Kwanini dhehebu la SDA huwa wanalishambiulia zaidi Kanisa Katoliki na siyo madhehebu mengine?

Allah haabudiwi kwa siku maalum anaabudiwa siku zote mara 5 kwa siku kwahiyo taarifa yako si ya kweli hawana uwezo huo
 
Hata ukiwauliza wenyewe hawana jibu
wanapandikizana sumu tu kwenye makambi yao. na hii imekuwa hivi vizazi na vizazi.

halafu mkatoliki kwa dharau wala hana habari na wasabato, ndio kwanza anaendelea na mambo yake.

sometime nawaona wasabato ni sawa na bondia anayetumia nguvu nyingi kurusha ngumi hewani, maana hazina madhara.
 

Siku ya kwanza ni jumamosi sio jumapili. Mosi ni moja na pili ni mbili then jumatatu. Kimsingi siku ya saba ni ijumaa.
 
Katoriki
 
kitali 👇🏾
Ahahhaa, mkuu issue ya Allah kwamba siyo Mungu huko sipo nadhani hizi ni lugha tu, although unaweza nisaidia kwa kiarabu mwenyezi Mungu anaitwaje kwa kiarabu?.
Hata mimi sizungumzii hilo la Mungu bali nazungumzia kuibadili sabato toka Jumamosi hadi Jumapili. Wenzetu wa Allah wao ni Ijumaa hivyo hawahusiki kabisa na hilo la mabadiliko ya siku ya kuabudu.
 
Basi imempasa askofu..... "Imempasa" ni hiyali au lazima wewe mwalimu wako wa Kiswahili........
Hapo kwenye matowashi ni Mimi na wewe ndugu si lazima kuoa Ila kwa askofu imempasa yaani ni azima....

Usisahau Neno IMEMPASA inamaana sawa na lazima ama wajibu ambao lazima uufanye.
Lakini pia usisahau swala la wanawake kua na mamlaka.


Nikushauri Acha huko litetee Neno la Mungu
 
Katoliki ni kanisa la oya oya sana,fikiria muumini na mhudhuriaji mzuri wa kanisa lakini haijui BIBLIA hata kwa intro tu.Matokeo yake majibu juu ya YESU ni mtihani kwao na hapo ndipo mpinga KRISTO anapowadaka.KARISMATIKI angalau wanafuatilia BIBLIA.
 
Katoliki ni kanisa la oya oya sana,fikiria muumini na mhudhuriaji mzuri wa kanisa lakini haijui BIBLIA hata kwa intro tu.Matokeo yake majibu juu ya YESU ni mtihani kwao na hapo ndipo mpinga KRISTO anapowadaka.KARISMATIKI angalau wanafuatilia BIBLIA.
Na hata wao iweje ahubiri mwanamke wakati bible imepiga stop
 
Umekazania mimi na wewe even Askofu ni binadamu kama mimi na wewe
Je kati ya wewe na askofu nani anatakiwa awe mkamilifu sana mbele ya watu ?
Ok nakuongezea tena mstari katika biblia na zipo nyingi sana sio kama wewe umebase na hicho imempasa
kuelewa Biblia sio rahisi ngoja nikueleweshe mdogo mdogo utaelewa
Soma 1 wakorintho 7:32-35 ambayo inasema kwamba;

Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.

Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.

Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
 
Unazunguka Lakini unaludi palepale ya kwamba askofu imempasa, ukipata mstari wowote ule ambao askofu sio lazima kuoa nitaandika Bango linalosema MIMI NI MPINGA KRISTO. Usisahau askofu imempasa kuoa huo ni wajibu sio hiyari kinyume cha hapo Hana sifa ya kuongoza kondoo wa Yesu Kristo huyo ana sifa ya kuongoza, kundi la Wana wa upotevu.

Usisahau pia haya.
Mwanamke kua na mamlaka kanisani ni kinyume na maandiko, kubatiza kwa kunyunyizia ni kinyume na maandiko.

