Kwanini Instagram na Facebook bado wanamlilia Magufuli?

Kwanini Instagram na Facebook bado wanamlilia Magufuli?

Maombolezi lazima yaendelee. Hayati rais alikuwa mpendwa wa wengi. Hamna haja kabisa kufungia hisia
 
Jiheshimu wewe usinidogolishe kamwe na Uhuru wa ku comment jukwaa lolote pinga hoja yangu kwa hoja, hafu kwanini utumie I'd tofauti kwa huu Uzi it means huamini unachokiandika, I'm free minded person siogopi ninachoamini so acheni matusi reja reja.

Povu kama lote,ukiguswa kidogo unashindwa kuhimili joto la mjadala, ujinga wa Multiple ID’s mnao nyinyi mliovamia JF na kuja kuifanya ikawa ya hovyo hovyo,JF ya enzi hadi tunaichangia isimame haikuwaga na ujinga kama huu!
 
Watu walipotea humu baada ya Sheria za mitandao na watu kupotezwa kwa kuwa na mawazo mubadala humu, pia moderation ya content imekuwa Kali kulingana na Sheria za mitandao ndio unaona hivo.
Pia humu Kuna I'd za vyama vyote kutetea ujinga kwa masilahi mapana ya vyama vyao, Ila hyo bado haiondoi ubora wa humu mtandao kwenye kujifunza Mambo ya msingi compared na hyo mitandao mingine
Umeilingalisha vipi wakati kwa mujibu wa komenti kule juu huwa huitumii?

Hujui kuwa ukitoa thread au maoni ya upande fulani unashambuliwa kama nyuki?
Hasa jukwaa la siasa? Bora hata majukwaa mengine unaweza kujifunza kwasababu kule watu hawawi katika mlengo fulani..

Huku jukwaa la siasa unaweza kujua hata hii jf ipo na mlengo upi.
 
Baada ya ishu ya CAG nikasema niingie mitandaoni nione reaction ya wananchi juu ya serikali ya JPM.

Twitter na JF kama kawaida ni matusi tu na kejeli kwa mwendazake, ila awa ni wachache na tumeshawazoea hawanaga madhala.

Nikasema niingie kwa majority ya wananchi huko Facebook na Instagram penye watumiaji 90% wa social media wa Tanzania.

Nikakuta vilio na kukata tamaa kwa wananchi baada ya kuona kipenzi chao JPM anazushiwa uongo na mema yake yanapondwa.

Wananchi imani yao kwa Magufuli ni kubwa sana, waite wajinga awajaelimika ila kuna namna JPM aligusa maisha yao na akatengeneza connection nao. Hakuna kitu mtafanya sasa hivi kufuta hii love ya raia kwa JPM.

Nawashauri CCM na wapinzani mnaoendeleza vita na JPM wasibeze hivi vilio maana awa wananchi watawaadhibu siku moja. Kumpuuza Magufuli ni kuwapuuza majority ya watanzania 93%.

Msije sema hamkuambiwa.
View attachment 1748149View attachment 1748150View attachment 1748151View attachment 1748152View attachment 1748153View attachment 1748154
Ndugu, wananchi umeelewa wanachokililia lakini? yawezekana ata hujasikia kilio cha wananchi. Ni mikumbo pengine lakini wapo wanaolia juu ya elimu bure(currently the only move done by the late kwenye elimu) Elimu bure was bogus attempt na sijui kwanini tumeruhusu elimu irudi nyuma kiasi kile. Mzee mkapa aliwahi kusema
"serikali za kiafrika zikiingia madarakani hudhani kila kilichofanywa na serikali zilizopita kuwa ovyo. Hakuna continuity kwenye utekelezaji"

Tulikuwa na sera nzuri sana kwenye elimu tangu nusu ya pili ya mheshimiwa mkapa na uasisi wa shule za kata wa mzee sumaye. Utekelezaji wake ulikuwa very successful Mpaka mwaka 2015 shule za sekondari zilifikia karibu 4000 Tanzania nzima 3000 more kuliko miaka 10 nyuma. Tuliongeza sana idadi ya wanafunzi mashuleni na kujongeza idadi ya walimu kwenye vituo.

Uhitaji wa walimu ni mkubwa leo kuliko uhitaji wa uhisani feki wa elimu bure ambayo in a real sense sio bure bado ni contributory kama ilivyokuwa mwanzo. Tatizo ni namna uongozi ulivyojaribu kuua kila kilichofanyika na watangulizi. Mbaya zaidi hilo lilifanywa uku likiaminisha wananchi kuwa huu unaofanyika ni msaada mkubwa sana na unafanywa na mtu aliyejitoa sana. Nimeongelea sana elimu maana nimeona namna inavyoteketea huku watu wakiaminishwa tofauti. Elimu ilifanywa siasa na hii imeitesa sana taaaluma.

Watanzania wengi hawana picha kamili juu ya ukuaji wa nchi. Wengi wanalia juu ya hearsays. watu wakifocus sana kwenye veracity ya rumours usahihi wake ni rahisi sana kupotea. Mfano watu waliaminishwa juu ya ukuaji wa uchumi na saga ya uchumi wa kati. very cheap political moves. Wanaolia wapo wanaosema kuwa tulienda uchumi wa kati and stuffs. Usahihi wa hili upo kwenye vitabu. Ukisoma DIRA 2025 utaona umuhimu wa uhuru wa kuihoji serikali. Tuna nguzo nne kwenye dira yetu ya maendeleo atleast all of them zimeguswa vibaya. Hakuna cha maendeleo ya watu, utawala bora wala ukuaji wa kiuchumi vilivyoachwa(ikiwa utakuwa mvivu kusoma tathmini za mpango wa 1 na 2 wa maendeleo tutajadili hili kwa kina)

Wapo wanaolia juu ya miradi. About 3000 kilometers za lami for 5 years. A good move lakini sio Godly move. wengi wa wanaolia wanaamini asilimia kubwa ya hizi barabara zimejengwa kipindi cha miaka 5 iliyopita. Binafsi nimesikia ata wabunge wakisema hili(labda ni zile zile cheap politics) nchi hii ina karibu kilometer elfu 13 (13,000 kms) za lami. shida ya miradi hii ni ugawaji wa tenda zake, uhalisia wa utekelezwaji wake, ushirikishwaji wa stakeholders na uhalisia wa gharama. Hili lilionywa na wengi sana humu kuwa transparency inahitajika kwenye utekelezwaji wa miradi ya kimkakati.

