Kwanini Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wake wa Rais?

Du!!Tunatofautiana sana akili.Mbingu na nchi
 
Hujajibu hoja yangu nyingine mkuu, umejibu upande mmoja tu.

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Hujajibu hoja yangu nyingine mkuu, umejibu upande mmoja tu.

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
Mkuu ni vigumu sana kwa Samia, kutoka Zanzibar, kuendesha nchi bila kuwa na mshauri wa karibu wa bara. Akina Mwigulu Nchemba, Ndugai nk wangemla nyama mbichi. Lazima Samia ajenge ngome yake kwa kuisimamisha juu ya mtu wa bara ambae si tishio kwake, na Samia ana historia na Kikwete. Kwa hiyo Kikwete ana role kubwa sana katika uraisi wa Samia. Na bila Kikwete watu kama kina January, Nape na Ridhiwani huo uwaziri huenda wasingeupata. In fact, January alienda mbali hata ku-demand wizara anayotaka na kutofanya kazi na wateule wa Magufuli. Katika normal circumstances January angeweza kuwa waziri, lakini sio wa wizara nyeti ya Nishati, sana sana Mambo ya Nchi za Nje. Bila KIkwete January asingethubutu kuwa that bold, japo baba yake ali influence kiasi. Lakini elewa pia nguvu ya Makamba Snr inapitia pia kwa Kikwete.

Na naweza hata kudiriki kusema Kikwete hakumshauri Samia amteue Prof. Mwandosya kuwa Makamu wa Raisi kwa kuwa kama Prof. Mwandosya angekuwa makamu wa Raisi nguvu ya Kikwete kwa Samia ingeuwa ndogo sana, au haipo kabisa!
 
hawa watu wa mbeya pia wanasumbuliwa na virusi vya tribalism kama akina naniliu.
 
Mwandosya ni professional, akili kubwa na mtu mwema sana.
 
hawa watu wa mbeya pia wanasumbuliwa na virusi vya tribalism kama akina naniliu.
Tribalism unayoisema ipo kila kabila. Na labda inakuwa visible zaidi kwa watu wa Mbeya kwa kuwa ni moja wapo ya makabila yaliyosoma enzi za mkoloni na wakawa na nafasi za juu ambazo ni wazi watakuwa visible wakifanya tribalism.

Lakini ukiangalia makabila mengine yaliyosoma utaona hawana tofauti na lawama wanazopewa Wanyakyusa. utaona wana tatizo hilo hilo - Wachaga - kila siku watu wanasema Chadema ni ya Wachaga. Wasukuma - kanda ya ziwa, Sukuma Gang, Wahaya - hawa ndio usiseme kwa jinsi wanavyosema wana tribalism. Hata Wakurya utaambiwa ukiwa jeshini kama sio Mkurya wewe hupandi vyeo. Hata Samia leo hii anasemwa anapendelea Wazanzibari. Sasa ni wazi basi tribalism inategemea tu unaiongelea katika mandhali gani.
 
Nayeye akakujibu hivi huku akikuuliza:[emoji1541]

Kwa hiyo mleta mada, unataka kutuambia mambo haya ya kufikirika.

1. Kikwete alimshauri Samia kuhusu Philip Mpango awe makamu wake wa Rais. Umejuaje?

2. Kikwete hakumshauri Samia kuhusu Professor Mwandosya kuwa makamu wake wa Rais. Umejuaje?

3. Kikwete huwa yuko busy kumshauri Samia kuhusu nani ashike nyazifa nyeti za serikali yake. Umejuaje?

4. Kitu chochote Kikwete anachomshauri Samia, ni lazima Samia afuate. Umejuaje?

Msingi wa hoja yako uko kwenye dhana ya kusadikika (assumption)


cc😡Synthesizer
 
Unasikitisha pamoja na uzoefu wako hapa JF.
Kwa hiyo watu kama wewe mna prefer PROFFESSIONAL MEDIOCRITY, au uswahili uswahili katika utawala wa nchi?
 
Naunga mkono hoja!
 

Hao unao wasema sasa, muda umewatupa mkono. Kama nchi, inathamini sana mchango wao, lkn wakati ni ukuta. Unafunga ukurasa. Sasa ni kurasa za watu wengine. Kama akina trat na trab.
 
Wewe ndo Professor mwenyewe nini? Mbona upo detailed sana?
 
Sikuhizi Hana professional arrogance
 
Nayeye akakujibu hivi huku akikuuliza:[emoji1541]

Msingi wa hoja yako uko kwenye dhana ya kusadikika (assumption)


cc😡Synthesizer
Basi kuna mtu hapa haelewi maana ya assumption katika analysis, maana hoja yangu iko kwenye scenarios sio assumption. Shule tamu!
 
Hapa we huoni kama kuna tatizo la kuchanganya siasa na taaluma. Katiba yetu ndio mbovu, acha kujadili watu, angalia nafasi hizo katiba inavyozikanganya. Kikwete kaupata urais kwa tabasamu lake watanzania wakajua maisha bora kwa kila mtu, unakumbuka kauli mbiu za kipindi chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…