Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Kwani sahivi nani analipia zote
Mwenye ardhi analipa kodi ya ardhi. Kampuni inalipa corparate tax, mtumiaji wa mwisho wa bidhaa au huduma analipa VAT n.k

Kuna sifa za kodi, mojawapo ni lazima iwe kisheria, imlenge mhusika mwenye sifa fulani n.k

Okey, Endelea na majibu.....
 
ARDHI ni mali ya Serikali ukitaka ukae bure basi usiitumie ardhi hiyo kwa kujenga ukijenga tu serikali lazima ikutoze kodi kwa hiyo AMUA
 
ARDHI ni mali ya Serikali ukitaka ukae bure basi usiitumie ardhi hiyo kwa kujenga ukijenga tu serikali lazima ikutoze kodi kwa hiyo AMUA
Basi hata hewa ni mali ya serikali?
Ujue haya mambo siyo msaafu! Ni kujadili tu kama ilivyokuwa kodi ya kichwa zamani!
Kila kijana wa kiume alitakiwa kulipia kodi ya kichwa!
Tulilalamika Ikafutwa kwasababu haikuwa na TIJA kama hii kodi ya pango la ardhi
 
Kwasababu ardhi ni mali ya Watanzania wote, unalipa kodi kuhalalisha kuachiwa uitumie, maana watanzania wenzako wanayo haki kumiliki hicho kiardhi unachomiliki
 
Mifumo tu ya ajabu ajabu ya kurithi alafu wahusika vitu kama hivi hawavipitii waone kama wanaweza kurekebisha
Kwann serikali isiwe msimamizi tu baada ya kukuuzia
 
Mtoa mada Ukifika mbinguni ulizia Malaika wa Misukosuko utanipata nina Divai kwaajili Yako. 👏👏
 
TRA Wameshafanya yao sahivi hupati umeme hadi ulipie kodi ya jengo
 
Kumbe ardhi ni bure kisa kaumba Mungu mbona mimi sina Basi ngoja nikajikatie kipande changu pale posta na mimi niwe naye
Wenzako walisha wai hapo posta,zamani pia palikua pori, tafuta na wwe pori lako!!
 
Kodi ya majengo kuanzia mwezi huu wameipandisha tena kwa 50% ...kupitia manunuz ya umeme
 
Wana copy kodi za Ulaya harafu makusanyo ya Kodi ni kuiba tuu kila kukicha hakuna kinachofanyika kila mwaka inatoka taarifa ya CAG ya wizi harafu wahuni wanabaki kuongeza kodi ya pangolin kwenye Umeme ili wapate za kuiba ziwe nyingi ukiwauliza kwa nini wameongeza hawana majibu wezi wakubwa...
 
Ardhi, ni mali ya Watanzania wote, wewe unapojitwalia ardhi maana yake wezako hawawezi kupata hiyo ardhi maana ushakuwa yako, hivyo kuleta usawa inabidi uilipie kodi ila uwe na haki ya kihalali ya kumiliki hiyo ardhi maana yake ni kuwa kodi unayo lipa ndio inakuwa uhalali wa kuwa mmiliki wa eneo lako unalomiliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…