"Pascal Mayalla, post: 33635440, member: 17813"]
Mkuu Nguruvi3, Mkuu Maalim Mohammed Said ni very controversial kwenye baadhi ya hoja zake, na kila akileta any controversial issue, ukihoji, kwake ni kama kumpiga chura take, anakumwagia nondo na nyingine ni zenye maurongo ndani yake.
Hoja ya Thani ameileta makusudi kufunika hoja ya Utumwa, Uarabu na ushiriki wa Sultan
Alijaribu kutumia TransAtalantic slave trade kutuondoa katika mstari tukamwambi huko sipo
Akatupeleka Kipumbwi tukamwambia tunakwenda, tukaishia mapinduzi daima na Sultan safi
Hapa kukawa na utata, ni ''double edged sword'' ima kumkubali Sultani na kuwakana Wamatumbi au kuwakubali wamatumbi na kumkana Sultan.
Ni ngumu, makundi hayo yanaunganishwa na kitu kimoja chenye ''interest'' kwake'
Ndio maana hawezi kusema mapinduzi ni halali au ni haramu, anafanya ''insinuation'' tu
Katika kubabisha anatuletea Picha ya Okello bila kutueleza ilipigwa lini, wapi na hao ni akina nani aliokaa nao.
Halafu anataka watu watambue Wazanzibar ''khalisi''
Kwanza hakuna kitu kinaitwa Mzanzibar khalisi tumemuuliza atueleze yupo je, kachikia
Pili kasema aliyepanga mapinduzi ni Abdallah Kassim Hanga.
Kama ndivyo, Hanga ndiye aliye organize watu kutoka Kipumbwi kwenda kumuondoa Sultan
Tatu, anasema anamfahamu Hanga .
Ikiwa ni hivyo, wazee wa Dar walijua mipango ya Hanga kupeleka watu kutoka Kipumbwi.
Nne, anasema Okello si lolote si chochote.
Ikiwa ni hivyo, kwanini alipewa kazi ya kutangaza Mapinduzi?
Je, wahusika akina Hanga walikuwa wapi na waliogopa nini?
Tano, je watu 12 wa mwanzo wa baraza la Mapinduzi walikuwa Wazanzibar ''khalisi'' au la
Watu wanadhani tupo hapa kumpinga MS, la hasha! tunachofanya ni ''ku-critic'' historia jambo la kawaida kabisa katika mijadala. Sasa kukiwa na disjointed story watu wasiseme!
Kama kuna upotoshaji kuna ku''debunk' hoja na ngano, si kumeza mazima
Katika utata na asivyoweza kutetea hoja bado anataka historia ya 'kweli'' ifundishwe