Dhana nzima ya utawala bora ilianza kupotea. Wapo walioamini zaidi kwenye kusikia kuliko kusikiliza. utaambiwa bunge live linafanya watu wasifanye kazi ila kila saa 1 TBC wako live wanazindua miradi.

Nchi haikupaswa kuongozwa kwa kulinda hadhi ya mtu juu namna anavyoonekana. Hata image yako ikiwa mbaya ila ukiwa na lakusema ipo mahali utalisema. Angesimama Hayati Benjamin Mkapa kukwambia juu ya sera alizofuma, transformations alizofanya, namna alivyopandisha uchumi kama ndoto ungelia sana.
 
Attachments

  • JamiiForums-1497101855.jpg
    JamiiForums-1497101855.jpg
    69.1 KB · Views: 1
Umeilingalisha vipi wakati kwa mujibu wa komenti kule juu huwa huitumii?

Hujui kuwa ukitoa thread au maoni ya upande fulani unashambuliwa kama nyuki?
Hasa jukwaa la siasa? Bora hata majukwaa mengine unaweza kujifunza kwasababu kule watu hawawi katika mlengo fulani..

Huku jukwaa la siasa unaweza kujua hata hii jf ipo na mlengo upi.

Jukwaa la Siasa Pro CHADEMA huwa wanaamini ni haki yao peke yao ku comment,ukija na mawazo tofauti utashambuliwa na kukejeliwa mpaka basi,nimecheka kwenye Thread ya Mwanakijiji kuna Pro-Chadema mmoja anamtukana kuwa hana akili na wala hajui system inavyofanya kazi akae kimya,nikamuuliza unamjua Mwanakijiji au unapuyanga tu,kashindwa kujibu kabaki kuniporomoshea matusi,halafu eti ndiyo wanajiona Great Thinker kuliko Users wa FB[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Niliisoma ile thread,alichowasilisha wachache sana walimuelewa.nilishangaa sana na majibu ya watu mle.

Muda mwingine mtu unaamua kukaa kimya tu unakuwa msomaji.
 
What if huwa wanafanya utani/comedy? Wewe una uhakika gani hao walikuwa serious na hicho walichokiandika,That’s alone doesn’t justify ur point kuwa ni Wajinga,come up with concrete reasons! Kama ni kuandika kwa kukosea hata wewe unakosea u’re not perfect either!
 
Sawa endeleeni na matusi yenu nyinyi si mnajua kuongea sana. Ila mjue wananchi sio wajinga wanamjua mbaya kwao na mzuri kwao. Magufuli kawafanyia mengi mazuri haya matusi ya kumuita fisadi yatawahukumu siku moja.
MATAGA mmepatwa na kiwewe.

Pambio mfululizo niaka 5 limewalemaza kabisa, mmekuwa vibudu. Jiwe aliwashika vibaya sana.

Mambo ya brainwashing na cult-following.

Niseme tu CORONA BABA LAO. Mtu kazikwa na mavi yake. Hehehehehe
 
Niliisoma ile thread,alichowasilisha wachache sana walimuelewa.nilishangaa sana na majibu ya watu mle.

Muda mwingine mtu unaamua kukaa kimya tu unakuwa msomaji.

Sasa hawa ndiyo wanajiona GT na kuwadharau users wa FB. Huo uzi ndiyo ulionyesha kiwango cha uelewa mdogo wa members wengi hasa Pro-Chadema,comments nyingine nilikiwa nasoma naishia kucheka hadi naangalia Profile ya aliyeandika.
 
MATAGA mmepatwa na kiwewe.

Pambio mfululizo niaka 5 limewalemaza kabisa, mmekuwa vibudu. Jiwe aliwashika vibaya sana.

Mambo ya brainwashing na cult-following.

Niseme tu CORONA BABA LAO. Mtu kazikwa na mavi yake. Hehehehehe

Naona hii Comment umeisave kwenye draft kabisa unakuwa unapaste tu unapojisikia[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Sasa hawa ndiyo wanajiona GT na kuwadharau users wa FB. Huo uzi ndiyo ulionyesha kiwango cha uelewa mdogo wa members wengi hasa Pro-Chadema,comments nyingine nilikiwa nasoma naishia kucheka hadi naangalia Profile ya aliyeandika.
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Povu kama lote,ukiguswa kidogo unashindwa kuhimili joto la mjadala, ujinga wa Multiple ID’s mnao nyinyi mliovamia JF na kuja kuifanya ikawa ya hovyo hovyo,JF ya enzi hadi tunaichangia isimame haikuwaga na ujinga kama huu!
Wewe ndo una povu had ukaanza personal attack, kuwa mvumilivu ndugu. Mwanaume mzima una I'd nyingi sijui ka Nini hafu siuende huko FB na IG unakoona Wana msifia mwendazake.mda wote tu jf ya sikuhizi si nzuri huku unaendelea ku comment na Wala hauachi.
 
Back
Top Bottom