DOKEZO Kwanini fremu Dodoma zinafungwa sana na biashara kufa kila uchwao?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Dom pagumu kwa baadhi ya biashara, kabla ya kufungua biashara unahitaji uumize akili haswa ujue ni biashara gani ukifanya itatoka vinginevyo ukikurupuka lazima ufunge.
Watu watatoa kila aina ya sababu, kuanzia TRA, kodi za pango, uchumi mbaya, lakini mimi nadhani sababu kubwa ni attitude ya watanzania i.e. kuiga biashara kwa sababu tu umeona fulani anafanya bila kuchunguza au kuwa na ujuzi. Kwa mfano ofisi za serikali na mshirika ya umma, kuna wanafanyazi wakipiga fedha wanachojua ni kukimbilia kuanzisha biashara na kuweka wafanyakazi wa kuiendeleza. Hii imesababisha kuwe na biashara nyingi za kuiga, na ambazo utafiti wa kina kuhusu uendeshaji, faida na masoko haujafanyika.
 
Wewe ajira za nioko ,unajua ni ajira ngapi zinazalishwa nchi hii ?
 
Kabisaa ,Kila mtu tigo pesaa , nilishawai fanya biashara ya kuuza na kusambaza gesi majumbani baada ya mwaka Kila mteja wg nae alikua muuzaji wa gesi nyumbani kwake , nikaachana na hio biashara
 
Rekebisha hilo neno la kwenye mabano ingawa ujumbe umeeleweka. It's supposed to be Varieties
 
Wengi walikimbilia Dodoma kwasababu ya ujio wa makao makuu ya ofisi na taasisi nyingi za kiserikali baada ya late Magufuli kuanza kuisimamia Dodoma kama mji mkuu wa nchi. Baadhi ya taasisi hizo zimerudisha miguu Dar kama sehemu yenye mizunguko mkubwa kibiashara na kifedha.
Poleni kwa wale ambao walikurupuka na sasa wanakuna vichwa kwa hasara kubwa wanazoingia sasa
 
Nitajie taasisi tano tu au wizara zilizoludi dar
 
Kwa sisi wenyeji tulishajua zsmani
Dodoma hapa wafanyabidhara wanadouble price sana vitu hence tunaagiza tu dar mfano TV maybe hisense inch 55 tu bei huku parefu tofauti na nikiagiza dar au kuifata mwenyewe .

Kingine mzunguko wa pesa ni wa msimu tu .

Halafu wafanyabishara wenyewe hawajiongezi .
Unakuta ma frame yamepangana yote ni maduka ya nguo..!

Kodi nazo ni kubwa kweli .
Biashara itatoka wapi hapo?
 
Hua unaagiza kwa bei gn nchi 55
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…