Kwanini historia anayosimulia Sheikh Mohammed Said haipingwi hadharani?

Kwanini historia anayosimulia Sheikh Mohammed Said haipingwi hadharani?

Sisi hatutaki historia ya wazee wake wala historia ya uislamu tunataka historia ya Tanganyika/Tanzania... as general
Inside10,
Historia ya hawa wazalendo niliowataja katika kitabu cha Abdul Sykes ndiyo historia ya Tanganyika.

Labda uikatae kwa kuwa si historia uliyofunzwa.

Huwezi kuandika historia ya vyama vya wafanyakazi kama hujamtaja babu yangu Salum Abdallah na Kassanga Tumbo viongozi wa TRAU na pia wanachama wa TANU.

MACHACHE KUHUSU BABU YANGU SALUM ABDALLAH
Salum Abdallah babu yangu akifanyakazi Loco Shed Tabora maarufu kwa jina la Baba Popo.

Alihamia Tabora kutoka Dar es Salaam baada ya Loco Shed kuhamishwa kutoka Dar es Salaam mwaka huo wa 1947.

1955 yeye na Kassanga Tumbo walianzisha chama Tanganyika Railways African Union (TRAU).

Salum Abdallah akiwa President na Kassanga Tumbo Secretary.

TRAU ina historia kubwa sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
TRAU ilifanya mgomo mwaka wa 1960 uliodumu siku 82.

Salum Abdallah aliongoza mgomo huo wa wafanyakazi wa Railways uliodumu miezi mitatu.

Kwa miezi mitatu treni, meli na mabasi ya Railway yalisimama hadi Waingereza waliposalimu amri na kuwaita viongozi wa wafanyakazi katika meza ya majadiliano.

Uhuru ulipopatikana babu yangu akapambana kwa fikra na msimamo wa Nyerere kuhusu vyama vya wafanyakazi Nyerere akitaka viwekwe chini ya TANU na viongozi wa vyama vya wafanyakazi pamoja na babu yangu wakipinga wazo hilo.

Yalipotokea maasi ya wanajeshi tarehe 20 Januari 1964 baada ya maasi kuzimwa na jeshi la Waingereza, Nyerere aliwakamata viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi na kuwaweka kizuizini.

Babu yangu alifungwa kwenye jela ya Uyui, Tabora na alipotoka kizuizini Tanganyika Railway African Union (TRAU) chama alichokiasisi mwaka wa 1955 kilikuwa kimepigwa marufuku pamoja na vyama vingine vya wafanyakazi na badala yake kimeundwa chama cha National Union of Tanganyika Workers (NUTA) kwa juhudi kubwa za Rashid Kawawa na Michael Kamaliza.

Babu yangu alihama Tabora na kwenda Urambo kupisha shari kwani zilienezwa taarifa za uongo kuwa yeye alikuwa katika kundi pamoja na Victor Mkello (kiongozi wa wafanyakazi wa mashamba ya mkonge) na Kassanga Tumbo walikuwa wamekula njama ya kupindua serikali na kumuua Rais Nyerere.

Babu yangu akajikita katika ukulima wa tumbaku Urambo huku akiendelea na ukulima wake wa miaka yote Kakola na Uyui Tabora.

Fredrick Mchauru aliendelea na utumishi katika serikali ya kikoloni na uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961 alishika nyadhifa mbalimbali katika serikali huru kama zilizvyoelezwa katika makala zilizochapwa na Raia Mwema.

Kama mimi nisingeaandika kitabu cha Abdul Sykes huenda historia hii ya babu yangu na wazalendo wengine isingejulikana na historia ambazo zingesomwa ndiyo hizi za watu kama Fredrick Mchauru na wengineo.

Salum Abdallah alifariki mwaka wa 1974 akiwa na umri kama miaka 80 akiwa mkimya sana kwa kuwa hapakuwa tena pale mjini na barza zilizokuwa zikijadili siasa kama miaka ya 1950 wakati wa kudai uhuru.

Siasa ilikuwa sasa jambo la kutisha watu wakihofu kukamatwa na kuwekwa gerezani.

