Mambo mengine mtu ukiwaza unaona kabisa maisha ni mepesi kimtindo lakini kuna baadhi ya wanadam wenye dhamana ya uongozi ndiyo waliyoyafanya maisha yawe magumu!
Tumeumbwa ardhi ilikuwapo, tumepata Uhuru, ardhi ilikuwapo milele hadi milele yote!
Sasa kwanini tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati tayali ipo BURE?
Huduma zingine za kijamii tunazolipia naelewa ni sawa zinazalishwa viwandani hivyo ni mhimu kulipia!
Sasa hili la kodi ya pango ya ardhi kwanini tulipie wakati tumekuja duniani ili tuishi kwenye ardhi halisi BURE?
Yaani kwa lugha nyepesi Ardhi ipo kundi moja na hewa! Kama tunalipia kodi ya ardhi kwanini tusilipie na kodi ya hewa?
Naomba kueleweshwa! Vinginevyo naomba serikali ifute hii TOZO ya ARDHI ya ardhi mara moja!
Ardhi Haipaswi kabisa kutozwa kodi TUMEPEWA BURE. WACHA TUISHI NAYO BURE!