Mengi wamechangia wenzangu hapo juu na baadhi ya sababu wewe pia
britanicca umezianisha hapo.
Kikubwa ambacho nilichojifunza, ambacho najifunza na bado naendelea kujifunza ni suala linalohusiana na KUJITAMBUA.
Kujitambua kuna uhusiano mkubwa sana na mambo mengi na yote ambayo yanatokea na kuyaishi katika maisha yetu.
Ukichunguza na kuangalia kwa kina utaona watoto, vijana na watu wazima hawajui utambulisho wao na ukimuuliza swali wewe ni nani? Atakujibu yeye ni
ephen_ au yeye ni
min -me na pengine atakujibu yeye ni
GENTAMYCINE,
Mwifwa,
raraa reree n.k .n.k
Twende kwenye mada yetu sasa, ili kuweza kujitambua kwanza tunapaswa kutambua na kufahamu identity zetu halisi, je, mimi ni nani? Sisi ni akina nani? Mimi nimetoka wapi? Mimi nilikuwa wapi? Je, kwanini ninaishi? Kuzaliwa kwangu ni kwa bahati Mbaya? Wajibu wangu ni nini katika maisha yangu? Wajibu wangu ni nini katika ulimwengu huu au dunia hii? Je, nimezaliwa ili niteseke? Nimezaliwa ili nisheherekee maisha?
Hayo ni maswali ambayo ili uweze kujitambua na kufahamu utambulisho wako halisi tunapaswa kuwa na ufahamu wa kina na majibu yake kwa ufasaha..
Sifahamu au pengine sina uhakika( nipo tayari kujifunza na kurekebishwa). Watu wengi sana katika ulimwengu huu wamefungwa na wapo katika gereza kwa kutokujua na kujitambua kuhusiana na wao ni nani? Identity ambazo wamekuwa wakijinasibu au kudhani katika fikra zao zimewafanya washindwe kufahamu kabisa life purpose yao au madhumuni ya maisha yao.
Mafundisho mengi hasa ya baadhi ya dini ambazo ni tumejishikiza au kujifunganisha nazo naongelea dini kongwe zimekuwa ndio gereza au jela kubwa ambazo zimekamata na kufunga ufahamu wa watu wengi sana.( nitajitahidi sana kuepuka kuongelea na kugusa Imani zetu kadiri nitakavyoweza katika Uzi huu).
Mafanikio na safari ya kujitambua inaanza kwa kujiuliza na kujihoji maswali mwenyewe na kujiongelesha wewe na wewe na kuongea wewe na wewe, hapa namaanisha ili niweze kufahamu na kupata maswali naongea na mimi na ninafanya majadiliano na mimi mwenyewe kwanza na mara kwa mara.
Katika safari hii ya kujitambua na kufahamu utambulisho wako ni lazima utoe makorokoro na makorokocho yote uliojaziwa au kupewa na kufundishwa katika fikra zako. Hapa una empty kabisa mind yako na unakuwa mjinga, ndio nimesema unakuwa mjinga ili uweze kuruhusu weledi, hekima na werevu kuingia ili uweze kufikia malengo ya kujitambua! Inaitwa ujinga wa werevu ambao ni bora na una manufaa kuliko werevu wa ujinga. Tunapaswa kuwa wajinga wa werevu ili tuweze kupata wisdom au hekima ambayo itakuwa na msaada mkubwa katika safari yetu.
Sasa basi baada ya wewe unaesoma Uzi huu kukubali kwa muda kuwa mjinga wa werevu tunaweza kuendelea, nikiongelea ujinga nafurahi sana ninapokumbuka maneno ya mama
FaizaFoxy ; umekwenda shule kusomea ujinga!
Fikra zetu na mawazo yetu yanapokuwa huru bila kujifungamanisha au kujishikiza na chochote ndipo hapo hekima na werevu wa kujua na kutambua utambulisho wako halisi unaupata kutoka ndani mwako na sio kutoka nje, hapa nasema majibu na ufahamu wa wewe ni nani upo tayari ndani yako ila ukishindwa kujua au kutambua kutokana na kuwa gerezani na kutokuwa huru. Hapa Unajikuta unaishi katika upeo huru na unaishi katika uhuru wa nafsi yako.
Mara nyingi na wengi wetu tumekua tukijitambulisha kutokana na jinsi tulivyo, muonekano wetu, kazi zetu, taaluma zetu, makabila yetu, rangi zetu, dini zetu, vyama vyetu, jinsia zetu n.k. n.k! Hapa ninachoweza kusema tumekuwa tukibeba na kungangania fake identity pasipo kufahamu na kutambua madhara na faida ya utambulisho tunaoungangania. Akili zetu au mind zetu zinatuweka katika mtego mkubwa kutukamata na kutuweka gerezani.
Je, mimi nani hasa? Wewe ni nani hasa? Mimi na wewe tunatofauti gani hasa?
Mimi ni ROHO, wewe ni ROHO, mimi na wewe ni ROHO hatuna tofauti.
Kama sisi ni Roho basi ni wazi kuwa sisi tulikuwepo, tupo na tutaendelea kuwepo na sisi hatuna mipaka tupo kila mahali hatuna ukomo wa kufanya chochote na zaidi tumekamilika na hatuna mapungufu kwa chochote! Sisi kama roho ni wakamilifu.
Sisi kama roho hatuhitaji kuomba sababu tunavyo vyote na tunamiliki vyote, vyote vilivyopo ni vya kwetu na vipo chini yetu katika mamlaka yetu.
Sisi kama roho sio tu tuna mamlaka au tumepewa mamlaka bali sisi ni mamlaka kamili inayojitosheleza na hatuhitaji msaada sababu tumekamilika.
Kumbuka tulipo kuwa watoto tuliweza na tulikuwa na mamlaka ya kumiliki chochote kile ndio maana mtoto utamsikia alisema lile ni gari langu na ile ni nyumba yangu! Umiliki unaanzia kutoka kwenye mawazo yetu na fikra zetu.
Mwisho ila sio kwa umuhimu utajiri ni matokeo ya kujitambua na kutumia nguvu na uwezo tulionao kupata, kufanya, kuishi na kumiliki chochote ukitakacho katika ulimwengu huu. Rasilimali zilizopo ulimwenguni ni zetu kwa pamoja na kwa manufaa yetu sote na sio kwa ajili ya wachache.
Ulimwengu umekamilika unatoa chochote kwa yeyote anayehitaji na yupo na mwenye tayari kupokea.
britanicca mkuu wangu, nashukuru kwa mada chokonozi hii. Natumaini itawasaidia na kuwafungua wengi.
Uzi huu ukafungue macho yako ya ndani na ukawe ufunguo wa yote uyatakayo.