Kwanini hamtaki kujibu haya maswali kwenye Biblia?

Kuna mengi yalitokea lakini hayajulikani, kwa sababu Kuna baadhi ya vitabu vilipigwa marufuku kutumika kwa maslahi ya watu Fulani. Majibu ya swali hili yanapatikana katika kitabu Cha "MAISHA YA ADAM NA EVA" ambacho nacho kimeondolewa kwenye bibilia za sasa. Kabla ya Eva Adamu alikuwa na mke mwingine na wengi hawajui hili kwa kuwa kitabu hiki hakitumiki.
 
😂Watakuambia Mungu anaweza yote...
Kuna mmoja huyo anajibu lake eti biblia imekaa kimya wewe unahoji nini? Kukaa kimya ina maana kuna maswali magumu hayana majibu.
Bahati mbaya watu hunakili tu yaliomo mle na kujifanya wana upako wakati hawana uwezo wa kujibu maswali magumu.
Watu wengi wasiokuwa na ufaulu mzuri shuleni ndio hao hugeuka wahubiri wetu.
Huwezi ona mtu mwenye GPA ya 4+ anakuwa muhubiri bali wale waliopata ufaulu mdogo huko mashuleni.
Ina maana tunahubiriwa na watu wenye IQ nfogo.
 
😂Mi simo huku...😂wasijenipiga mawe na kunitishia gesi baada ya kufa
 
Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?

Hiyo ni lugha ya mafumbo. Ilitumiwa kwa makusudi kabisa. Adam ni mtu wa kwanza kuumbwa, si kimwili ila kiroho, kwa kupewa neno la Mungu ili alisambaze kwa wanyama (wajinga wasio na neno). Ni mtu wa kwanza kutoka mavumbini (kwa watu wasio na neno) kupokea neno kutoka kwa Mungu, na ndiyo uumbaji wenyewe wa kwanza.
 
😂😂😂Hili Chaka lenu la mafumbo si tulishakataa
 
Habari zenu,

Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia:

"Ukisoma mwanzo unaambiwa Adam na Hawa walimzaa Kaini na Habili, baadaye Kaini alimuua nduguye Habili. Baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini (Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni). Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa Henoko."

Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
Inawezekana akawa ni dada yake. Enzi hizo, walikuwa wakiwataja watoto wa kiume tu, au ikitokea Jambo la kutaja idadi ya watu, watasema wanaume kadhaa ilhali na wanawake/ watoto pia walikuwapo.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mungu anaishi!! Ila taarifa nyingi ndani ya biblia zimeondolewa.
 
Ukikua utajua kuwa kumbe Adam na Hawa ni majina wakilishi ya mtu mume na mtu mke, Kaini na Abel pia utakuta ni majina wakilishi ya uzao wa mwanadamu baada ya kutenda dhambi ya asili, utajua kuwa biblia sio kitabu cha historia au notebook ya Mwenyezi Mungu kwamba kila alichokifanya alikuwa anaandika, la khasa, biblia ni kitabu chenye "ujumbe" wa Mungu kwa wanadamu wa zama na enzi yote... kadiri ya askofu mkuu wa dsm, mhashamu Thadeus Ruwa'ichi, mjubilei wa miaka 25 ya uaskofu na professor wa maandiko matakatifu mwenye shahada ya juu ya udaktari wa metafizikia ya maandiko matakatifu.
 
Habari zenu,

Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia:

"Ukisoma mwanzo unaambiwa Adam na Hawa walimzaa Kaini na Habili, baadaye Kaini alimuua nduguye Habili. Baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini (Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni). Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa Henoko."

Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
Na wewe jibu swali je Allah ktk uumbaji wake kati ya Dunia na Mbingu alianza kuumba nini? Quran 2:29
 
Mbona hilo rahisi, alianza kuumba mbingu....
Kama ni msomaji wa Quran hilo sio swali
 
Unaposema kupitia babu na Bibi to endless una uhakika na ushahidi unao?
Au una force assumptions zako ziwe sahihi na fact 100%?

