Kwanini Hayati Dkt Magufuli aliichukia sana Kaskazini lakini sasa Rais Samia anaipenda sana hii Kanda?

Mradi mkubwa wa maji hapa Arusha uliogharimu karibu bilioni 500, kusambazwa kwa umeme vijiji vya Arusha manyara mpaka kilindi Tanga kote huko ni umeme, Kufufuliwa kwa Bandari ya Tanga yote kafanya Magufuli lakini bado mtasema alikuwa anachukia kanda Yetu ACSEE binadamu sijui utamfanyia nini aridhike
 
Aliyekuambia duniani kuna uwiano ni nani? Unajua maana ya vidole kupishana urefu? Hatulingani. Hata nchi zilizoendekea yako majimbo ni tajiri kuliko mengine. Halafu Kilimanjaro utajiri wao ni wa kupambana. Utamlinganisha na Mndengereko? Hata hivyo pamoja na kuwa Yule Shetani anayeeoza ardhini alikandamiza Kilimanjaro ikiwemo hata Mtangulizi wake lakini bado Kilimanjaro iko vizuri. Walichofanya baada ya Hizo awamu mbili kuwabagua waliunda Umoja wa Maendeleo kila Eneo wakaanza kujichangisha wakajenga barabara zao au kuongezea nguvu TARURA ili waongeze kilometer za barabara. Sasa hawa watu wapambanaji unataka eti kuwaambia mambo ya uniformity. Chuki ya Magufuli kaskazini ilikuwa ya ajabu mno. Msoga aliichukia lakini kwa kiasi.

Huyu Mh. Rais Samia anajua umuhimu wa Kilimanjaro na Arusha ndiyo maana anazitendea haki.

Lile Jitu life mara Saba.
Magufuri aliwafufulia reli ambayo ilikuwa imekufa kwa miaka 28 sasahivi wachaga wanasafirisha biashara zao kwa kuchagua,watumie reli au magari,Samia kaisha fanya kipi kipya hapo?
 
Utawala wa hovyo sana yaani ulioamini umasikini (unyonge) ndio fahari.

Ajabu ni kuwa wajinga bado ni wengi ambao walitumiwa kama mtaji wa kisiasa.
😀😀😀Nchi ilipata pakavu sana aise
 
NB, Ifikapo 2025 kaskazini haina chaguo zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan hii ni ndani na nje ya CCM, Kama kweli tunatamani kuiona kaskazini yetu inamea kwa kasi,

Usitupangie..

Tutachagua Kwa kadri ya Matakwa yetu.
 
Nakuombea ujazwe roho mtakatifu ili urudi kufanya editing.
Huu uzi umekaa kibaguzi kibaguzi hivi..watanzania wenzangu tuachane na mawazo ya kikanda, kikabila, au kidini..mawazo Kama haya hayataipeleka nchi yetu mbele..Tukatae ubaguzi wa aina yoyote ile kwenye nchi yetu..na tumuunge mama mkono kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuijenga nchi yetu.. Kwenye bandiko ametaja mtu na kabila lake kitu ambacho si sawa kwa umoja wa nchi yetu.
Kwa taarifa tu kwa mleta uzi..mpaka huku Kanda ya ziwa Kuna miradi mikubwa mno inayofanywa na serikali ya mama Samia..
Shime ndugu zangu Watanzania tusibaguane kwa dini, Kanda au kabila..na tuwakataee kwa nguvu zetu zote watu wote wanaotaka kupanda mbegu ya ubaguzi kwenye nchi yetu
Hongera mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa unayoifanya ya kuwaleta Watanzania wote pamoja..
Kazi iendelee
 
Yeye alichukia ubadhilifu ikatokea bahati mbaya wabadhilifu waliowengi wakawa wanatokea huko

Hakuna ubishi hawa jamaa walijinufaisha Sana kwakutumia nafasi zao na walitumia vema fursa zao na kuwabeba NDUGU zao.

