Watu watatoa kila aina ya sababu, kuanzia TRA, kodi za pango, uchumi mbaya, lakini mimi nadhani sababu kubwa ni attitude ya watanzania i.e. kuiga biashara kwa sababu tu umeona fulani anafanya bila kuchunguza au kuwa na ujuzi. Kwa mfano ofisi za serikali na mshirika ya umma, kuna wanafanyazi wakipiga fedha wanachojua ni kukimbilia kuanzisha biashara na kuweka wafanyakazi wa kuiendeleza. Hii imesababisha kuwe na biashara nyingi za kuiga, na ambazo utafiti wa kina kuhusu uendeshaji, faida na masoko haujafanyika.