Kwanini Kanisa Katoliki linahamasisha umaskini na halitaki kabisa watu waponywe na maradhi? Au wanafaidika nao

Shida ni kwamba kanisa katiliki linasisitiza umaskini kama ambavyo jpm alisisitiza watu kuwa wanyonge.
Siyo kweli, wao wanasisitiza utajili kwa kufanya kazi. Huo ujinga wa I receive haunaga nafasi huko..!!

By the way, tushazowea kusemwa, kutukanwa na wengi wasio wakatoliki. Tunachokifanya sisi tunakusikiliza, ukimaliza tunaenda kanisani kwetu kusali halafu baada ya kusali tunakwenda kwenye kitimoto, halafu tunarudi home. We tukana, kejeli, etc wala hatutakufuata na mitutu wala mapanga.

HANGAIKENI NA MABORITI YENU, MTUACHE NA VIBANZI VYETU..!!
 
Ukisikiliza mahubili ya maaskofu wa kanisa katoliki au mapadre, wanapiga vita sana wachungaji wanaowaombea watu kufanikiw kifedha au maisha kiujumla. Kwa sasa maaskofu wote wa katoliki wamemlia kolabo mwamposa. Mahubili yote ni yeye.

Wanaponda sana kwamba kwa nini anawaombea watu wafanikiwe. Na watu wanazidi kumiminika sana kwake which means wanaponywa na wanafaidika.

Ushauri wangu kwa maaskofu au mapadre, hubirini injili ya kweli na watu watawafuata msitumie nguvu mtaaibika
Maombi ya mafanikio siyo lazima kwenda kwa mitume na manabii (wa siku hizi wengi ni wa uongo na matapeli) au makanisani na nyumba nyingine za ibada.
Tunatakiwa kuunganisha utu wetu wa ndani pia dhamiri zetu na Mungu kwa Imani kwamba yeye ndiye Muweza wa yote.
Ujinga umesababisha watu washindwe kutofautisha Mungu wa kweli na sanamu za kutengeneza.
Mungu ametuwekea kanuni za asili ambazo lazima tuzifuate kwa kutumia akili alizotupa ili tupate mafanikio.
Hakuna njia ya mkatomkato katika haki.
 
Siyo kweli, wao wanasisitiza utajili kwa kufanya kazi. Huo ujinga wa I receive haunaga nafasi huko..!!

By the way, tushazowea kusemwa, kutukanwa na wengi wasio wakatoliki. Tunachokifanya sisi tunakusikiliza, ukimaliza tunaenda kanisani kwetu kusali halafu baada ya kusali tunakwenda kwenye kitimoto, halafu tunarudi home. We tukana, kejeli, etc wala hatutakufuata na mitutu wala mapanga.

HANGAIKENI NA MABORITI YENU, MTUACHE NA VIBANZI VYETU..!!
Sema.kwamba baada ya kusali mnaenda kulewa smart gin na kongagi
 
Ukisikiliza mahubili ya maaskofu wa kanisa katoliki au mapadre, wanapiga vita sana wachungaji wanaowaombea watu kufanikiw kifedha au maisha kiujumla. Kwa sasa maaskofu wote wa katoliki wamemlia kolabo mwamposa. Mahubili yote ni yeye.

Wanaponda sana kwamba kwa nini anawaombea watu wafanikiwe. Na watu wanazidi kumiminika sana kwake which means wanaponywa na wanafaidika.

Ushauri wangu kwa maaskofu au mapadre, hubirini injili ya kweli na watu watawafuata msitumie nguvu mtaaibika
Yesu alishinda jaribio la shetani la ahadi ya utajiri. Wala Yesu hakuja kuhubiri habari za utajiri wa dunia hii bali habari za Ufalme wa Mungu. Alisisitiza tuuze tulivyo navyo na kuwapa maskini na kisha tumfuate. Hao manabii wanaohubiri Utajiri ni wafuasi wa shetani maana kuna uhusiano mkubwa sana kati ya Shetani na Utajiri wa dunia hii.

