Kwanini Kila anayefanikiwa lazima aitwe Mwizi, atoa Kafara, Free mason, Tapeli

Mi mtu Mzima Kidogo ambaye nimeishi miongo kadhaa na kushuhudia uongozi wa awamu zote na nimekaa vijijini na mijini

Kwanini Kila mtaa au kijiji au mji mtu akionekana kupata maendeleo watu ukimbilia

1. Mwizi
2. Katoa Kafara
3. Free mason
4. Tapeli

Kwanini uwa wengi hawasujudu nguvu za kazi wanazofanya watu ?

Unakuta kijana mdogo tu anajitahidi analima kisasa zaidi mazao anayataftia soko na kuweza kuuza kwa gredi ya Juu sana! Ila kwasababu ameuza zaidi ya wengine ataambiwa ni Freemason, au anatumia madawa!

Au mtu anafanya biashara yake, amefanya utafiti wa kutosha, amejitosa kwenye ulimwengu wa biashara kwa mtaji huo mdogo au muda Mwingine mikopo ya mabenki, halali usiku kucha lakin ukisikia akianza kufanikiwa kwenye familia wanaangalia Kama kuza zezeta wanasema katolewa Kafara, au ni Tapeli au Mwizi usiku anatumia bunduki kukaba watu!

Tokea Nimezaliwa nimekua nimezaa nimekuza

Kila Tajiri hata mwenye mafanikio ya kawaida tu vijijini unapoishi, watasema ni mwizi , ni Ana chuma ulete, ametoa Kafara, wakati Wengine wamepata Mali tukiwa tunawaona kwa macho yetu kutokana na juhudi zao,

Je hii ni kutokana na uelewa finyu? Ni wivu au ni ujinga??

Nipe maoni yako, na kabla hujatoa maoni chunguza matajiri watano tu kijijini kwenu alafu jaribu kuvuta kumbukumbu uwa wanapewa sifa zipi?

Britanicca
Hata huko Kwenue akina Prighozhin na wenzake Lukeshenko ni majambazi wa miaka mingi wakishirikiani na kina Putin.

Nani ambaye hajui?
 
Hayo maneno tazama mara nyingi huwekwa akilini na jamii ya watu wavivu ni sawa na mtu anayeishi Kwa kuamini chama fulani kikitawala atapata pesa na maisha mazuri wakati yeye kakaa tu jibu ni uvivu
Inaonekana wewe ni mwizi na ukisemwa una nuna.

Matajiri wote duniani wanajua siri hii. Hakuna Clean Bilionea. Mtaje tuone.
 
Mifumo ya nchi yetu ni migumu sana kutobowa ndio maana ukifanikiwa kutobowa mapema lazima jamii iamini mwenzetu una booster.

Kwa mfano mwaka fulani nilitaka nichukuwe damu kwenye machinjio Nairobi kule hawana issue nayo niilete Tanzania kutengeza chakula cha hayo masharti yake ya kuingiza hiyo damu nilipita sijui TFDA nikaambiea nenda wizara ya mifugo na kilimo kufika wizara ya mifugo mwenyewe nilikoma masharti yake na nikaachana na hiyo biashara.

Aya juzi kati nimepata tender ya kusupply dagaa wa Bukoba ulaya kwenda EMS wanakwambia upate kibali kutoka kwa walewale wizara ya mifugo ni upuuzi mtupu.

Naweza kuwa nje ya mada ila najaribu kuonesha Bongo hakuna opportunity zaidi ya kukwamishana, ndio maana ukiupata mfumo wa kutobowa lazima watu washangae.

Halafu kingine mbongo hawezi kukuonesha njia aliyopita kihalali kupata mafanikio atakupiga porojo tu, kwahiyo utajiri wao kuhusishwa na darkness ways ni sahihi kabisa.
Ni tajie waliotoboa Tz bila kushirikiana na wezi wa ccm
 
Underlying reason ni CHUKI

Mimi naonaga huruma Sana kama Kwenye ule Uzi wa Marehemu Sauli jamaa kasemwa sana. Eti utajiri wa punje mara mkataba wa kuzimu umekata. Sijui jogoo alifanyaje

Shida sio ewe mtu mzima. Shida ni kwa watoto wadogo wanaowasikiliza wapumbavu kaka zao, baba zao, wajomba zao, rafiki zao, nk

Kijiji kwetu kuna tajiri mmoja anaitwa Hemedi mpka leo yupo, wakat tunakua kuna stori kuwa jamaa akiwa anakimbiza gari basi jua kabeba kichwa cha mtu anapeleka kuzindika. Mpka leo nikiona gar yake nakumbuka huo upuuzi
Kama unadhani kutoboa ni kwa maneno si nawewe ungekuwa umetoboa?
 
