Kwanini kelele za "Linda Mgongo" wanapigiwa wa kiume tu? Kwani mabinti wako salama?

Kwanini kelele za "Linda Mgongo" wanapigiwa wa kiume tu? Kwani mabinti wako salama?

Na hapa ndio utaona unafiki wa wabongo. Huwa nashangaa bongo fleva 90% zinahamasisha kumla mwanamke jicho.

Sasa hawaoni mtu akizoea huo mchezo kwa wanawake iko siku atajaribu kwa wanaume wenzake!!

Kama issue ni linda mgongo iwe kwa jinsia zote.
Hii kampeni si kampeni dhidi ya ushoga.

Ingekuwa kampeni dhidi ya ushoga ingewahusisha ma basha na ma lesbian.

Ni kampeni ya mfumodume.

Iko hivi, katika mfumodume, mtu anayeukataa uanaume kwa makusudi anaandamwa sana.

Kwa sababu inaonekana amejaliwa tunu kuu kuliko zote, ya kuwa mwanamme, halafu kaikataa.

Ndiyo maana mtu shoga anayefirwa anaandamwa kuliko wote.

Hata mabasha hawaandamwi sana, kwa sababu kwa kiasi fulani wanaonekana wao uanaume wao bado upo, ndiyo maana wanafanya, hawafanywi.

Ndiyo maana unakuta lesbians, ambao kimsingi ni mashoga pia, hawasakamwi sana, wanaonekana hawa ni wanawake wanacheza tu, wakipata mwanamme rijali wataacha.

Na kampeni hii imejikita katika saikolojia kwa kina mpaka wanaoifanya pengine hawajui vizuri kuwa wanaifanya.

Mpaka wanawake wanafanya kampeni ya mfumodume ya kuufanya uanaume kuwa ndiyo tuzo kubwa sana.

Ndiyo maana mwanamme anayefanywa anatukanwa sana, lakini mwanamke anayewafanya wanawake wenzake, stud, husikii kutukanwa sana, labda kama kachukua mwanamke wa mwanamme fulani tu.

Kwa hivyo, katika mfumo huu ambao hauchukii mtu kufirwa ila unachukia mwanamme kufirwa, mwanamke kufirwa inaonekana sawa tu.

Ndiyo maana mpaka kwenye nyimbo zinazopendwa sana za Bongofleva wanaongelea mwanamke kufirwa, lakini hakuna backlash.

Inaonekana ni kawaida tu.

Hii ni kampeni ya mfumodume, hata neno lenyewe shoga maana yake ni rafiki wa kike, mwanamme kuitwa shoga maana yake kaondoa uanaume wake, sasa hujaona kuwa hata neno lenyewe tu halijamgusa lesbian wala basha hapo?

Hii ni kampeni ya mfumodume.
 
Anzisha kampeni ya kupinga ufiraji wa wanawake, hakuna mwenye hati miliki ya kuanzisha hizo kampeni.
Suala si kuanzisha kampeni, suala ni logical consiatency.

Kutafuta jibu, kampeni hii maana yake nini hasa?

Bila ya logical consistency unaweza kuambiwa hii ni kampeni dhidi ya ushoga, ukadanganywa na kamoeni kama siasa za uchaguzi, wakati kwa kweli hii si kamoeni dhidi ya ushoga, ni kampeni ya kuwapaisha wanaume na kuwadogosha wanawake tu.

Kwamba mwanamme akifirwa dunia itaanguka, lakini mwanamke kufirwa ni kazi yake tu, hamna cha ajabu.

Ndiyo ujumbe wa kampeni hii.
 
Kwa hivyo, katika mfumo huu ambao hauchukii mtu kufirwa ila unavhukia mwanamme kufirwa, mwanamke kufirwa inaonekana sawa tu.
Nimekuelewa kwa muktadha wako. Ila specially kwenye hii para huoni kampeni haiwezi fanikiwa sababu ime focus kwenye supply side imesahau demand side?

Yaani unawaambia watu wasitumie bangi ila wanaouza bangi huwagusi?
 
IMG-20260926-WA0155.jpg
 
Ndugu siwez zaa mtoto wa kiume narudia kiume halafu aingiliwe kama mwanamke

Inaumiza Zaid ya uchungu wa leba
Unamuona huyu?

Huyu ndiye anaelezea vizuri ninachoandika hapo juu.

Kwake huyu, mwanamke kuingiliwa hivyo ni sawa tu.

Lakini mwanamme kuingiliwa hivyo ni uchungu zaidi ya uchungu wa leba.

Exactly my point of contention.
 
Mkuu Mimi sijakuelewa vizuri, paragraph ya pili umekubali kabisa kuwa kama watoto wa kike wanafanya kinyume basi na watoto wa kiume nao pia wafanyiwe kinyume...hayo maneno yako mkuu hayajakaa sawa, Kwa mtazamo wangu!
 
Wakuu, inakuwaje!Kuna swali moja la kijamii linalonikosesha amani sana mtaani kwa sasa na nimeona tulilete hapa jukwaani tulichambue kiume: Kwanini nguvu zote, kampeni, na kelele za "linda mgongo wako" zimehamia kwa watoto wa kiume tu? Kwani mgongo wa mtoto wa kike haupigiwi kelele ulindwe? Kwani mabinti wamekuwa salama ghafla au wamesahaulika kwenye hili jinamizi linaloendelea nchini?

