Unaongelea kina nani?maana zanzibar haikuwa na waarabu wala ngoz nyeupe yoyote, walituvamia na kututawala kimabavu kupitia Usultan
Historia haifutiki ya ukombozi wa visiwa vyetu vya Zanzibar kutoka katika makucha ya Wareno. Oman baada ya wao kujikombowa na madhila chini ya utawala
wa Kireno kutoka 1508 hadi 1631 ndio ikawa sababu ya
kukombolewa Zanzibar.
Imam Seif alifanya ukombozi wa visiwa hivi. Alikubali maombi ya wazee wa Visiwa hivi na akatuma majeshi na kwenda Mombasa na kuishambulia
Ngome ya Yesu katika mwaka 1661. Majeshi hayo ya Waoman waliuteka mji wa Mombasa lakini hawa kuweza kuwafukuza Wareno.
Mtawala mpya wa Oman alipopatikana Imam Seif bin
Sultan Al Yarubi (Qaidul Ardh) akatuma majahazi 18
yenye jumla ya askari 3000
kutoka makabila mbalimbali
ya Mashariki ya kati yakiongozwa na Jemedari
Mkuu wa kabila la kibulushi
Kutoka pwani ya Makarani
Jimbo la Baluchistan la Uajemi. Jemedari Amir Shahdad Chotah.
Tunakumbuka historia ya watu wa Oman na tunajuwa
na kuthamini roho za raia zao waliopoteza maisha yao kwaajili yetu Wazanzibari na hatutaweza
kusahau mchango wao watu wa Oman.
Hatutawasahau wazee walio kwenda Oman kuomba msaada wa Jeshi la kuja kutukombowa kutokana na unyama na mateso ya Wareno waliowatendea wazee wetu wa hapa Zanzibar na wa huko Oman.
UJUMBE WA WATU 8
1) Mwinyi Nguti wa Mwinyi
Mwinzangu, mzee wa Waswahili wa Mombasa.
2) Mwishihali Bin Ndari
3) Maalim Ndao Bin Haji
4) Mwinyi Mole Bin Haji
5) Shekh Ahmed Al - Malindi
6) Mtomato wa Mtorogo
7) Kubo wa Mwamzungu
( mzee wa kidigo)
8)Shahame Bin Shoka
(wa kisiwa cha Pemba)
Mwenyezi Mungu awarehemu na kuwalipa pepo maana ndio sababu ya Uislamu ukatamalak visiwani petu. Kama si Rehma zake Mwenyezi Mungu leo tungali kuwa na msalaba vifuani mwetu.
KARIBU sana Mfalme wa Oman Zanzibar tungelifurahi kama ungelitutembelea hapa visiwani. Tunamuomba Rais wetu Hussein Mwinyi aione historia yetu na ya Waoman kwa moyo na jicho lenye faraja na aweze kumualika Mfalme wa Oman kuja tembea katika visiwa vyetu vilivyo Sheni utamaduni wa nchi mbali mbali khususana wa watu wa Oman.