Dar es Salaam magari binafsi aina ya Landcruiser V8 yako mengi sana?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Sijajua watu wanafukua wapi hela, Kila siku huku Dar Nakutana Na land cruiser v8 zenye condition nzuri tena Gari binafsi zenye Plate number D, najiuliza na hii mishahara midogo ya taasisi za kibongo ya laki 8 kwa mwezi, watu wanawezaje miliki Na ku-maintain gari ya Tshs million 80 - million 200 plus?

Anaenunua Toyota v8 kwenye account atakua na Tsh ngapi? Ina maana hapa bongo Watu wengi kiasi ni matajiri?
 
Mkuu kama nchi tupo watu mill 60 unadhani hizo viieite ulizoona hapo Dar zinafika hata 1mill?

Halafu zipo pia za mchongo refer kesi ya sabaya ile aliinunua kwa mwarabu 60mill mpaka ikaja kujulikanika kwamba jamaa alikuwa na houseboy shoga.
 
Kuna mzungu mmoja alikuja bongo field, alipofika akaanza kuzunguka mikoa mbali mbali na kujionea jinsi majumba na mahekalu yamejengwa hio haikua ajabu ila ajabu ni Kwamba kumbe hayo majumba na mahekalu ni ya watu binafsi na akaambiwa asilimia kubwa ya hizo nyumba Watu wanajenga Kwa Pesa zao, akashangaa Sana kumbe walivyokua wanaambiwa Afrika maskini akajua watu Bado wanaishi Kwenye huts house kumbe sivyo bwana

Sasa akauliza viongozi wetu kwanini huwa wanaenda kulia Lia misaada kule na wanapewa na maajabu wanakuja kuitumbua Kwa Raha zao huku?

Akajibiwa nature ya mwafrika ni omba omba!
 
Sijajua watu wanafukua wapi hela, Kila cku huku dar Nakutana Na land cruiser v8 zenye condition nzuri tena Gari binafsi zenye Plate number d, najiuliza na hii mishahara midogo ya taasisi za kibongo ya laki 8 kwa mwezi, watu wanawezaje miliki Na ku-maintain gari ya Tshs million 80 - million 200 plus?

Anaenunua Toyota v8 kwenye account atakua na tsh ngapi? Ina maana hapa bongo Watu wengi kiasi ni matajiri?
Watu wanakodisha bunduki wanapata pesa
 
Kuna mzungu mmoja alikuja bongo field ,alipofika akaanza kuzunguka mikoa mbali mbali na kujionea jinsi majumba na mahekalu yamejengwa hio haikua ajabu ila ajabu ni Kwamba kumbe hayo majumba na mahekalu ni ya watu binafsi na akaambiwa asilimia kubwa ya hizo nyumba Watu wanajenga Kwa Pesa zao,akashangaa Sana kumbe walivyokua wanaambiwa Afrika maskini akajua watu Bado wanaishi Kwenye huts house kumbe sivyo bwana,
Sasa akauliza viongozi wetu kwanini hua wanaenda kulia Lia misaada kule na wanapewa na maajabu wanakuja kuitumbua Kwa Raha zao huku?
Akajibiwa nature ya mwafrika ni omba omba!

Hii Story nilisikia mara ya kwanza 2008 nadhani ilikuwa comment ndani ya Bongocelebrity.
 
Mkuu, baada ya miaka 5 na mimi ntavuta huyu mnyama ndio roho yangu itulie,
20211128_224941.jpg
 
Kilimo
Madini
Uvuvi
Nishati
Usafirishaji
N.k






Ila kubwa kuliko yote NI madini na ufisadi(michongo)
True Siri ya utajiri ipo kwenye madini pesa za chap na uhakika zipo ardhini kwenye madini. Ukiyajua kuchimba milioni 300, 500 ni sawa na buku. Huyu jamaa ashangai vijana tena wadogo wanaingiza basi 6 kwa mpigo.
Utajiri upo kwenye madini.
 
Nchi ya 10 kwa utajiri unakuaje masikini, KILA sehemu ni mali tele zimejaa hadi watu vijijini wanajenga juu ya madini.
 
Back
Top Bottom