Kwanini dhehebu la SDA huwa wanalishambiulia zaidi Kanisa Katoliki na siyo madhehebu mengine?

Wasabato wanapinga mfumo wa upapa(papal system) hivyo VATICAN ni adui moja kwa moja , nimebahatika kukaa nao karibu, wanaamini katika kupumzika siku ya jumamosi (ya Saba) .

Note :wanawake wa kisabato wanaongoza kwa nywele natural [emoji16]
Ila Wana megwa ka kawa
 
Huwa Kuna SDA wameajiriwa RC wanahudhuria mpk ekaristi...unafiki Dunia hili hautaisha
 
Hii vita haijawahi kupata mshindi, kila mtu asali na kuamini anavyoona.
Sijawahi kuona mkatholiki akikashifu au kukosoa dini za wengine ila wengine ndio huwa wanakashifu. Kwa misingi hii, hakuna vita hapa zaidi ya shambulio
 
Mungu mwenyewe analionya hilo Kanisa kwa ukengeufu wake tena kwa kuliita mama wa makahaba wasabato wasisingiziwe kwa lolote wao wanasema kile biblia isemacho tu
 
Wapi kwenye biblia umewahi kusikia imeagizwa

Tuombe kwa kupitia Mariam

Tuabudu siku ya kwanza ya juma

Kutubu kupitia mapadri

Tubatize kwa maji ya jagi na beseni

Tule meza ya Bwana mkate tu bila divai wala kutawadhana miguu

Tule najisi

Tubatize watoto

Wasabato wakisema hayo wakatoliki na nduguzo myafanyayo siyo sahihi wanakosea nini na huku Isaya anasema

ISA. :58:1
Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
 
Siku ya kwanza ya juma ni jumamosi ndugu. Mosi ni moja , pili ni mbili na tatu ni tatu so hao wasabato wenyewe nilitegemea wawe wanasali ijumaa kama wafuasi wa Mudi
 
Siku ya kwanza ya juma ni jumamosi ndugu. Mosi ni moja , pili ni mbili na tatu ni tatu so hao wasabato wenyewe nilitegemea wawe wanasali ijumaa kama wafuasi wa Mudi
Umetumia lugha ya kiswahili vipi ukitumia kingereza? Nenda sasa kamalize na kiarabu na kiebrania lugha za kale ndio utashangazwa. Saturday kingereza, Sabti kiarabu ni siku ya karne maelefu kabla ya kiswahili kuja na hizo mosi na pili
 
Wakatoliki kupitia Maaskofu wao ndiyo walioweka mpangilio wa Biblia nandiyo walikuwa watunzaji wa Biblia inayosomwa na haohao Wasabato!
Hujawahi ijua historia ya biblia wewe. Ilikuwa ikichomwa moto hio ipotee duniani, na hao wakatoriki, katoriki ya leo na ya awali na zama za kati wana historia complicated sana
 
Hujawahi ijua historia ya biblia wewe. Ilikuwa ikichomwa moto hio ipotee duniani, na hao wakatoriki, katoriki ya leo na ya awali na zama za kati wana historia complicated sana
Em njoo unywe kei vant achana na hao wasikusumbue kichwa
 
Siku ya kwanza ya juma ni jumamosi ndugu. Mosi ni moja , pili ni mbili na tatu ni tatu so hao wasabato wenyewe nilitegemea wawe wanasali ijumaa kama wafuasi wa Mudi
"Ijumaa" kuu ni siku aliyokufa yesu,,kwenye biblia kuna mtu alienda kuuomba mwili wa yesu siku hiyo ili sabato ikiingia isiukute mwili msalabani,siku ya tatu ya umauti wake, yaani siku ya kwanza ya juma (jumapili yesu akafufuka) hata pasaka ndo maana inakuwaga jpili. Soma biblia utajua vingi na utabreak Free kutoka kwenye cheni za wazungu na waarabu
 
Sisi tunasoma pia na Agano jipya..kwanini hao wasabato hawalitaki agano jipya?.ikiwa hilo agano la kale lilikua sheria nyingi zilikua za Mussa..ambazo Yesu alipokuja aliziboresha..
Sawa,kwenye agano jipya ni wapi nguruwe ameruhusiwa kuliwa?tupe andiko
 
Mpk hapa ubishi umeisha kumbe kuna dhehebu linaitwa katoriki...wakatoriki..
endeleeni kubishana..

KANISA MOJA TAKATIFU LA MITUME ndipo imani yangu ilipo...
Mtume gani alikuwa mkatoliki?tupe andiko ndugu,mtaje mmoja tu,usije tu ukasema mtume na nabii mwamposa
 
Soma Luke 8:26 je, wale Nguruwe waliokuwa wakichungwa hawakuwa mlimani hawakumilikiwa?
Kumbuka walikuwa Wakichungwa!
Harama inachungwa? Or inamilikiwa!?
 
Mtume gani alikuwa mkatoliki?tupe andiko ndugu,mtaje mmoja tu,usije tu ukasema mtume na nabii mwamposa
Hao kina mwamposya watume wa kisasa..
Sio walikua wakatoliki ila tumefuata nyao zao kuanzisha kanisa
Mfano...mtume Petro
Juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa...
 
BIBLIA KUHOJI, HIVYO WAKATOLIKI HUWA HIYO LIGI WANAIKIMBIA ,HAWAYATAKI MAANDIKO YA BIBLIA AMBAYO PIA MARA MOJAMOJA NA WAO BIBLIA WANAITUMIA..
Hata wewe ni Msabato. Hivi umewahi walau muda ukafuatilia ibada ya RC? Kila siku ina neno la Tafakari kutoka katika Biblia, hapa nasisitiza, kila siku ina neno lake la Tafakari na kila siku kuna Ibada, halafu anakuja mtu kusema eti Biblia haitumiwi RC. Nitajie siku yoyote mwaka huu nikupe neno la siku hiyo halafu uangalie linatoka nje au ndani ya Biblia.
Vitu vingine muwe mnauliza. Katekisimu ni kama syllabus ya mafundisho, mtoto wa Form One huwezi kumpa hesabu ya Integration, vivyo hivyo Katekisimu inaonyesha mtiririko wa mafundisho, lakini contents zote zinatoka kwenye Biblia, sasa hapo RC wapongezwe au walaumiwe? Maana RC wanaamini katika elimu, haiwezekani ukasoma Biblia kwa kukariri maandishi bila kuelewa mantiki ya andiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…