Enyi wana wa Eva, zichunguzeni sana hizo roho zinazohubiri utajiri wa dunia hii na kuwauuzia mafuta ya upako msije mkanaswa pamoja nao katika mtego wa kwenda jehanamu ya moto kwa kuiabudi kitu msichokijua. Kumbekeni si kila asema bwana bwana na kutoa mapepo kwa jina la Yesu basi ni wa Yesu. Wengine mawakala wake na Ibilisi, lile koja kuu na mtawala wa Ulimwengu huu.
 
Jumapili iliyopota mapadre na maaskofu wote walimhuniri mwamposa tu.
Sio kweli. Huku kwetu umasaini ndani ndani huku Jumapili ya 11 Mwaka B tar. 16 June 2024 padre alihubiri kuhusu Ufalme wa Mungu uko wapi? Au ww unadhani Jf inasomwa hapo Dar pekee? Huyo Mwamposa inakuwaje? Mbona sisi huku hatujawahi kumuona?
 
Ukichunguza kwa makini viongozi wa kikatoliki ni wanyonyaji wakubwa, angalia wanavyotumia jumuiya ndogo katika kukamua watu bila huruma.
Huo ni uzushi. Una nia ovu ya kufitinisha waumini na viongozi wao. Hebu katafute pesa achana na Fitina mkuu.
 
Ukisikiliza mahubili ya maaskofu wa kanisa katoliki au mapadre, wanapiga vita sana wachungaji wanaowaombea watu kufanikiw kifedha au maisha kiujumla. Kwa sasa maaskofu wote wa katoliki wamemlia kolabo mwamposa. Mahubili yote ni yeye.

Wanaponda sana kwamba kwa nini anawaombea watu wafanikiwe. Na watu wanazidi kumiminika sana kwake which means wanaponywa na wanafaidika.

Ushauri wangu kwa maaskofu au mapadre, hubirini injili ya kweli na watu watawafuata msitumie nguvu mtaaibika
Unapigwa hela wewe stuka. Injili ni habar njema iletayo wokovu. Na tena tumetumwa kutangaza habar njem za ufalme w Mungu sio kununua maji sio nn
 
Shida ni kwamba kanisa katiliki linasisitiza umaskini kama ambavyo jpm alisisitiza watu kuwa wanyonge.
Lingekuwa linasisitiza umaskini,waumini wasingekuwa wanaomba kwa masaa mawili tu kwa juma ili wapate muda wa kufanya kazi,vp nyinyi mnaobudu karibia kila siku tena kuanzia alfajili mpaka jioni, kama sio kuwatia watu umaskini ni nini?
Toka ulivyoanza kuomba upokee,majumba,magari na utajiri huku ukipeleka visenti vyako madhabahuni umeambulia nn mpaka sasa,sanasana mnatajirisha matapeli kwa upumbavu wenu.
Magufuli hakuwa muumini wa umaskini,ndiomana kila mara aliwaambia watanzania kuwa Taifa lao ni tajiri,si ajabu mpaka wakapatikana akina Laizer ambao sijui kama atakuja kutokea mwingine sababu laslimali zinaishia kutajirisha wageni huku wazawa wakibaki taabani,kalagabaho😎
 
Kafanye utafiti wa maneno yako kanisa katoliki alijawahi kuwa na wasiwasi wa waumini wake kuondoka tangu kuanzishwa na ndiyomaana makanisa mengi yamemeguka kutoka kwalo na bado ndo kanisa linaloongoza kwakuwa na waumini wengi duniani. Africa tumedanganywa sana tunadhani kuombewa au kuomba kunaondoa umaskini! Kwa namna hii atuwezi kuendelea. Kazi ndiyo msingi mkuu wa utajiri na kuondoa umaskini na sio maombezi. Ikiwa unadhani vinginevyo basi utilize kwanini kwenye makanisa hayo sadaka tena za mafungu na zaka zingelikuwa azitolewi kwenye makanisa bali wangeliomba tu na wangelishushiwa kila kitu.
 
Umesema sahihi kabisa. Hawa watu sijui ni kwa nini wanashindwa au hawataki kwa makusudi kuukubali ukweli kwamba hata Yesu mwenyewe alifanya kazi tokea akiwa mtoto hadi utu uzima. Si Ingekuwa rahisi kwake kuomba? Yani ni ujinga sana kwamba Kiongozi wako anafanya kazi halafu wewe mfuasi unataka eti ulale hufanyi kazi unashindia maombi. :KEKBye:
 
Back
Top Bottom