Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 19,484
- 38,416
Kaini na Abel walikuwa na dada zao. Tamaduni za watu wa Mashariki ya kati ziliwatukuza zaidi wanaume kuliko wanawake.Habari zenu,
Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia:
"Ukisoma mwanzo unaambiwa Adam na Hawa walimzaa Kaini na Habili, baadaye Kaini alimuua nduguye Habili. Baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini (Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni). Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa Henoko."
Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
Abel alioa mojawapo wa dada zake. Na adam alikuwa nao mabinti wengi tu.
Hata mfano Yakobo hakuwa na watoto 12 wanaume tu bali pia alikuwa na mabinti wengi na siyo Dina peke yake ambaye tunaona kisa chake baada ya majanga.
Hivyo hivyo Avram, Isaack n.k
Angalia pia Marko 6:44. Inasema Yesu alilisha watu elfu 5 wanaume. Huu ni utamaduni wa kuwatukuza wanaume. Haiwezekani ule mkutano walikuwepo wanaume elfu 5 na hakukuwa na wanawake au watoto. Lazima walikuwepo ila walioripotiwa ni wanaume tu