Kwanini historia anayosimulia Sheikh Mohammed Said haipingwi hadharani?

Watanganyika wa Dini zote waligombania UHURU na wengine walikuwa na Agenda zao wenyewe.

Sidhani hao akina Sykes kama Mkoloni angekuwa ni Sultani wa Kiarabu sidhani kama wangedai UHURU.

Ilibidi JOHN OKELLO awasaidie huko Zanzibar kumng'oa Sultani wa Kiarabu.
 
Watanganyika wa Dini zote waligombania UHURU na wengine walikuwa na Agenda zao wenyewe.
IMHO....
Unaweza kuweka majina yao hapa hao wapigania uhuru wengine?

Mimi nimewataja wengi katika kitabu cha Abdul Sykes: Shariffa bint Mzee, Zarula bint Abdulrahman, Tatu bint Mzee, Mama bint Mwalimu, Nyange bint Chande, Amina Kinabo, Fatma bint Matola, Hawa bint Maftah, Halima Selengia, Halima bint Khamis...

Bibi Titi Mohamed.
Nasubiri orodha yako.
 
Wewe Ni msomaji wa JF kweli? Maana nakumbuka watu wamempinga na kupongeza Sana. Kabla ya kuandika fanya uchunguzi kwanza
 
Kinasomeshwa Uganda na Kenya kwenye misikiti au kwenye mtaala wa elimu ya sekondari/ msingi.

Nawashukuru waliokupiga stop Tanzania usieneze itikadi yako mbaya
Huihui,
Kwanza unajua hatua mswada unapitia hadi Oxford wanachapa kitabu?
Ningeweza kusema mengi lakini ya nini.

Kitabu hiki "The Torch on Kilimanjaro," sasa kimechapwa mara mbili na watoto wa shule za msingi Kenya na Uganda wanakisoma.

Nimetosheka na hili.


Toleo la Kwanza

Toleo la Pili
 
Uchuro huo nani anataka?? Waislamu wanaotaka kusoma wanajuwa vitabu vya kusoma lakini hawahangaiki na hiyo itikadi ya mzee Mohamed
Hui...
Nimepokea tuzo tatu kutoka kwa Waislam kwa kuhifadhi historia.
Hapa JF nimechaguliwa Mwandishi Bora mara mbili.

Jumla tuzo tano.

Kitabu cha Abdul Sykes kimechapwa mara nne toka 1998 na tunakwenda toleo la tano.

Kwa miaka 25 kitabu hiki kinajadiliwa.
Hili si jambo la kawaida.




Maxence Melo akinikabidhi cheti
 
Mkwawa Kinjekitile Ngwale John Okelo Chief Songea Milambo nk. nk.
 
Historia anayoizungumza Mzee Mohamed Said ni ya Waislam. Hiyo inapaswa kugundishwa Madrasa kama wana mitaala ya historia. Na wa kumjibu ni Waislam maana ndiyo waliozungumziwa humo kwenye historia yake
 
Historia anayoizungumza Mzee Mohamed Said ni ya Waislam. Hiyo inapaswa kugundishwa Madrasa kama wana mitaala ya historia. Na wa kumjibu ni Waislam maana ndiyo waliozungumziwa humo kwenye historia yake
Je Waislamu sio Watanganyika?! Tunataka Historia ya Watanganyika.
 
Mambo mengine kuyajadili ni kupoteza muda tu, Historia ya Wazee wa Kariakoo ijadiliwe huko huko kariakoo. Nyerere aliona mbali sana
Nyerere yule mkatoliki kinoma na mdini nambari moja
 
Nyinyi eti Mchungaji wenu ni Nabii Tito
 
Mkwawa Kinjekitile Ngwale John Okelo Chief Songea Milambo nk. nk.
Imh...
Nami nakuongezea wengine katika orodha yako na kukupa taarifa zaidi.
Mkwawa jina lake ni Abdallah.

Nduna Songea Mbano jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano.
Hassan Omar Makunganya.

Pamoja na wengine walionyongwa na kuzikwa katika kaburi la halaiki baada ya Vita Vya Maji Maji ni Mkomanile.

Huyu ni mwanamke pekee aliyekuwa jemadari katika Vita Vya Maji Maji.
Siku zote anatajwa kwa jina moja tu Mkomanile.

Jina lake ni Khadija Mkomanile.

Lakini kabla ya kunyongwa alifika Fr. Yohannes Hafliger kutoka Peramiho Mission akawaambia hawa wazalendo wapatao 67 kuwa wakikubali kubatizwa na kuwa Wakristo hukumu ya kifo itafutwa.

Khadija Mkomanile akapewa jina jipya la Yacintha jina la Khadija likafutwa na kwa wengine ikawa ni hivyo.

Wote wazalendo 67 wakanyongwa.
Naamini umejifunza kitu hapa.
 
sawa lets research yako na wewe iliyobase na kutoka wigo mpana zaid. mim nahangaika na research najua ugumu wake
leta yako mtaalam.mana kama ni kutoka mr mohamed katoka kila kona kuanzia southern province. kaenda mpaka ukerewe kawataja kina dennis phombea.kawataja kina john rupia kila mtu kaelezwa kwa ushiriki wake. unapotaka history iwe moulded into your own views inakua sio historia hio.historia inajiandika yenyewe.wqcha kujitia pambani .kasome Mein Kampf so utakuja kulalamika mbona historia imebase germany tu ilhal mfano vita vilipiganwa dunia nzima? historia imerekebishwa kila.mshirik ametambulika.sote tumesoma jukwaan hapa tumejua wazee hawa walijitoa kwa vile hawakua na white collar job walikua hawana cha kupoteza wakina mshume kiyate.tunasomeshwa kuwa southern provinces ni umoja wa madobi ndio ulianza harakat. waliokuwa wameajiriwa na mkoloni walikuwa hawatak kabisa kusikia hrakati na hata mission zilikua zinakataza mambo hayo ndio mana hutasikia mahali mission fulan kuligawiwa kad za tanu ila misikitin mikutano ya tanu na kadi ziligawiwa
 
Hayo ni majina tu,hatujui waliyapataje labda kwa hofu ya kuogopa Arab Slave Trade hata leo ukienda Usukumani Selemani na Hamisi wako wengi tu lakini wanaabudu Mizimu ya Babu zao.
 
Hayo ni majina tu,hatujui waliyapataje labda kwa hofu ya kuogopa Arab Slave Trade hata leo ukienda Usukumani Selemani na Hamisi wako wengi tu lakini wanaabudu Mizimu ya Babu zao.
Wewe sasa umevaa jezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…