Habari zenu,
Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia:
"Ukisoma mwanzo unaambiwa Adam na Hawa walimzaa Kaini na Habili, baadaye Kaini alimuua nduguye Habili. Baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini (Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni). Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa Henoko."
Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
Soma Biblia Mwanzo 5:1 - 7
iki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
6 Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi.
7 Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake.
Ukisoma mstari wa 4 unaonyesha kuwa Adam na Hawa walizaa watoto waume kwa wake. Bila shaka kabisa walioana wao kwa wao ili kuendeleza uzao. Hakukuwa na katazo lolote linalozuia kaka na dada kuoana kwa wakati ule.