Kwa mtazamo wangu kama migongo ya watoto wa kike tunaona sawa sioni shida wa kiume pia kutumika yao

You better watch your back
Mwaka jana nilisoma kitabu cha mwandishi aliyetoa kitabu cha Magufuli, nafikiri anaitwa Kabendera. Ameongelea tatizo la ushoga kwenye siasa za CCM. Akasema viongozi wakubwa serikalini wananunua vijana wadogo ili kuwatumia kung'arisha nyota zao za kisiasa. Juzi niliona mtu X anasema hivi sasa kuna mashoga wengi kwenye baraza mawaziri kuliko kipindi kingine cha historia ya Tanzania. Watanzania ambao ni wajinga wakisikia kuwa ukimlawiti kijana mdogo unatajirika na wao wanafanya hivyo. Mlawiti ni kibaka kama wezi. Hii kampeni tuiunge mkono.
 
Nimekuelewa kwa muktadha wako. Ila specially kwenye hii para huoni kampeni haiwezi fanikiwa sababu ime focus kwenye supply side imesahau demand side?

Yaani unawaambia watu wasitumie bangi ila wanaouza bangi huwagusi?
Kampeni haiwezi kufanikiwa kwa sababu wabongo hawajui wanataka nini.

Watu hawajui wanapinga nini, wanapinga ufiraji au wanapinga wanaume kufirwa?

Kama wanapinga ufiraji mbona kufira wanawake wenye matako makubwa ni kama fashion mpaka kwenye Bongofleva wanaimba?

Hata elimu yao kuhusu haya mambo ni ndogo, wakisikia ushoga wanachojua wao ni kufirana tu.

Wakati kuna mashoga asexual. Kuna bisexual, kuna lesbians. Kuna mambo mengi sana kwenye hili suala.

Hata lugha ya kujadili haya mambo hawana.

Ukiuliza shoga ni nani tu ni mjadala.

Je, shoga ni msenge tu? Au hata basha ni shoga? Wale lesbians nao ni mashoga?

Watu waume wanaoji present kike lakini hawafirwi, nao ni mashoga?

Wale ma crossdressers kina Chuche ambao hawafirwi, nao ni mashoga?

Tunaposema mashoga tunamaanisha nini?

Wabongo wengi hawajui, wamerukia tu hoja.
 
Kibongobongo mabinti hiyo ni kazi yao.

Tatizo ni wanaume tu.

Hata mabasha hawasemwi, wanaosemwa ni wale waliokataa uanaume tu.

Hata ma lwsbian hawasemwi, kwa sababu wanaonekana wanavheza tu.

Tatizo linaonekana ni watu waliokataa uanaume na kuchujua kazi ya wanawake.
Mabasha ndo watu wachafu hata kuliko shoga!
 
Asili ya mwanamke ni kufanywa, mwanaume asili yake ni kufanya.

Hii ina maana kwamba mfumo wake tu wa homoni wote una generate hisia za kufanywa.

Na pili kufanywa, ni dhana ambayo inaweza kutazamwa kama weakness ya kimfumo kibailojia.

Mwanamke kushiriki sex kinyume na maumbile ni swala ambalo linatambulika kama taboo na hii inatiwa nguvu na mafunzo ya dini.

Jamii ime adapt huo mfumo na kuanza kui picture anal sex kwa mwanamke kama dhambi na chukizo kwa Mungu lakini pia hata kimaadili.

Na ndio maana ikibainika kwamba mwanamke amefanya hilo tendo, jamii itaonesha masikitiko lakini haiwezi ku react the same way kama ingemtokea kwa mwanaume.
 
Kibongobongo mabinti hiyo ni kazi yao.

Tatizo ni wanaume tu.

Hata mabasha hawasemwi, wanaosemwa ni wale waliokataa uanaume tu.

Hata ma lesbian hawasemwi, kwa sababu wanaonekana wanacheza tu.

Tatizo linaonekana ni watu waliokataa uanaume na kuchukua kazi ya wanawake.
Haswaa
 
Asili ya mwanamke ni kufanywa, mwanaume asili yake ni kufanya.

Hii ina maana kwamba mfumo wake tu wa homoni wote una generate hisia za kufanywa.

Na pili kufanywa, ni dhana ambayo inaweza kutazamwa kama weakness ya kimfumo kibailojia.

Mwanamke kushiriki sex kinyume na maumbile ni swala ambalo linatambulika kama taboo na hii inatiwa nguvu na mafunzo ya dini.

Jamii ime adapt huo mfumo na kuanza kui picture anal sex kwa mwanamke kama dhambi na chukizo kwa Mungu lakini pia hata kimaadili.

Na ndio maana ikibainika kwamba mwanamke amefanya hilo tendo, jamii itaonesha masikitiko lakini haiwezi ku react the same way kama ingemtokea kwa mwanaume.
Huu ni UNAFIKI.
 
Kati ya hao wawili ambaye mgongo wake ukidukuliwa ipi ni aibu kuu na fedheha??

Linda mgongo wako kwa wivu mkubwa

NB: haimaanishi wanawake wasilinde migongo yao la hasha ila katika hao wawili mwanaume ndiyo inabidi awe makini zaidi na mgongo wake maana yeye ni pump na kazi ya pump ni kupampu na siyo kupampiwa
Mwingine huyu hapa anahalalisha huku anajistukia.

Hii ni vita ya mfumodume ya kusema "mwanamke kufirwa ni kazi yake, ila mwanamme ni aibu kuu na fedheha kubwa".

Kimsingi huu ndio ujumbe hapa, nimeuweka plain and simple kuondoa lugha za ku hedge na kujishaua.
 
Back
Top Bottom