Kuna kufanya kazi kwa bidii,kufanya kazi kwa akili nyingi,kufanya kazi kwa malengo.haya yoye hayana guarantee ya mtu kuwa tajiri au kufanikiwa kwa asilimia hata 3%.

ni ngumu sana kuelewa hili kama sio mtu wa kujaribu fulsa zozote unazohisi zinaweza kukuvusha sehemu flani,ila tu uwe na mnufaika au mtu wa karibu wa mtu mwenye mahela mjini hapa.

Watu wanataka mbinu za kupiga hatua hamsemi.matokeo yake ni kusimangana kama hivi na kuja kutuchamba kama akima chief godlove.
 
Ndio njia yetu masikini ku justify umaskini wetu. Tupuuze tu.
Mkuu kama unadhani kutoboa ni Rahisi wewe umetoboa? Kama sivyo ni kwanini?

Tuseme basi wewe bado unajitafuta je Baba yako naye bado anajitafuta? Je alitoboa?

Mabilionea wote hapa Tz Enzi za Magufuli walikubwa na Kashfa za Wizi, uporaji, utapeli, ufisadi.

Sasa katika mazingira kama haya unawasemaje wanatuhumu matajiri?

Imefika mahali huwezi kuwa tajiri kama hushirikiani na mafisadi.

Hapa Tz tu uwadindie ccm kwa mambo yao ya giza uone kama utatoboa.

Kwa hiyo maoni ya jamii kwa jamii yetu ni ya msingi.

Wewe kabwela ndio unapinga wakati huo utajiri huna na huenda ukafa hujaufikia.
 
Kuna kufanya kazi kwa bidii,kufanya kazi kwa akili nyingi,kufanya kazi kwa malengo.haya yoye hayana guarantee ya mtu kuwa tajiri au kufanikiwa kwa asilimia hata 3%.

ni ngumu sana kuelewa hili kama sio mtu wa kujaribu fulsa zozote unazohisi zinaweza kukuvusha sehemu flani,ila tu uwe na mnufaika au mtu wa karibu wa mtu mwenye mahela mjini hapa.

Watu wanataka mbinu za kupiga hatua hamsemi.matokeo yake ni kusimangana kama hivi na kuja kutuchamba kama akima chief godlove.
Watu ni wabishi. Unajua kuna watu wanajifanyaga wanaujua utajiri.

Ntakutajia matajiri walioibuka haraka haraka na mbinu zao.

1. Kiboko ya wachawi
2. Mwamposa
3. Machenzie wa kenya
4. Msukuma
5. Mwigulu.

Sasa jamii ikiwatazama hawa unadhani watapata ujumbe gani kuhusu Utajiri?

Kama unadhani kutoboa ni maneno mbona weww hujatoboa?
 
Kwa mazîngira Magumu ya huku Afrika kuwa tajiri NI ngumu Sana. Ili uwe tajiri yakupasa úwe na Moja ya Sifa tajwa Hapo juu;
1. Muuza Unga,
2. Fisadi
3. Nyonyaji na mdhulumaji WA fedha za Wengine. (utapeli)
4. Urithi
5. Mambo ya kichawi na ushirikina Kwa vile hayathibitiki siwezi kuyaweka.

Kukuta tajiri aliyetoboa kwa Haki NI ngumu Sana Kwa mazîngira ya Afrika.
 
Mkuu kama unadhani kutoboa ni Rahisi wewe umetoboa? Kama sivyo ni kwanini?

Tuseme basi wewe bado unajitafuta je Baba yako naye bado anajitafuta? Je alitoboa?

Mabilionea wote hapa Tz Enzi za Magufuli walikubwa na Kashfa za Wizi, uporaji, utapeli, ufisadi.

Sasa katika mazingira kama haya unawasemaje wanatuhumu matajiri?

Imefika mahali huwezi kuwa tajiri kama hushirikiani na mafisadi.

Hapa Tz tu uwadindie ccm kwa mambo yao ya giza uone kama utatoboa.

Kwa hiyo maoni ya jamii kwa jamii yetu ni ya msingi.

