Kwanini jamii za kiAsia zinaonekana kufanya vyema kwenye akili mnemba( AI) na Semiconductors

Kwanini jamii za kiAsia zinaonekana kufanya vyema kwenye akili mnemba( AI) na Semiconductors

Kwa nini hizi jamii za Asia zinaonekana kufanya vyema kwenye AI kwa sasa duniani ? Hasa jamii ya kichina iwe ndani ya nchi zao za kuzaliwa au hata nje ya nchi zao

Nini siri ya mafanikio yao au upande gani una mafanikio kwao katika maeneo haya ?
Mzee miez kama mitatu nyuma nilikuwa Beijing. Hilo jimbo limeweka sheria akili mnemba inafundishwq tangu darasa la kwanza
 
Unadhani kwanini iko ivyo!!?
Labda akili ya Mwafrika haijushughulishi sana kuwaza, kukariri na kuelewa mambo magumu kwa sababu mazingira yanayomzunguka ni mepesi ukilinganisha na jamii nyingine nyingi( "Necessity is the mother of invention") , Waarabu nafikiri tatizo lao kubwa lilikuja kuwa kwenye kuipa dini kipaumbele zaidi kuliko ilm dunia ndipo ikawa mwisho wa golden age of Islam, wahusika wakuu walikuwa ni Muhammad bin Abd al Wahhab na watu wa aina yake.
 
Hili linaweza kuwa ndio jibu sahihi la huu uzi, maana hata kwenye mashindano ya International Olympiad In Informatics, wachina na wakorea ndio huwa wanaibuka washindi kisha ndio wanafuatia wamarekani.
Hata hao wamarekani ni wamarekani wenye asili ya Asia huunda team
 
Wewe ndo hujui Tofauti ya AI na semiconductor.

1. Semiconductor kwa ujumla ni hardware
2. AI ni software

UAE na Saudi AI inafanywa na local companies hardware ndio inatoka Usa.

Dunia nzima mwenye hardware competitive ya AI ni Usa na China pekee.
Wewe ndio huelewei chochote, hakuna AI ya maana inafanyika bila semiconductors/Chips. Ni ujinga zaidi kufikiri AI ni software tu.
 
Mzee miez kama mitatu nyuma nilikuwa Beijing. Hilo jimbo limeweka sheria akili mnemba inafundishwq tangu darasa la kwanza
Nzuri hii ingewezekana nasi tungefanya kama tungekuwa na uchumi mzuri na siasa nzuri
 
Marekani kuna cheap labour?
Cheap labour ipo kwa standards zao huko Marekani hasa kwenye entry level jobs. Mtaalumu anayeenda Marekani kutoka India, China, Iran, Pakistan n.k hata akilipiwa nusu ya pesa ambayo angelipwa Mmarekani kwa kazi hiyo hiyo atachekelea sana na kukenua nje meno yote 32.
 
Wewe ndio huelewei chochote, hakuna AI ya maana inafanyika bila semiconductors/Chips. Ni ujinga zaidi kufikiri AI ni software tu.
Kwa logic hii basi uzi ufungwe, maana dominant hardware ya AI ni Nvidia na to some Extent mchina, Hao Korea, Japan, Wahindi na wengineo hawana hizo Hardware so nao hawana issue Yoyote.
 
Usijali Africa tuna vyuo vyetu na watu smart kabisa.
Nitakuletea kitabu cha

HIRIZI EDITION plus
Jifunze Teknolojia ya AI kutoka Gamboshi

 Nawasilisha
 
Mbona hata jamii za wazungu, Warusi, WaIran, WaIsrael, Waturuki n.k zinafanya vizuri pia kwenye AI??
Jamii kubwa ambazo hazifanyia vizuri kwenye AI katika maeneo yao ni Waafrika na Waarabu.
Huyo ni pro china ni kichaa kbs huyo lengo ni kutaka kumpa credit mchina mwizi wa tech za watu wa mfatilie post zake humu
 
Upo sahihi sijasema ni kumejaa watu wa Asia tu hapana nazungumzia uwingi wa watu wa Asia ni wengi katika maeneo hayo.

Fuatilia makampuni ya akili mnemba duniani utakuta wachina wakutosha na wahindi wazungu wapo lakini sio kwa kiwango cha watu wa Asia
Cheap labour
Hata marekani ana kiwanda cha apple China sababu gharama za uzalishaji huko ni cheap sn hasa wafanyakaz wanalipwa kidogo sn kuliko wa huko America na Europe
 
Kwa nini hizi jamii za Asia zinaonekana kufanya vyema kwenye AI kwa sasa duniani ? Hasa jamii ya kichina iwe ndani ya nchi zao za kuzaliwa au hata nje ya nchi zao

Nini siri ya mafanikio yao au upande gani una mafanikio kwao katika maeneo haya ?
wao hawana upuuzi wa no reforms no elections
 
Kwa logic hii basi uzi ufungwe, maana dominant hardware ya AI ni Nvidia na to some Extent mchina, Hao Korea, Japan, Wahindi na wengineo hawana hizo Hardware so nao hawana issue Yoyote.
Uzi hauwezi kufungwa kwa mawazo yako duni na mepesi ya kushindwa kujua hakuna AI bila hardware. NVIDIA kuwa dominant wa semiconductor/chips za AI haimaanishi wengine hawazilishi hizo hardware. Samsung, STMicroelectronics, ASML,Renesas, ROHM na wengine wengi tu wanazalisha semiconductors, ishu ni ubora na ukubwa wa uzalishaji. Makampuni mengine yanazalisha semiconductor kuuza kama biashara yao kuu, mengine yanazalisha semiconductors kwa ajili ya matumizi kuweka kenye bidhaa zao kuu kama drones, simu, computer n.k na ikibidi wanaongezea kwa kununua kutoka nje. Ustadh hii mada inahitaji elimu dunia kiasi na exposure, tulia ujifunze.
 
Sasa kama Bundle lenyewe halishikiki na watu mnapeana Imani za Kusadikika (Mipango ya Mungu) unadhani mtaweza kufanikisha kwa lolote....; Bongo hata Wasanii wamejitahidi kwenye Usanii na kutoa nyimbo ingawa no thanks to Serikali kwa kufanya Bundle bei mbaya hivyo wadau kushindwa kucheki kazi zao (Hata mtu akiwa na kiji TV chake Youtube Serikali inataka walipe)


Kwa kukujibu Asians hard working na kuna incentives na nyezo za kuweza kufanya mambo; wakati western ni madogo wengi wazembe na wamebweteka huku bongo ni Serikali ndio haiweki mazingira bora ya kukuza ubongo wa Madogo katika their Thinking....
 
Miaka ya 1980 mpaka 2000's nchi nyingi za Asia kama China, Taiwan na Korea zilipeleka kwa wingi sana raia wake US na Ulaya wakasome masome ya teknolojia ikiwemo computer na IT, pia wamefanya udukuzi mkubwa sana wa teknolojia kupitia idara zao za kijasusi. Hii yote ni mikakati yao serikali zao pia waliyotumia kuwafikia wazungu kiteknolojia.
Aliyeanzisha TSMC ya Taiwan alisoma Havard, MIT na Stanford Universities.
Mwanzilishi wa SMIC pia amesoma na kufanya kazi Marekani
Xi Jinping
"50% of world’s best AI researchers are Chinese and many of those work at U.S.-based AI labs."
-Nvidia CEO Jensen Huang​
 
Back
Top Bottom