Dr. Mariposa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,264
- 10,535
Hii ndio sababu tunalipishwa Ardhi?Ni kwa sababu unapotumia ardhi unamnyima mwingine fursa ya kuitumia hiyo ardhi.
Usingeweka wewe nyumba juu ya hiyo ardhi ningeweka mimi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ndio sababu tunalipishwa Ardhi?Ni kwa sababu unapotumia ardhi unamnyima mwingine fursa ya kuitumia hiyo ardhi.
Usingeweka wewe nyumba juu ya hiyo ardhi ningeweka mimi
Shukrani sana The Broker kwa ufafanuzi,Ardhi ni Mali ya umma, na Rais ndo amekabidhiwa kama msimamizi thus wote tumekodishiwa kutumia tena kwa muda maalum. Ndo mana kuna hati za miaka 33, 99 ndo mana tunalipa kodi. Ukipata muda pitia sheria ya, Ardhi ya mwaka 1999 na maboresho yake.
Shangaa na wewe Dr.Hii ndio sababu tunalipishwa Ardhi?
Hapa sasa umeeleweka,Kinacholipiwa kodi ni UMILIKI; OWNERSHIP. It is entitled to you and not to someone else. Kikishakuwa ni chako mwingine hana fursa nacho sharti ukilipie. Hiyo ndio kanuni.
Na ndio maana maeneo ya public hayalipiwi kwa sababu ni free to everybody kama ilivyo hewa.
Sijui unaongea kitu gani! Serikali kwamba imeweka dola kulinda eneo langu!Kodi ya pango la ardhi inatozwa ili wewe mmiliki upate ulinzi wa dola katika kipande chako za ardhi. Bila ulinzi wa dola mtu mwingine ye yote mwenye nguvu za misuli au fedha anaweza kuvamia eneo lako na kukunyang'anya na ukakosa wa kukusaidia.
Hivyo serikali inatoza kodi ili iendelee kukulindia kipande chako unachomiliki. Na kwa kufanya hivyo kupunguza migogoro ambayo ingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mungu ni suala la dini, Serikali haina mambo ya dini ina Jeshi.Ndio ni kwa mujibu wa hao wakusanya kodi ndio waliitunga hiyo sheria,lakini bado swali la mtoa mada litabaki palepale ni kwa nini iwe hivyo wakati ardhi yote iliumbwa na Mungu ili binadamu waitumie?
kwani kisima chako umechimba unalipia nini tenaKisima nilichochimba mwenyewe nyumbani kwangu
Mungu ni Mungu na dini ni dini.Mungu ni suala la dini, Serikali haina mambo ya dini ina Jeshi.
Suala la kodi zipi ziwepo na zipi zisiwepo ni suala la sheria. Hatuna kodi ya hewa ila tulikuwa na kodi ya kichwa kilichobeba pua na mdomo inayovuta hewa, tukaifuta. Hata ya ardhi tunaweza futa.Kwa nini tukodishwe na Serikali wakati Ardhi tumeikuta na Kama ilivyo hewa ndio urithi wa mwanadamu?
Kama tunakiri kuwa wakoloni walitwaa ardhi zetu, wakagawa vipande na kuweka Serikali zao, zikajiendesha kwa kodi za dhulma kama hii, kwa nini Serekali yetu inaendeleza ukoloni ule ule kwa watu wake?
Wanasema sheria yaliyochini ya kiwanja chako hutakiwi kuyavuna pasipo kibari na kulipia kodi ya kisima (bonde)kwani kisima chako umechimba unalipia nini tena
Ndo tunarudi pale pale kuwa huwezi sema serikali ifute hiyo kodi sababu ardhi tumepewa bure na Mungu.Mungu ni Mungu na dini ni dini.
Kwani kuna mtu ambaye hajui kwamba ardhi iliumbwa na Mungu?bila kujali dini yake ni ipi
Ungesema serikali hawana Mungu labda ila ukisema hawana dini bado wanaye Mungu ambaye anawawezesha kuamka kila siku asubuhi na kwenda kutunga sheria.Ndo tunarudi pale pale kuwa huwezi sema serikali ifute hiyo kodi sababu ardhi tumepewa bure na Mungu.
Serikali inataka mapato na ili ufute hayo mapato unahitaji mbadala wa hayo mapato. Ukija na stori za Mungu jibu ni jepesi tu serikali haina dini.
Hata kama hana dini! Hiyo ardhi akiiona anafikili iliagizwa ulaya? Ardhi ni urithi tumerithishwa ili tuwarithishe wengine kwa kupeana fidia! Ni kitu ambacho kipo pasipo hiari yetu!Mungu ni Mungu na dini ni dini.
Kwani kuna mtu ambaye hajui kwamba ardhi iliumbwa na Mungu?bila kujali dini yake ni ipi
Hapo unaingiza kwenye imani yako sasa boss.Ungesema serikali hawana Mungu labda ila ukisema hawana dini bado wanaye Mungu ambaye anawawezesha kuamka kila siku asubuhi na kwenda kutunga sheria.
Broh mi nasema maisha ni mepesi sana lakini kuna watu wanatuwangia! Makodi ya ajabu hata kwenye vitu vya bureNdiyo mana wana jeuri ya kununua magari ya kifahari na likipata jeraha tu wanauziana wenywewe,
Unapanga frem na Bado unaambiwa
ulipe tena Kodi ya pango, hiyo ni tofauti n tra na ukienda manispa unakutana na Kodi ukirudi mtahani kuna Kodi tena ya taka na ulinzi Bado mitaro unasafisha!
Alafu unaambiwa vijana mkaajiajiri wakati ukifungua duka hata ujaanza tu unakadiriwa Kodi!
Wala sijachanganya mada,kuna mtu nilikuwa nimemjibu hiyo comment,aliniambia kuwa mimi sijui umuhimu wa kodi wala maana ya kodi ndio nikamjibu yeye anayejua umuhimu wa kodi ameona wapi hiyo kodi ikifanya kazi ipasavyoAna changanya! Hakuna anaepinga kodi! Tatizo unachukua kodi kwenye nini!
Mfano kodi ya mifugo, kodi ya ardhi, kodi ya jengo zote hizi hazina tija kabisa ni wizi!
Already existing on its nature! Kwanini uombe kodi!
Zamani kulikuwa na kodi ya kichwa! Vyote hivi ilikuwa ni unyama wa hali ya juuu! VIFUTWE VYOTE
Boss, kodi ya ardhi ipo kisheria kupitia bunge lako tukufu. Hakuna aibu hapo kuna sheria. Kama hatuitaki ni suala la kushinikiza mbadala bungeni pawepo mswada sheria ibadilike.Hata kama hana dini! Hiyo ardhi akiiona anafikili iliagizwa ulaya? Ardhi ni urithi tumerithishwa ili tuwarithishe wengine kwa kupeana fidia! Ni kitu ambacho kipo pasipo hiari yetu!
Ardhi ni ya wote, usipotaka utaikanyaga, utailima, utaivuna na mavumbini utarudi!
Sasa huyu anaetoza kodi ya ardhi hana aibu hata kidogo
Wala sijataja dini yangu hapo,niko neutral.Hapo unaingiza kwenye imani yako sasa boss.