Jinsi ulivyojibu hoja inaonesha wewe ni mtu wa namna gani. Usomi unataka hoja ijibiwe kwa hoja, kuuliza maswali ya kidadisi na kukubali kujifunza mambo mapya kila siku (Socratic Method of Learning). Kunishambulia mimi binafsi kwamba natumia ChatGpt kumenishangaza mno, hasa kwa mtu ambaye binafsi nilimuona msomi. Mimi nimesoma historia zamani kipindi ambacho hata hizi teknolojia hazikuwepo. Unaponiambia natumia ChatGpt ambayo hata sijui kuitumia, naona unanitukana tu. Binafsi siwezi kukurushia vijembe kwasababu naamini sifahamu kila kitu, mbali na kwamba nimesomea historia na falsafa za kale kwa muda mrefu tu. Ila nitakisema kile nachokifahamu, ukitaka kwenda kufanya utafiti itapendeza, ukiendelea kuamini kwamba unafahamu kila kitu, basi hewala pia. Turidi hojani:
Mosi, mbali na kuwepo vyanzo vya kihistoria ambavy vimegundulika miaka ya hivi karibuni, vyanzo vikubwa vya historia ya kale ni waandishi wa Kigiriki na Kilatini, mfano Herodotus, Strabo, Polybius, Xenophon na Josephus. Taarifa za msingi za dola la madola ya kiajemi ambazo hata wasomi wakubwa duniani wanazitegemea ziliandikwa na Herodotus kwenye kitabu chake cha The Histories. Unapoendelea kubishana na vyanzo ambavyo hata hao wasomi unaowataja wanavitumia unanipa ukakasi sana. Hizi hapa ni kurasa chache za kitabu cha Herodotus kinachozungumzia vita baina ya Uajemi na Ethiopia:
View attachment 2739581
Hapa anaendelea kuelezea jinsi waajemi walivyoshindwa vita dhidi ya Waethiopia:
View attachment 2739583
Pili, unavyozungumzia Archaeological Evidence kuleta uthibitisho wa dola la Umedi & Uajemi, hata mimi binafsi nakushangaa. Hakuna anayepinga uwepo wa dola la Umedi & Uajemi, miaka ya 5th BCE. Ambacho nakushangaa ni kitendo cha wewe kushindwa kukubali kwamba eneo ambalo madola ya Uajemi yamekuwepo ni barabara ya dunia (International Pathway) ambayo baadaye ilikuja kuwa The Silk-Road, iliyounganisha dunia (The Known World) kwa miaka zaidi ya 3000. Hata waajemi wenyewe kiasili ni watu waliohamia kutoka The Indus Valley baada ya kipindi cha Bronze Age kuanguka. Eneo lile liliunganisha dunia biashara ya dunia kutoka Ulaya, Afrika, Arabia na Mashariki ya Mbali.
Hata tunaposoma The Islamic Golden Age, kipindi ambacho The Abbasid Caliphate waliiletea dunia mapinduzi makubwa kwenye sayansi, teknolojia na falsafa, moja ya chanzo kikubwa ni uwepo wa dola hili kwenye sehemu ya barabara ya dunia. Wasomi wa kiislamu walijifunza mambo mengi kutoka Rumi, Uajemi na India ambayo wewe na mimi leo hii tunayasoma. Leo hii msomi yoyote akitoa hoja kwamba Marekani limekuwa taifa kubwa bila msaada wa kijiografia nitamshangaa mno. Kama umesoma vizuri historia, naamini utakuwa unafahamu kuhusu, The Bubonic Plague, tauni ambayo iliua mamilioni ya watu barani Asia na Ulaya.
Ugonjwa ule ulianzia Uchina lakini ulifika kwa haraka mno Ulaya kwasababu ya barabara ya kimataifa (International Pathway/ The Silk Road/Steppe Road) ambayo iliunganisha mabara zaidi ya matatu kibiashara. Huwezi kupinga Geography kwenye maendeleo ya taifa lolote lile kubwa, hence the word GEOPOLITICS. Msomi Tim Marshall kwenye kitabu chake maarufu kiitwacho, PRISONERS OF GEOGRAPHY: TEN MAPS THAT TELL YOU EVERYTHING YOU NEED TO KNOW ABOUT GLOBAL POLITICS, anasema hivi:
View attachment 2739634
Jiografia huathiri mno ustawi wa madola makubwa, kiufupi hata maendeleo ya sayansi na teknolojia hayaletwi na akili za watu peke yake, bali muingiliano wa kiutamaduni ambao hushawishiwa mno na jiografia. Mataifa ya Uajemi yemedumu kwa muda mrefu kwasababu jiografia iliwasaidia kukua kiutamaduni, kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia. Mbinu za kijeshi alizotumia Koreshi alijifunza kwa The Scythians, mbinu za mahesabu za kiajemi zilitokea India. Mbona haya yanafahamika vizuri tu.
Tatu, leo umenifanya nichangamke na kupitia madaftari yangu ya notsi ambazo niliziandika nikiwa chuoni nafanya tafiti kuhusu madola ya Kiajemi miaka mingi sana iliyopita. Binafsi hatukuwa na GOOGLE wala ChatGpt, ilikuwa ni kwenda maktaba kuinamisha mgongo mpaka usikuwa wa manane. Wengi wenu mngesoma kwenye mazingira ambayo tumesoma sisi, ya vitabu bila kompyuta mngetia akili. Zamani watu walikuwa hawafaulu wengi kwasababu hakukuwa na dezo, unajua historia, unajua historia, hujui historia unabaki kuwa mjinga mpaka mwisho. Hapa nilikuwa nachukua notsi kwenye mada iitwayo "Why Were the Iranian Empires So Successful" . Mwalimu wa kizungu alikuwa anasoma IMRA (Dictation) sisi tunaandaa notsi zetu fupi (Summary), hakuna ChatGpt wala GOOGLE Hebu angalia:
View attachment 2739637
View attachment 2739638
View attachment 2739641
View attachment 2739643
View attachment 2739648
Baada ya hapa, tulifundishwa kuhus CYRUS THE GREAT- RISE OF THE ACHAEMENID EMPIRE, na baadaye tukafanya mitihani kibao, pamoja na majadiliano. Hivyo naposema nakifahamu kitu wala sijisifii au kutaka mnione nafahamu, ila nasema ili tujifunze:
View attachment 2739657
Hii hapa PHILIP'S ATLAS OF WORLD HISTORY, nimeisomea miaka mingi nyuma nikiwa HIGH-SCHOOL mwaka wa mwisho, mpaka leo ninayo na nimewatunzia watoto wangu wanaendelea kuitumia. Kuna kipindi nilikuwa nimekariri karibia michoro yote na picha za hii Atlas.
View attachment 2739667View attachment 2739668
Mkuu Venus wewe ni watu ambao nawaheshimu sana humu ndani, japo sikufahamu. Uliposema mimi ni ChatGpt a.k.a Roboti, I was really flattered. Watu kunihisi mimi ni kompyuta au kikundi cha watu inaonesha kwamba I Have Mastered My Craft, All Praise To The Most High. Hakuna ChatGpt wala Google ni nidhamu ya kupenda kusoma na uzeoefu wa kazi yangu ambayo naipenda mno na nimeifanya kwa miaka mingi sana.