Hii kampeni si kampeni dhidi ya ushoga.
Ingekuwa kampeni dhidi ya ushoga ingewahusisha ma basha na ma lesbian.
Ni kampeni ya mfumodume.
Iko hivi, katika mfumodume, mtu anayeukataa uanaume kwa makusudi anaandamwa sana.
Kwa sababu inaonekana amejaliwa tunu kuu kuliko zote, ya kuwa mwanamme, halafu kaikataa.
Ndiyo maana mtu shoga anayefirwa anaandamwa kuliko wote.
Hata mabasha hawaandamwi sana, kwa sababu kwa kiasi fulani wanaonekana wao uanaume wao bado upo, ndiyo maana wanafanya, hawafanywi.
Ndiyo maana unakuta lesbians, ambao kimsingi ni mashoga pia, hawasakamwi sana, wanaonekana hawa ni wanawake wanacheza tu, wakipata mwanamme rijali wataacha.
Na kampeni hii imejikita katika saikolojia kwa kina mpaka wanaoifanya pengine hawajui vizuri kuwa wanaifanya.
Mpaka wanawake wanafanya kampeni ya mfumodume ya kuufanya uanaume kuwa ndiyo tuzo kubwa sana.
Ndiyo maana mwanamme anayefanywa anatukanwa sana, lakini mwanamke anayewafanya wanawake wenzake, stud, husikii kutukanwa sana, labda kama kachukua mwanamke wa mwanamme fulani tu.
Kwa hivyo, katika mfumo huu ambao hauchukii mtu kufirwa ila unachukia mwanamme kufirwa, mwanamke kufirwa inaonekana sawa tu.
Ndiyo maana mpaka kwenye nyimbo zinazopendwa sana za Bongofleva wanaongelea mwanamke kufirwa, lakini hakuna backlash.
Inaonekana ni kawaida tu.
Hii ni kampeni ya mfumodume, hata neno lenyewe shoga maana yake ni rafiki wa kike, mwanamme kuitwa shoga maana yake kaondoa uanaume wake, sasa hujaona kuwa hata neno lenyewe tu halijamgusa lesbian wala basha hapo?
Hii ni kampeni ya mfumodume.