Kwanini Kanisa Katoliki linahamasisha umaskini na halitaki kabisa watu waponywe na maradhi? Au wanafaidika nao

Wana hofu ya kukimbiwa na waumini wao wanaokwenda kwa mwamposa kupata uponyaji. Kingine hawana mafundisho ya kutosha kuwajenga waumini wao kiroho ile tunaita malisho ya majani mabichi.
 
Wana hofu ya kukimbiwa na waumini wao wanaokwenda kwa mwamposa kupata uponyaji. Kingine hawana mafundisho ya kutosha kuwajenga waumini wao kiroho ile tunaita malisho ya majani mabichi.
 
Your browser is not able to display this video.

hapo vipi πŸ‘†πŸ‘†πŸ‘†
 
Siku ukija kuujua ukweli .. utaachana hizi mishe za dini
 


Na wewe akili huna, kuombewa kunatoa umaskini au Ufukara? Nyie watu, hivyo vichwa vimejaa matope tupu..!!
 
Kwa sababu hao hao wachungaji utajiri wao ni sadaka za hao wanaodai wanawaombea wafanikiwe kifedha wao wenyewe mbona hawajiombei wakafanikiwa ila wakiwa na shida waumini utasikia, sadaka ya kumjengea mchungaji, sadaka ya kununua gari, sadaka sijui ya nini. So, huo ni utapeli mafanikio ni kuchapa kazi na hao mapadri na maaskofu wa kanisa katoliki nao wanachangiwa pesa hawajawahi kuwambia waumini pesa inapatikana kwa kuombea.
Chapa kazi pesa inakuja.
 
Kanisa halipigi vita wachungaji (genuine) wenye karama ya uponyaji na wanaofanya hivyo kama sehemu ya huduma za makanisa yao. Kanisa Katoliki linapiga vita wachungaji wanaoombea kisanii/wachumia tumbo/wanaowahadaa waumini wao na watu wengine kwamba wanafufua wafu, wanawaombea watu kuwa matajiri etc. Kuna baadhi ya Wakatoliki pia wanaokwenda kwenye hayo makanisa na kudhani matatizo yao yataisha. Wameenda, wameliwa fedha na hawakuponywa, kisha wakarudi na polepole wamegundua kwamba wametapeliwa kutokana na shida walizokuwa nazo. Hili ndilo tatizo. Hata Mimi naamini kama Mungu anaweza kuwasikiliza hao wachungaji, kwa nini nikimwomba mimi asinisikilize? Hivyo, Kanisa Katoliki linawa'alert' waumini wao na hata waumini wengine waangalie wasije wakatapeliwa kama wenzao walivyotapeliwa. Kama huo uponyaji ni wa kweli, kwa nini Tanzania bado watu wengi wanahangaika na matatizo ya kila aina na hawajasaidiwa kama ni rahisi hivyo?
 
Nani kawapa mandate katoliki kihariri makasa wakati masanamu yao sisi hatuyasemi.
 
Mtumishi acha ubishi. Haya nenda kachukue utajiri kwa Mwaposa.
 
Una akili kisha wakati wa Misa unabusu sanamu ilichongwa Mwenge vinyago na mmakonde mnywa Smart gin
 
So the suggestion is for the Catholic Churches to open ' healing clinics' like Mwamposa with a tariff of charges for each patient posted on the walls?
 
hapo vipi πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Kanisa Katoliki limekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya afya nchini Tanzania kupitia hospitali zao ambazo zinatoa huduma za afya kwa jamii. Baadhi ya hospitali zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki Tanzania ni pamoja na:

Hospitali ya Rufaa ya Bugando - Mwanza

Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari - Dodoma

Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Elizabeth - Shinyanga

Hospitali ya Mtakatifu Therese wa Mtoto Yesu - Songea

Hospitali ya Mtakatifu Francis - Ifakara

Peramiho mission Hospital
Ruvuma

Ndanda mission Hospital
Mtwara

Hizi ni baadhi tu ya hospitali za Kanisa Katoliki ambazo zinatoa huduma za afya nchini Tanzania, na zimekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha afya ya jamii.
Bado kuna Zahanati,vituo vya afya na taasisi nyingi zinazoshughulika na huduma za afya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…