Bwana Bima
JF-Expert Member
- Jul 29, 2014
- 429
- 929
Fanyeni utafiti wa kutosha. Jiulize why alipoulizwa kuhusu dhambi ya uasherati yetu hakukazia hizo amri kumu badala yake akatoa kanuni kwamba mtu anayemtazama mwanamke na kumtaman amezini moyon mwake? Alipoulizwa ili umpendeze Mungu why hakuanza kuorodhesha hizo amri ba masheria badala yake akataja jambo moja tu yani upendo kwa Mungu na Jirani?Kaangalie amri kumi za Mungu zilizokwenge Biblia, kisha utakapoona Sabato basi ujue ndio hiyohiyo hakuna amri nyingine ya Sabato zaidi ya Ile iliyoandikwa kwenye amri kumi.
Kutimiza Torati hata wewe ukiifuata unatimiza, unafuata, unaifanya kama ilivyoagiza. Hiyo ndio maana yake.
Kumpendeza Mungu ni kufuata amri na sheria zake na sio vinginevyo. Yesu alichosema ni kuhusu upendo lakini kisheria na Torati upendo unatafsirika katika sheria. Za Mungu.
Sabato ni moja ya amri za Mungu ambazo haya huyo Yesu mnayemfuata aliifuata Kwa adabu na heshima Kwa sababu Mungu aliagiza iwe hivyo.
Yesu aliposema hayo kwa kunukuu torati alitaja amri ya msingi kabisa kwa wakristo bila kujali mahali alipo duniani. Mfano kama unampenda Mungu huwez kuzini au kama unampenda jirani(neno pana) huwezi kumsemea uwongo.
Nakuelewesha tena ukianza kuzifuatilia hizo amri kumi bado kulikua na vijiamri vidogo vidogo vingi vinaingia hapo kutia ndani hata vijiamri vya sabato. Ndomana nilimuuliza mwenzako mbona mnangangania sabato ya siku tu na si zingine? Kwa msingi huo unaposema yesu alikuja kutimiza kwa majibu yake ni kama yesu alikuja kuziboresha. Yan hizo amri na sheria zilikua msingi tu na zenye kasoro nyingi. Yesu akaja kuweka kila kitu sawa.
Ndio sababu kila siku unaambiwa moyo wa mtu wa upendo ndio jambo ambalo Mungu anataka na sio masheria ya waisrael ambayo walipewa ili wasijichanganye na mataifa ya kipagani kwa wakati huo.
Sasa tuulizane nyie wasabato ni waisraeli? Mbona kila kitu kilichowahusu hamkifuati mnatenga vingine? Waisraeli walikua na lengo pa kuikumbuka sabato na maandiko yanafunua kwamba ni ili kukumbuka mateso na jinsi Mungu alivyowaokoa wakiwa misri, je nyie mnaifuata sabato kwa lengo gani? mnaifuata sabato ya siku ya Mungu kupumzika au sabato ya siku ya kawaida?