Wewe kabwela ndio unapinga wakati huo utajiri huna na huenda ukafa hujaufikia.
Utajiri ni jambo zito,bahati mbaya wenye nao huwa wanapenda na wanataka tuamini ni akili na nguvu zao zimewafikisha walipo,tukigoma kabisa kama wasivyotaka wanatuchamba.

Unaotea fulsa ya kukuingizia angarau 1mln kwa mwezi,unakula hela husika miezi 6 baadae anatokea mshindani ama bishara inaanza kuyumba kwa changamoto yoyote tu.

Kwa sisi wenye imani na Mungu alisema wazi tajiri kuuona ufalme wa mbinguni ni kizaa zaa,sababu bila faulo na kanjanja huwezi tajirika.
 
Kwa mazîngira Magumu ya huku Afrika kuwa tajiri NI ngumu Sana. Ili uwe tajiri yakupasa úwe na Moja ya Sifa tajwa Hapo juu;
1. Muuza Unga,
2. Fisadi
3. Nyonyaji na mdhulumaji WA fedha za Wengine. (utapeli)
4. Urithi
5. Mambo ya kichawi na ushirikina Kwa vile hayathibitiki siwezi kuyaweka.

Kukuta tajiri aliyetoboa kwa Haki NI ngumu Sana Kwa mazîngira ya Afrika.
Mkuu mbona kuna wengine wametoboa BILA hayo mambo
Mfano Bakhressa au mzee mengi
Britanicca
 
Kwa mazîngira Magumu ya huku Afrika kuwa tajiri NI ngumu Sana. Ili uwe tajiri yakupasa úwe na Moja ya Sifa tajwa Hapo juu;
1. Muuza Unga,
2. Fisadi
3. Nyonyaji na mdhulumaji WA fedha za Wengine. (utapeli)
4. Urithi
5. Mambo ya kichawi na ushirikina Kwa vile hayathibitiki siwezi kuyaweka.

Kukuta tajiri aliyetoboa kwa Haki NI ngumu Sana Kwa mazîngira ya Afrika.
Atakayepinga hizi Nondo ajiandae kufa maskini tu.
 
Mi mtu Mzima Kidogo ambaye nimeishi miongo kadhaa na kushuhudia uongozi wa awamu zote na nimekaa vijijini na mijini

Kwanini Kila mtaa au kijiji au mji mtu akionekana kupata maendeleo watu ukimbilia

1. Mwizi
2. Katoa Kafara
3. Free mason
4. Tapeli

Kwanini uwa wengi hawasujudu nguvu za kazi wanazofanya watu ?

Unakuta kijana mdogo tu anajitahidi analima kisasa zaidi mazao anayataftia soko na kuweza kuuza kwa gredi ya Juu sana! Ila kwasababu ameuza zaidi ya wengine ataambiwa ni Freemason, au anatumia madawa!

Au mtu anafanya biashara yake, amefanya utafiti wa kutosha, amejitosa kwenye ulimwengu wa biashara kwa mtaji huo mdogo au muda Mwingine mikopo ya mabenki, halali usiku kucha lakin ukisikia akianza kufanikiwa kwenye familia wanaangalia Kama kuza zezeta wanasema katolewa Kafara, au ni Tapeli au Mwizi usiku anatumia bunduki kukaba watu!

Tokea Nimezaliwa nimekua nimezaa nimekuza

Kila Tajiri hata mwenye mafanikio ya kawaida tu vijijini unapoishi, watasema ni mwizi , ni Ana chuma ulete, ametoa Kafara, wakati Wengine wamepata Mali tukiwa tunawaona kwa macho yetu kutokana na juhudi zao,

Je hii ni kutokana na uelewa finyu? Ni wivu au ni ujinga??

Nipe maoni yako, na kabla hujatoa maoni chunguza matajiri watano tu kijijini kwenu alafu jaribu kuvuta kumbukumbu uwa wanapewa sifa zipi?

Britanicca
Mara nyingine uelewa finyu hasa ma3neo ys vijijini,ila pia yapo yake mafanikio ya mwendokasi yani mla kwa urefu wa kamba ka kwapua anaenda kuzifichia kwenye mafanikio ya kuzuka,hupewa tafsiri isiyo sahihi.
 
Mf. A na B wamelima mashamba yanayopakana, wana mtaalamu mmoja na wanatumia mbinu zanazofanana. Matokeo yake B anavuna mara 10 ya A. Hapo kuna nini?
 
Back
Top Bottom