Kwanini gharama za kutuma pesa kutoka Akaunti ya benki kwenda mtandao ya simu ni kubwa sana?

Simbanking hasara sana kwa wateja wa banks, ila ni faida kubwa kwa mabenki. Serikali inatakiwa itoe masharti kwa gharama rasmi za fedha za Simbanking..!!

Banks nyingi zinawanyonya sana wateja wao kwa Simbanking, hasa CRDB, NMB… Ingetakiwa Simbanking gharama zake ziwe ndogo kuliko hata gharama za kwenda bank kutoa fedha au iwe sawa na gharama za ATM au chini..!!

Mimi nailaumu Serikali kwa hili, hasa wizara ya fedha, ingethibiti hili, gharama za Simbanking ni kubwa sana bila sbb yoyote
 
Huduma nilizoacha kutumia
1. Kutoa fedha zilizoko kwenye account ya bank kwa wakala
2. Kutumia apps mbali mbali za fedha kwenye simu
3. Kutuma ama kutoa fedha kwenye account ya bank kwa njia ya simu

Waweza ona imerahisha huduma bali ni garama sanaa
 
Una compare na nini? Kubwa zaidi ya nini ? Ngapi ulitaka iwe ndio uone fair ?
 
weka takwimu uzi unoge!
 
TAFUTENI FEDHA MAZEE na mtumie muda wenu vizuri kwenye mambo yenye tija na ya maana, hivi mmejaribu kutafakari kuhusu muda na usumbufu ulipo wakati unahangaika kukaa kwenye foleni kufanya miamala ukiwa benki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…