Baada ya ishu ya CAG nikasema niingie mitandaoni nione reaction ya wananchi juu ya serikali ya JPM.
Twitter na JF kama kawaida ni matusi tu na kejeli kwa mwendazake, ila awa ni wachache na tumeshawazoea hawanaga madhala.
Nikasema niingie kwa majority ya wananchi huko Facebook na Instagram penye watumiaji 90% wa social media wa Tanzania.
Nikakuta vilio na kukata tamaa kwa wananchi baada ya kuona kipenzi chao JPM anazushiwa uongo na mema yake yanapondwa.
Wananchi imani yao kwa Magufuli ni kubwa sana, waite wajinga awajaelimika ila kuna namna JPM aligusa maisha yao na akatengeneza connection nao. Hakuna kitu mtafanya sasa hivi kufuta hii love ya raia kwa JPM.
Nawashauri CCM na wapinzani mnaoendeleza vita na JPM wasibeze hivi vilio maana awa wananchi watawaadhibu siku moja. Kumpuuza Magufuli ni kuwapuuza majority ya watanzania 93%.
Msije sema hamkuambiwa.
View attachment 1748149View attachment 1748150View attachment 1748151View attachment 1748152View attachment 1748153View attachment 1748154
Ndugu, wananchi umeelewa wanachokililia lakini? yawezekana ata hujasikia kilio cha wananchi. Ni mikumbo pengine lakini wapo wanaolia juu ya elimu bure(currently the only move done by the late kwenye elimu) Elimu bure was bogus attempt na sijui kwanini tumeruhusu elimu irudi nyuma kiasi kile. Mzee mkapa aliwahi kusema
"serikali za kiafrika zikiingia madarakani hudhani kila kilichofanywa na serikali zilizopita kuwa ovyo. Hakuna continuity kwenye utekelezaji"
Tulikuwa na sera nzuri sana kwenye elimu tangu nusu ya pili ya mheshimiwa mkapa na uasisi wa shule za kata wa mzee sumaye. Utekelezaji wake ulikuwa very successful Mpaka mwaka 2015 shule za sekondari zilifikia karibu 4000 Tanzania nzima 3000 more kuliko miaka 10 nyuma. Tuliongeza sana idadi ya wanafunzi mashuleni na kujongeza idadi ya walimu kwenye vituo.
Uhitaji wa walimu ni mkubwa leo kuliko uhitaji wa uhisani feki wa elimu bure ambayo in a real sense sio bure bado ni contributory kama ilivyokuwa mwanzo. Tatizo ni namna uongozi ulivyojaribu kuua kila kilichofanyika na watangulizi. Mbaya zaidi hilo lilifanywa uku likiaminisha wananchi kuwa huu unaofanyika ni msaada mkubwa sana na unafanywa na mtu aliyejitoa sana. Nimeongelea sana elimu maana nimeona namna inavyoteketea huku watu wakiaminishwa tofauti. Elimu ilifanywa siasa na hii imeitesa sana taaaluma.
Watanzania wengi hawana picha kamili juu ya ukuaji wa nchi. Wengi wanalia juu ya hearsays. watu wakifocus sana kwenye veracity ya rumours usahihi wake ni rahisi sana kupotea. Mfano watu waliaminishwa juu ya ukuaji wa uchumi na saga ya uchumi wa kati. very cheap political moves. Wanaolia wapo wanaosema kuwa tulienda uchumi wa kati and stuffs. Usahihi wa hili upo kwenye vitabu. Ukisoma DIRA 2025 utaona umuhimu wa uhuru wa kuihoji serikali. Tuna nguzo nne kwenye dira yetu ya maendeleo atleast all of them zimeguswa vibaya. Hakuna cha maendeleo ya watu, utawala bora wala ukuaji wa kiuchumi vilivyoachwa(ikiwa utakuwa mvivu kusoma tathmini za mpango wa 1 na 2 wa maendeleo tutajadili hili kwa kina)
Wapo wanaolia juu ya miradi. About 3000 kilometers za lami for 5 years. A good move lakini sio Godly move. wengi wa wanaolia wanaamini asilimia kubwa ya hizi barabara zimejengwa kipindi cha miaka 5 iliyopita. Binafsi nimesikia ata wabunge wakisema hili(labda ni zile zile cheap politics) nchi hii ina karibu kilometer elfu 13 (13,000 kms) za lami. shida ya miradi hii ni ugawaji wa tenda zake, uhalisia wa utekelezwaji wake, ushirikishwaji wa stakeholders na uhalisia wa gharama. Hili lilionywa na wengi sana humu kuwa transparency inahitajika kwenye utekelezwaji wa miradi ya kimkakati.
Dhana nzima ya utawala bora ilianza kupotea. Wapo walioamini zaidi kwenye kusikia kuliko kusikiliza. utaambiwa bunge live linafanya watu wasifanye kazi ila kila saa 1 TBC wako live wanazindua miradi.
Nchi haikupaswa kuongozwa kwa kulinda hadhi ya mtu juu namna anavyoonekana. Hata image yako ikiwa mbaya ila ukiwa na lakusema ipo mahali utalisema. Angesimama Hayati Benjamin Mkapa kukwambia juu ya sera alizofuma, transformations alizofanya, namna alivyopandisha uchumi kama ndoto ungelia sana.