Kwanini hamtaki kujibu haya maswali kwenye Biblia?

Atakuwa alimaanisha mji alioishi na siyo ulimwengu kama tunaoufahamu leo. Na ukumbuke enzi zile vitabu viliandikwa kwenye ngozi au magamba ya miti. Leo hii kuna mamilioni ya vitabu na bado dunia ina nafasi ya kutosha
 
Rudi secondary usome biology
Mungu ni zaidi ya biologist, engineer, mkemia yoyote duniani

Nilipokuwa nasoma Biology jinsi tumeumbwa na mifumo ya kuendeleza uhai ya binadamu nikaamini kweli Mungu yupo

Mpaka leo bado wanadamu wanajifunza mwili wa binadamu na hawajamaliza

Niliposoma Geography kuhusu dunia na features zake, Physics na laws zake

Nikakubaliana na haya maneno ya Warumi 1:20

Warumi 1:20
Neno: Bibilia Takatifu


20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani uwezo wake wa milele na Uungu wake, umedhihirika wazi wazi kutokana na vitu alivyoviumba. Kwa hiyo watu hawana kisingizio.
 
Nani alikwambia aliingiza wanyama wote kwenye safina ilikuwa ni dume na jike tu kila aina ya wanyama, wadudu na ndege

Unafikiri kwa uwezo na nguvu za Mungu ambaye amekuumba wewe atashindwa kufanya miujiza kama hiyo?
Soma biology...😂uje na namba za species wote duniani...uje na vyakula vyao... temperature wanaotakiwa kuishi...space wanaotakiwa kukaa... afu ndo uniambie wameishije kwenye kiboti ambacho hata titanic ni kubwa.
😂😂😂Halafu kama alitaka kufanya miujiza kwa Nini ahangaike na wanyama si angefunga macho na kufungua watu waovu wote wafe au awafanye wasiwe waovu bac...
😂 Kingine hii story ni copy na paste ya epic of Gilgamesh epic of artrasis sijui genesis ya wahindi...etc... it's so old Hadi makabila ya Tanganyika yana story za wet n wild Kama hizi
😂😂Finally mbona Mungu wako kafeli coz baada ya kutuogelesha bado watu wabaya wapo...so point ilikuwa nini....
 
😂😂😂A Hindu can say the same akasema brahma ndo muumbaji
Same as Islam na Allah
Greek na Zeus
😂Hio invisible qualities are clearly seen ni verse ya kipuuzi Sana...
Bado hujajibu why Mungu wako hatuambii chochote kipya...anasema magonjwa ni mapepo na sio bacteria virus au protozoans ..au alikuwa hajui...he says nothing abt cells au ubongo unavyohusika na emotions ...haongelei chochote kuhusu fungi...😂😂😂yupo very limited in knowledge.
Wewe Kama unataka kuamini Mungu yupo it's okay...ila sio huyu wa mchongo wa kuweka wanyama wote duniani na watu wawili kwenye bustani...polar bear anaishije kwenye bustani...😂😂😂we mtu mzima ujue
 
😂😂😂😂Siwezi...coz dini haipo hivyo...dini ni kuteka akili tu .. unamwambia mtu kuwa yeye ni mgonjwa na anahitaji dawa haraka Sana na hii ndo dawa Kama hutaki utaugua milele...that's
Unaweza mwanangu hujui tu, kuna wadau wanakusubiria wewe tuwe na mwanzilishi wa dini muafrika ili tubalance au sio
 
😂😂😂Halafu kama alitaka kufanya miujiza kwa Nini ahangaike na wanyama si angefunga macho na kufungua watu waovu wote wafe au awafanye wasiwe waovu bac...
Mungu ametupa uhuru tuwe wema au tuwe waovu hataki kutuendesha kama maroboti. Anataka tumpende kutoka moyoni sio yeye atulazimishe

Yoshua 24:15 BHN

Kama hamtaki kumtumikia Mwenyezi-Mungu, basi chagueni leo hii ni nani mtakayemtumikia
 
😂😂Finally mbona Mungu wako kafeli coz baada ya kutuogelesha bado watu wabaya wapo...so point ilikuwa nini....
Wakati wa Mungu wa kuondoa watu wabaya mazima bado ulikuwa haujafika.

Baada ya Adamu na Hawa kumkosea Mungu, kwenye MWANZO 3:15 alitoa huu unabii
Mwanzo 3:15 BHN
Nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, kati ya uzawa wako na uzawa wake; yeye atakiponda kichwa chako, nawe utamwuma kisigino chake.”

Unabii huo utakapotimia ndio utakuwa wakati wake Mungu wa kuwaondoa watu wabaya wasiwepo kabisa
 
anasema magonjwa ni mapepo na sio bacteria virus au protozoans
Hakuna mahali Biblia inasema magonjwa ni mapepo. Mapepo na magonjwa ni vitu viwili tofauti

Nyakati za Biblia watu waliumwa magonjwa kama yetu na hayakuwa mapepo mafano Timothy alikuwa na ugonjwa wa tumbo

1 Timotheo 5:23
Neno: Bibilia Takatifu

23 Usiendelee kunywa maji tu bali tumia divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako na maumivu yako ya mara kwa mara.

Haijasemwa Timothy alikuwa na mapepo


Hata madaktari wanaotibu magonjwa kama madaktari wa siku hizi walikuwepo kutibu magonjwa kama tunayoumwa leo mfano Luka alikuwa daktari kabla hajawa mtume wa Yesu

Wakolosai 4:14

Luka, yule daktari mpendwa

 
Biblia ni hadithi za kutungwa sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za kusisimua za joka la Mdimu.

Bible is a Fairytale, Mythology, Fictional book.
Hata wewe ni wa kutungwa vilevile.
 
apo chacha! wanatheologist Wana majibu ya maana wamefundishwa huko chuoni
 
Thibitisha kauli yako kwa hoja haii siyo kuacha hoja hewani . Uumbaji uliendelea ? Wewe umejuaje ulikuwepo???....
 
Sasa mtU aliyewaymba hao viumbe atashindwaje kuviongoza ili viadapt hali iliyokuwa kwenye safina?
😂😂😂Wangesema...ishu ni kwamba walikuwa hawajui waliotunga hizi story....okay achana na Hilo...maji yalijaa urefu wa milima mirefu duniani. Tuassume wapo usawa wa everest...Hilo baridi hao ng'ombe si watakufa...hiyo pressure iliyopo hapo je.. that's geography. Ehe baada ya kuachiwa walizalianaje coz genetically species pair haziwezi propagate kiufanisi...😂in short ili hii story ifanye kazi u have to put miracles kila sekunde asa why mess with the flood na uuwe wanyama wasio na hatia wakati angeweza tu kimiujiza kuua watu wabaya...plus baada ya hapo watu wabaya waliendelea kuwepo immediately after the flood...😂story ya kitoto sana hii
 
Mke wa kwanza wa Adam ni Lilith na siyo Eva/Hawa. Walipokorofishana na Lilith kuondoka ndipo akaja Eva
Where's ur biblical evidence? 😂Nimesema Lilith ni excuse kwa sababu ya contradictions kibao kwenye bible. Pale mwanzo Mungu kaumba male n female...baadae Mara Adam yupo mwenyewe so they had to make up a story
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…