Kilichofanyika ni kupulizia dawa ya sumu kwenye shimo walilojificha matokeo yake waliumia wadudu wanaofanana
 
Mama anaupiga mwingi 15 mingine tena kwake
Rais Samia ndio mtu Sahihi 2025 kama kweli tunahitaji na sisi wa kaskazini kutambulika kama WATANZANIA,

Hii tupende tusipende, Ila tukiendelea na ma-CHADEMA yetu tutabaki wa hivi hivi tu,
 
View attachment 2203354
Tanzania tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi miongo mitatu iliyopita,

Kanda yote ya kaskazini imeanguakia kwenye mikono ya Upinzani na wapinzani,

Hayati Rais Dkt Benjamin William Mkapa ndio Rais wa kwanza kuonja shubiri ya Upinzani na Wapinzani Tanzania,

Mpinzani wa kwanza strong wa CCM alitoka kanda ya kaskazini Mkoa wa Kilimanjaro,

Mhe Dkt Augustine Lyatonga Mrema Mchaga wa Kiraracha Vunjo ndio Mtanzania wa kwanza aliyeitikisa CCM vilivyo,

Mhe Dkt Augustine Lyatonga Mrema Mchaga wa Kiraracha Vunjo aliwahi kuwa mgombea tishio wa Urais wa JMT kupitia Chama cha NCCR -Mageuzi,

Tangu enzi za Mchaga Dkt Augustino Lyatonga Mrema hadi sasa kwa akina Freeman Mbowe wa CHADEMA mchaga wa Machame Vyama vyote 19 vya Upinzani 83% vinaongozwa na watu kutoka Kanda ya kaskazi,

Kanda nzima ya kaskazini imekuwa ikionesha Upinzani mkubwa kwa CCM karibu katika kila chaguzi tangu Uchaguzi wa mwaka 1995,

Marais wote walioiongoza Tanzania baada ya mfumo wa Vyama vingi walichagua zaidi kuitenga kaskazini licha ya kaskazini kuwa mbele kimaendeleo kulikofanya na wamisionari hata kabla ya Tanzania kupata Uhuru,

Hali ilikuwa mbaya zaidi awamu ya tano pale ambapo Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli alipotamka hadharani kuwa kaskazini inapashwa kusubiri ili na maeneo mengine nayo yapate maendeleo,

Leo mambo ni tofauti sana kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwani amemwaga miradi ambayo haijawahi kushuhudiwa huko kaskazini tangu Uhuru wa nchi hii,

Kuhusu miradi lukuki ya mabilioni inayojengwa na Rais Samia Suluhu Hassan kanda ya kaskazini nadhani kila anayeishi mikoa ya Tanga, K'njaro,Arusha na Manyara atakuwa shahidi wa yeye mwenyewe,

Nilipoona Rais Samia tena ameichagua na kuiheshimisha Arusha ya kaskazini kwa kuipa heshima kubwa ya Uzinduzi wa "Tanzania Royal Tour Film " hapa Tanzania,

Huu ukawa ushahidi wangu mwingine ulioondoa chembe ya shaka kuwa Rais wa Awamu ya Sita Mhe Samia Suluhu Hassan anaipenda sana kanda ya kaskazini kuliko Marais wote waliowahi kuiongoza Tanzania baada ya mfumo wa Vyama vingi mwaka 1992,

Mtakumbuka Rais Samia baada tu ya kuapishwa alikwenda Arusha na akatoa zaidi ya TZS 500BL sawa 80% ya bajeti nzima ya Wizara ya Maji ya Tanzania nzima akawapatia Arusha kwaajili ya Mradi mkubwa wa maji uliokwama tangu enzi za Rais Jakaya Kikwete,

Haya yote yawafungue macho wananchi wa mikoa ya Tanga, K'njaro, Arusha na Manyara kuwa CCM ya Awamu ya Sita Chini ya Mkt wake na Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan inawapenda sana,

Lazima Wafahamu kuwa hivi vyama vya Upinzani wanavyovikumbatia ndio haswa mchawi wao kwenye maendeleo yao hasa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi,

Kaskazini msipomuunga mkono huyu Mama itawachukua miaka mingi sana kupata mtu wa msaada kwenu kama huyu Mama,

NB, Ifikapo 2025 kaskazini haina chaguo zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan hii ni ndani na nje ya CCM, Kama kweli tunatamani kuiona kaskazini yetu inamea kwa kasi,
Rais Samia anatupenda mno kaskazini
 
Kipindi cha sita Ndio kaskazini ilibandikwa UGAIDI halafu kama movie wakamchomoa.
Yaani WANAKUROGA halafu WANAKUAGUA. Hili kupanda huruma na upendo wa Kaskazini
 
Adui wa Adui yako ni rafiki wa kimkakati.
 
Back
Top Bottom