Ndugu yangu sio kwamba nakuvuta uje ninaposali hapana, Mimi Ninachotimiza ni kimoja tu kukushuhudia Neno la Kristo tu ni hivyo tu. Biblia haiwezi hapa ikasema askofu aoe na sehemu nyingine ikasema tofauti, ama pale isimluhusu mwanamke kua na mamlaka kanisani halafu pale ikasema vile. Kamwe haiwezi kua hivyo.

wewe Amini kwamba biblia imesema imempasa askofu aoe na hakuna sehemu Inayopinga Jambo hilo, Amini hivyo hilo ni kweli Amini Tu ndugu yangu. Yesu aliwaambia msipoamini mtakufa katika dhambi yenu. Hakuna hata sehemu moja aliposema MSIPOELEWA no ni kuamini Tu Amini Tu ndugu.


natamani kuongea na wewe kwa simu ndugu. Ubarikiwe
 
wengi wanachanganyikiwa kuhusu hilo, wakidhani kuwa mtu yeyote anayeitwa askofu ni lazima aoe…lakini unapaswa uelewe kuwa hapo Mtume Paulo alisema hivyo kwa mantiki ipi?, hakuwalenga wale ambao hawajaoa bado hapana, bali aliwalenga wale ambao wanao wake zaidi ya mmoja..kwamba hao ndio hawapaswi kuwa maaskofu, kwasababu ni lazima waonyeshe kielelezo kwanza wao wenyewe katika nyumba zao na ndio waje kuchunga wa nje, sasa kama mtu alikuwa na wake 6 kabla hajaamini na akaingia kwenye ukristo na ukristo unasema mtu anapaswa awe na mke mmoja, sasa unadhani wale atakaowachunga yeye kama askofu atakuwa anacho kielelezo gani?

Na ndio maana haipaswi mtu yeyote anayeitwa askofu au mchungaji awe na mke zaidi ya mmoja…Lakini haikumaanisha pale kwamba ni lazima kila anayetaka kuwa askofu awe na mke, huo ni uelewa hafifu wa maandiko. Kumbuka mtume Paulo naye hakuwa na mke, lakini alikuwa mwangalizi wa makanisa yote, Kristo naye hakuwa na mke lakini yeye ndiye Askofu wa maaskofu. Hivyo hapo maneno hayo yaliwalenga wale ambao tayari wanao mke zaidi ya mmoja.

1Wakoritho 7:32 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;

33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.

34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe

Ubarikiwe.
 
Sisi tunasoma pia na Agano jipya..kwanini hao wasabato hawalitaki agano jipya?.ikiwa hilo agano la kale lilikua sheria nyingi zilikua za Mussa..ambazo Yesu alipokuja aliziboresha..
Hao SDA wanasoma Agano la Kale na Agano jipya.
 
Sisi tunasoma pia na Agano jipya..kwanini hao wasabato hawalitaki agano jipya?.ikiwa hilo agano la kale lilikua sheria nyingi zilikua za Mussa..ambazo Yesu alipokuja aliziboresha..
Wasabato hawana agano lolote, wao wana biblia kwa ujumla wake

Hudhuria ibada yao utajionea, kuna sheria zilitolewa na Mussa na zikaondolewa na Yesu kama kulipiza ubaya kwa ubaya etc na kutakiwa kusamehe 7 mara 70, lakini kuna vitu havikubadilika na havitokuja kubadilika kamwe

Ikiwemo Amri 10 za Mungu na hapo ndipo tofauti inapoanzia baina ya Wasabato na madhehebu mengine ikiwemo ya kipentekosti, wakatoliki na kadhalika


Ukiona tu kanisa lako au imani yako katika mafundisho yake imeiacha hata amri moja kati ya zile 10, toka huko haraka sana bila kugeuka nyuma. . .
 
Catechism ni guideline tu. Na kanisa lilikuwepo kabla ya bibilia, Bibilia pia ni mapokeo ya kanisa walicompile vitabu jo, kasome tena.
Na ibada ya masanamu ilikuwepo kabla ya kanisa na mnaitekeleza mpaka leo, hivi inakuaje mtu na akili zako timamu unasujudu mbele ya sanamu la mwanamke halagu mnamwita mama wa masihi?, Unajifanyiaje sanamu la kuchonga na unaamini lina baraka wakati limetengenezwa na fundi mwenye mikono kama wewe?
 
Ndugu wakolinto wa Kwanza Sura ya 7:32-34 hapo hakuna askofu na usipalazimishe pawe. Maana maelezo yako unalazimisha, Neno linasema askofu imempasa awe na mke mmoja Tu. Hilo ndivyo ilivyo si vinginevyo hakuna nyongeza ya hiyo. Askofu ni wajibu kuoa. Unapokuja kwa Paulo usifosi iwe kwake kwa maana yeye alikua na huduma nzito mno ya kupeleka ujumbe kwa wamataifa Paulo yeye ana huduma ya tofauti na amepata hiyo neema, ni sawasawa na Musa Mungu anawaambia waislael kwamba msijitengenezee vinyago Lakini anaambiwa Musa tengeneza nyoka Wa Shaba, hivyo neema hiyo, hiyo kwa Musa ndivyo ilivyo kwa Paulo .

Neno la Mungu linasema askofu imempasa awe na mke mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…