Juu kule umeongea kuhusu serikali inavyo take advantage na Ujinga wetu
Fikiria kua tukiongea habari za ushoga tutaungana dini zote,waislamu,wakristo,wapagan,CCM,CUF,Watanzania wote kwa umoja wetu tutaungana kupiga vita jambo hilo but Watanzania haohao huwezi kuwapata kwa umoja huo wakitaka haki,Kukemea Rushwa,State killings,uwajibikaji kwa serikali
Kwamba jambo hilo ambalo ni Uamuzi wa watu binafsi ni hatari zaidi na kukera zaidi ya watu kupokwa haki zao??
Kama nusu ya nguvu inayotumika kujadili masuala ya kipuuzi ingetumika kwa kujadili mambo chanya,kama taifa tungepiga hatua ila ndio hivyo kama Taifa hatujui priorities zetu,siku ambayo Lissu ana kesi ya kunyongwa yupo mahakamani watu wapo busy kujadili magari ya Heche na Hotel room ya Lema,Week hii yote atakua Dudu baya..
Tumekua so easy to be manipulated by political spins either kwa kuanzishiwa au kwa wenyewe kujiwasha gari
Exactly.
Na haya mambo hayapo Tanzania tu, ila labda sisi tunakosa dissenting voices tunaishi kwa kufuata mkumbo sana. Kuna style fulani za watawala walioshindwa ku deliver mambo muhimu kwa wananchi ku distract watu kutoka mambo muhimu ya kiuchumi, kifalsafa, kisiasa, kwa kuwapa some stupid culture wars.
Kuna mtu Marekani aliandika kitabu kinaitwa "What's The Matter With Kansas". Watu wa jimbo la Kansas walikuwa wanapiga kura kinyume na interests zao za kiuchumi na kisiasa kwa kuaminishwa kuwa wao ni Conservatives tu.
Hiki kinachoendelea Tanzania ni sawa na hiyo habari ya "Whats The Matter With Kansas".
Watu hawana kazi, hawana elimu, wanauawa na kutekwa kama ng'ombe, wanaibiwa chaguzi, halafu kama haitoshi huyo Makamu wa Rais wa uchaguzi wa kuibiwa naye anatolewa kwa Tweet ya TISS (unauziwa maziwa feki, halafu hayo maziwa feki nayo unanyang'anywa) halafu haonekani hata kuwaelezea kwamba kajiuzulu kweli, hatujui hata kama yupo hai, CCM wanakula upinzani mpaka balozi wao mstaafu Polepole wanamtazamisha mashariki na kumchinjia baharini. Lissu naye wanajitayarisha kumchinja.
Ukianzisha biashara TRA inakukamua kodi mpaka mavi kama unaenda kuzikwa.
Ukirithi kiwanja tu ni mgogoro mkubwa sana.
Ukimaliza chuo na kukaa miaka mitano bila kazi wala si jambo la ajabu, watu washazoea hawajui kuwa hili si jambo la kawaida.
Jana niliangalia mtu Marekani analalamika kuwa wahitimu wa vyuo asilimia 66 tu ndio wamepata kazi miezi 9 baada ya kuhitimu, alikuwa analalamika ajira ngumu.
Yani tumezoea umasikini na ujinga mpaka hata hatuujui kuwa huu ni umasikini na ujinga. Tumekuwa kama yule samaki ambaye maisha yake yote anaishi kwenye maji, kayazoea sana maji, mpaka hajui kuwa anaishi katika maji!
Nikacheka sana. Nikijisemea mwenyewe huko Tanzania watu wameacha hata kuhesabu. Ukiwapa asilimia 66 ya wahitimu kazi ndani ya miezi 9 ya kuhitimu kwao watasema umeupiga mwingi sana tu.
Watu wameshindwa kabisa kuishi kwa kutumia human potential yao, unaona watu wana akili basi mifumo tu ndiyo inawaangusha.
Nchi ina maliasili nyingi sana, ila watu wana umasikini wa kutupwa, abject poverty.
Inequality kubwa sana. Tofauti kati ya masikini na tajiri nchi hiyo hiyo moja ni kama watu wanaishi Ulaya ya matajiri na Afrika ya mashenzini.
But somehow, ushoga, habari ya mtu kujiamulia ana sexual orientation gani yeye mwenyewe, a right yo self determination, a human right, ndiyo habari inayosumbua watu.
I'm like, are you for real?
Where are your priorities?