Kwanini JWTZ imeanza kutumia Salamu za Chama cha Mapinduzi (KAZI NA UTU)?

Kwanini JWTZ imeanza kutumia Salamu za Chama cha Mapinduzi (KAZI NA UTU)?

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania nini kimewasibu?

Wanatumia salaam za Chama cha Mapinduzi za Kazi na Utu. Halafu wanalazimisha baadhi ya vyombo vya habari vikate hicho kipande cha Salaam za CCM. Nimeshangaa sana.

Screenshot_20260704_143316_Threads.jpg

Pili Maandamano wanaita Vurugu. Je, wanalinda katiba ya Nchi gani? Katiba ya Tanzania inatambua Maandamano, Ila Walinda Katiba wanadai ni Vurugu na Fujo.

Watu wanataka maandamano 7/7/2026, eti wanatoka na kusema maandamano ni Vurugu. Wapi katiba imesema maandamano ni Vurugu?

Nne na Mbaya zaidi eti Jeshi linawaomba Wananchi kutoa taarifa kwa viongozi wa Vijiji/Mitaa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu uchochezi au viashiria vya uvunjifu wa amani. Nimeshangaa sana.
Screenshot_20260704_141343_Instagram.jpg

Kwanini kazi ya Polisi inataka kufanywa na Jeshi la Wananchi?

TUJIKUMBUSHE MAJUKUMU YA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA.​

  1. Kulinda Katiba na uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  2. Kulinda mipaka ya nchi dhidi ya uvamizi au vitisho kutoka nje.
  3. Kufanya mafunzo na mazoezi ya kijeshi ili kuwa tayari wakati wote kukabiliana na tishio lolote.
  4. Kuelimisha umma kuhusu ulinzi wa taifa, ikiwemo kukuza uzalendo na uelewa wa masuala ya ulinzi.
  5. Kushirikiana na mamlaka za kiraia katika uokoaji na utoaji wa misaada wakati wa maafa kama mafuriko, moto, matetemeko ya ardhi na dharura nyingine.
  6. Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Taifa.
  7. Kushiriki katika operesheni za kulinda amani kimataifa, chini ya United Nations au mashirika ya kikanda pale Tanzania inapochangia vikosi vya ulinzi wa amani.
 
Siku za nyuma jeshi lilikuwa ni sehemu ya CCM, kwani liliishajitenga na chama hicho?

Wanajeshi walijumuika siasani mpaka wengine walikuwa wanagombea ubunge.

Jeshi lilikuwa ni tawi la CCM, si ajabu jeshi likilinda chama chao cha CCM kisiondolewe madarakani na wao wapo itakuwa ni aibu!
 
Ili mambo yasiwe mengi ni bora kibaki chama kimoja tu cha ccm, hivi vya upinzani vifutwe vyote ijulikane ni nchi ya chama kimoja.

Ya nini kuzuga wazungu wafadhili na wahisani kwamba nchi ni ya vyama vingi wakati wananchi hawaoni siasa ya vyama vingi ikifanya kazi yake kidemokrasia?

Jeshi la wananchi halipaswi kujionesha ni la chama fulani, lenyewe linatakiwa kuwa neutral kwenye mambo ya vyama vya siasa.

Kama linafanya mapinduzi kumuondoa mtawala wa kiraia muovu hapo sawa, litakuwa linalinda maslahi ya taifa na kisha kuacha utawala wa kiraia uchukue hatamu tena, yaani kazi yake ni kulinda nchi
 
Hakujawahi kuwa na jeshi la Wananchi toka wakati wa Nyerere mpaka sasa bali ni jeshi la CCM.

Wakati wa Mwalimu walikuwa wakisema zidumu fikra za Mwenyekiti kama hufahamu historia ya hilo jeshi lenu na uhusiano wake na CCM na siasa za Tanzania basi utashangaa hiyo kauli ya kazi na utu.

Kwangu sio kauli mpya bali ni kitu cha kawaida tu jeshi la CCM kukilinda chama chake kwa vikauli uchwara kama hivyo toka enzi za Mtakatifu wenu Nyerere.
 
Kazi na utu ni salamu aliyoianzisha rais wa nchi akiwa kwenye tukio la kiserikali
 
Bila shaka zitakuwa salamu za saba saba!
 
Hatuna Jeshi hapa. Hiki ni kikundi cha kulinda maslahi ya watawala pekee. Tanganyika we are fvckd off!
 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania nini kimewasibu?

Wanatumia salaam za Chama cha Mapinduzi za Kazi na Utu. Halafu wanalazimisha baadhi ya vyombo vya habari vikate hicho kipande cha Salaam za CCM. Nimeshangaa sana.
View attachment 3622352
View attachment 3622356
Pili Maandamano wanaita Vurugu. Je, wanalinda katiba ya Nchi gani? Katiba ya Tanzania inatambua Maandamano, Ila Walinda Katiba wanadai ni Vurugu na Fujo.

Watu wanataka maandamano 7/7/2026, eti wanatoka na kusema maandamano ni Vurugu. Wapi katiba imesema maandamano ni Vurugu?

Nne na Mbaya zaidi eti Jeshi linawaomba Wananchi kutoa taarifa kwa viongozi wa Vijiji/Mitaa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu uchochezi au viashiria vya uvunjifu wa amani. Nimeshangaa sana.
View attachment 3622357
Kwanini kazi ya Polisi inataka kufanywa na Jeshi la Wananchi?

TUJIKUMBUSHE MAJUKUMU YA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA.​

  1. Kulinda Katiba na uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  2. Kulinda mipaka ya nchi dhidi ya uvamizi au vitisho kutoka nje.
  3. Kufanya mafunzo na mazoezi ya kijeshi ili kuwa tayari wakati wote kukabiliana na tishio lolote.
  4. Kuelimisha umma kuhusu ulinzi wa taifa, ikiwemo kukuza uzalendo na uelewa wa masuala ya ulinzi.
  5. Kushirikiana na mamlaka za kiraia katika uokoaji na utoaji wa misaada wakati wa maafa kama mafuriko, moto, matetemeko ya ardhi na dharura nyingine.
  6. Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Taifa.
  7. Kushiriki katika operesheni za kulinda amani kimataifa, chini ya United Nations au mashirika ya kikanda pale Tanzania inapochangia vikosi vya ulinzi wa amani.
Samia anahakikisha anavuruga kila kitu,yaani hili jeshi limeshafikia level za FARDC la DRC,jeshi limeingiliwa na incompetency ya hali ya juu sana,yaani rushwa nje nje,hapa tulipofikia operesheni watakayoiweza ni kupambana na raia wasiokuwa na silaha,ila hawataweza kupambana na hata jeshi la burundi,M23 ndo wanaweza kuja mpaka uvunguni oale magogoni bila upinzani wowote
 
Back
Top Bottom