Babu yangu akiungulia ndani kwa ndani kwa chuki dhidi ya TANU chama alichokiendea mbio na kuhudhuria mikutano yake yote ya siri mwaka wa 1953 pamoja na wazee wenzake akina Maulidi na Abdallah Kivuruga, Rajab Saleh Tambwe, Abubakar Mwilima kuwataja wachache, na kuwa mmoja wa waasisi wake mjini Tabora mwaka wa 1955.

Siku zote yeye baada ya kuona vyama vya wafanyakazi vimekwa chini ya TANU na serikali yake aliwaona viongozi wapya wa vyama hivi vibaraka wa serikali hawataweza kupigania haki za wafanyakazi kwa dhati.

Picha: Kulia ni Christopher Kassanga Tumbo anaefuata ni Salum Abdallah.

 

Attachments

  • 1724855793830.jpeg
    1724855793830.jpeg
    83.9 KB · Views: 4
sawa lets research yako na wewe iliyobase na kutoka wigo mpana zaid. mim nahangaika na research najua ugumu wake
leta yako mtaalam.mana kama ni kutoka mr mohamed katoka kila kona kuanzia southern province. kaenda mpaka ukerewe kawataja kina dennis phombea.kawataja kina john rupia kila mtu kaelezwa kwa ushiriki wake. unapotaka history iwe moulded into your own views inakua sio historia hio.historia inajiandika yenyewe.wqcha kujitia pambani .kasome Mein Kampf so utakuja kulalamika mbona historia imebase germany tu ilhal mfano vita vilipiganwa dunia nzima? historia imerekebishwa kila.mshirik ametambulika.sote tumesoma jukwaan hapa tumejua wazee hawa walijitoa kwa vile hawakua na white collar job walikua hawana cha kupoteza wakina mshume kiyate.tunasomeshwa kuwa southern provinces ni umoja wa madobi ndio ulianza harakat. waliokuwa wameajiriwa na mkoloni walikuwa hawatak kabisa kusikia hrakati na hata mission zilikua zinakataza mambo hayo ndio mana hutasikia mahali mission fulan kuligawiwa kad za tanu ila misikitin mikutano ya tanu na kadi ziligawiwa
Ushauri:
Jifunze kwanza kuandika uandikaji wako unachosha,hata ulichokiandika sijakisoma.
 
The same question

Kwanini historia inayosimuliwa na Nabii Tito haipingwi hadharani?

 
Huihui,
Kwanza unajua hatua mswada unapitia hadi Oxford wanachapa kitabu?
Ningeweza kusema mengi lakini ya nini.

Kitabu hiki "The Torch on Kilimanjaro," sasa kimechapwa mara mbili na watoto wa shule za msingi Kenya na Uganda wanakisoma.

Nimetosheka na hili.

View attachment 3081509
Toleo la Kwanza
View attachment 3081512
Toleo la Pili
Waache Wakenya na Waganda wasome matakataka lakini siyo sisi
 
Kasome kitabu cha Padri savillon, Kanisa Katoliki na siasa Za Tanzania bara
Umenukuu swali langu ninachotaka ni Majibu kama wewe ndio umeona unijibu basi nenda kwenye hicho Kitabu ukanukuu jibu ninalolihitaji kisha uliweke hapa kwa manufaa ya wasomaji na wachangiaji wote.
 
Umenukuu swali langu ninachotaka ni Majibu kama wewe ndio umeona unijibu basi nenda kwenye hicho Kitabu ukanukuu jibu ninalolihitaji kisha uliweke hapa kwa manufaa ya wasomaji na wachangiaji wote.
Wacha uvivu , Mimi si mchungaji wako ,
Hilo jibu Kama unalitaka katafute kitabu
 
Kweli si nafuu kwani , huyo mama ametoka kwa maandamano ya Mbowe na Lissu wake, Hao watu alisema Mbowe waliouliwa na kupotea wamerejea? Ulisahau kuwa kaondoshwa Nape na Makamba wamerudishwa walewale akina Kabudi na Lukuvi. Pole sana endelea kukimbiza mwenge ukumulike mchana
Unapuyanga tu wala hufuati mada. Wewe umetamani Kenya kwa kuiona ya maana kuliko Tanzania , mimi nimekujibu kuwa ujuwaji wao hauna tija mwisho wa siku. Sasa ya Mbowe, Lukuvi yanatokea wapi
 
Comments ndo zitakueleza watanzania ni watu wa aina gani.

We soma comments tu
 
Back
Top Bottom