Sababu za safari kuwa ndefu ni 2
1) Ni Mungu hakutaka wakutane na vita mapema kwa sababu bado ni taifa changa.
Kutoka 13:17
"Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri;"
2) Ni kwa sababu Mungu aliwaadhibu kwa kipindi cha miaka 40 mpaka kizazi kilichomkaidi yeye kipite ndo safari iendelee.
Hesabu 14:34
"Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu."