Kwanini Iran imezipita Ethiopia na Liberia?

Kwanini Iran imezipita Ethiopia na Liberia?

Muda wako mwingi ambao huna kazi unautumia kufanya nn
Sijawahi kuwa na muda wa aina hiyo mkuu! Mara nyingi nimelazimika kuahirisha mambo mengine kwa sababu ya kutokuwa na muda wa kuyafanya.

Labda, muda pekee ambao naweza nikasema nipo huru, ni kipindi nikiwa safarini. Nyakati kama hizo nazitumia kusoma vitabu. Nina kawaida ya kutembea na kitabu bila kujali kama ni safari ndefu au fupi.
 
Popote penye mtu mweusi ni matatizo, Haiti ni mfano halisi!
Naichukia hiyo kauli, lakini sina point zenye mashiko kuthibitisha uhalali wa pingamizi langu.

Nachukia sana. Natamani meza ipinduliwe ili habari zinazomhusu Mwafrika ziwe ni Habari chanya pekee.
 
Wapo wengi sana na kwa haraka tu watu weusi wamevumbua vitu au bidhaa 50,000 ndio elfu hamsini popote walipo wengi wakiwa watumwa au wafanyabiashara huko [emoji631]

Kuna alievumbua Traffic light na hata alievunbua refrigerator za malori ni mtu mweusi

Tumo kwenye historia ila tatizo la mtu mweusi anapovumbua kitu haendelezi kama mtu mweupe anakuwa na patent na kuwa na shirika endelevu na kurithishana kama wazungu.

Hapa ni baadhi ya bidhaa tulizovumbua weusi
Ukosoma zote utashangaa sana ila ndio hivyo tena

Wamevumbua na mzungu akaendeleza huko huko kwao ila sio UK wala Germany ni USA.

View attachment 2739183
Hata aliyetengeneza drones za kivita USA ni Mnaijeria, alipovumbua tu akapewa uraia wa USA jumla jumla.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna nchi ya Afrika iliyowahi kuwa huru.
Tuna uhuru wa bendera. Hawa viongozi wetu ni mawakala wa mabwana zao whites.
Ni km jela Nyapara anavyocontrol wafungwa ili kumsaidia Askari Magereza.
Aisee!
 
Ndugu Venus Star kasema mimi ni ChatGpt a.k.a robot, truth be told I'm flattered.....
Hapana! Huenda wewe ni Profesa wa Historia. Na sitashangaa nikiambiwa wamiliki wa ChatGp wanafanya kazi nawe kama mtaalam wa Historia.
 
Samahani sana ndugu yangu kwa kukukosea.

Naomba nikae nisome vizuri hii comment yako kisha niweke comment yangu vizuri.

Lakini wewe umeanza kuongelea karne 5 BCE. Mimi nimeongelea 4000BCE kumbuka miaka ilikuwa inasomeka kwa reduction before CE.

Vilevile hujaiomgelea kabisa Ethiopia kuiweka chungu kimoja na Iran.

Ngoja nimalizie kazi kisha niandike maelezo kwa undani.
Hongera! Inaonesha wewe ni msomi mwelewa na mstaarabu!

Mada imekuwa "debate" elimishi.
 
Haiti achana nao hao ni mizimu inayotembea
Yaani kila nyumba lazima ukute misanamu
Sokoni bidhaa nyingi na wauzaji wengi sana wanauza bidhaa za ushirikina tu hata magari yao yote wameweka voodoo
Wanaamini uchawi sana kuliko dini
Serikali yao inaamini katika uchawi?
 
Africa kusini makaburu bdo wako mkuu nchi inawazungu wakutosha ila na misri wale jamaa ni waarabu ila cjui walifikaje huku [emoji23][emoji23]
Kwa mantiki hiyo, unataka kusema tatizo ni mtu mweusi? Usijibu kwa sababu nahisi sitalipenda jibu utakalolitoa. Inafikirisha na kukasrisha.
 
Iran has people of jewish ancestry and that's why their IQ is higher compared to Africans.
Kama ndivyo, kwa nini na Ethiopia nayo isiifananie Iran japo kwa mbali? Inasemekana Waethiopia chimbuko lao ni Uyahudi!
 
Lakini nafikiri nchi nyingi za Kiafrika hazijaifikia Mexico kiuchumi.
75% uchumi wa Mexico umetokana na biashara haramu (madawa ya kulevya) si kwenye inshu za technology, elimu, diplomacy, maendeleo ya uchumi halali sawa na Mataifa mengine ya kihistoria kama Greek, Uajemi, Italy n.k.

Magwiji wa biashara hiyo wengi wao wamekuwa wakisumbua sana duniani kukwepana na hukumu za mahakama na magereza ya kimataifa.
Screenshot_2023-09-06-14-32-05-63_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
Screenshot_2023-09-06-14-32-14-95_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg


Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kutiana moyo katika vitu vya kipuuzi ni kurudishana nyuma. Anatakiwa kuchekwa.
Naamini asilimia ishirini ya Watanzania wangefanya alau "vitu vya kipuuzi" kama Masoud Kipanya nchi ingeongeza kasi ya kupiga hatua kimaendeleo.

Usimbeze Kipanya mkuu, alikofika inaweza ikawa ni hatua moja kuelekea kwenye ugunduzi mkubwa utakaoacha wengi vinywa wazi kwa mshangao mzuri.
 
Back
Top Bottom