Hivi kama wewe mwenyewe hujijui umetokea wapi,...utaweza kujua alipotokea Mungu?

Nadhani ni rahisi zaidi kujijua wewe kwanza,...Kisha ndiyo uanze kuhoji Mungu katokea wapi.

Mfano unaweza kujiuliza:-
Question_Scientifically,between sperms and Human being which was the first to appear,?

Answer_Sperms are a part of human reproduction, so technically, human beings came first.

Sasa hapo unapaswa ujiulize kama scientifically Watu walianza kuwepo kabla ya reproduction,. then hao watu walitokea wapi while reproduction haikuwepo?

Unaweza ukajiuliza maswali kama hayo,..huenda moyo wako ukaelewa.
Kusema kweli binadamu, katokea wapi kila mtu, hajui wala mungu, yupo au hayupo, ni ubunifu wa kibinadamu tu, wa kufikilika, tupotupo yani "hatuelewi"?
 
Hakuna sehemu inasema alipotoka nje ya Edeni alikutana na watu

Mwanzo 3:23-24 BHN
23. Basi, Mwenyezi-Mungu akamfukuza Adamu nje ya bustani ya Edeni, ili akailime ardhi ambamo alitwaliwa.

24. Alimfukuza nje, na kuweka mlinzi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia iendayo kwenye mti wa uhai
.
Ushaidi aliyeshuhudia ni nani??
 
Idadai ya Waisrael wakati wanatoka utumwani Misri kwenda Nchi ya Kaanani, walikuwa watu laki 6, bila kuhesabu wanawake na watoto
Yesu aliwalisha kwa samaki mmoja na mikate mitano watu elfu tano, bila kujali wanawake na watoto
Sijui kama nitakuwa nimejibu swali lako
Sio kweli. Kama wanawake walikua hawatajwi, mbona Hawa alitajwa na tukajua ndio mke wa Adam.
 
Habari zenu,

Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia:

"Ukisoma mwanzo unaambiwa Adam na Hawa walimzaa Kaini na Habili, baadaye Kaini alimuua nduguye Habili. Baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini (Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni). Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa Henoko."

Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
Elewa biblia usikariri Adam kasimama badala ya binaadam wakiume na eva kama wakike haimaanishi aliumba watu wawili tu bali wake kwa waume
 
Nani alikwambia aliingiza wanyama wote kwenye safina ilikuwa ni dume na jike tu kila aina ya wanyama, wadudu na ndege

Unafikiri kwa uwezo na nguvu za Mungu ambaye amekuumba wewe atashindwa kufanya miujiza kama hiyo?
Mungu alikua na uwezo wa kusema tu kama muweza wa yote??
 
Ninachojua kutoka kwa mafundisho ya kiislam, Adam na hawa walikuwa wanazaa pacha mke na mme , ila kuoana ikabidi , wabadilishane pacha yaani kaini aoe pacha wa khabili , alikaidi akasema atamwoa pacha wake mwenyewe kwan alisema ni msuri sanaa ! Hivyo kwa swali lako majibu ni kwamba walikuwa wakizaa pacha wa rangi mbali mbali na dhumuni ni kutanbuana eg mweupe, mweusi nk!!
 
Habari zenu,

Naombeni majibu ya haya maswali kwenye maneno ya Biblia:

"Ukisoma mwanzo unaambiwa Adam na Hawa walimzaa Kaini na Habili, baadaye Kaini alimuua nduguye Habili. Baada ya hiyo hali Mungu akamfukuza Kaini (Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana akakaa katika nchi ya Nodi mbele ya Edeni). Kaini akamjua mkewe naye akapata mimba akamzaa Henoko."

Swali liko hapo; Huyo mke wa Kaini alitoka wapi wakati Mungu alikuwa ameumba watu wawili tu na walizaa watoto wawili na kati ya hao mmoja alikuwa amefariki? Huyo mke alitoka wapi, embu tupeni majibu?
NENDA KAMUULIZE.
 
Back
Top Bottom