Kwanini Kila anayefanikiwa lazima aitwe Mwizi, atoa Kafara, Free mason, Tapeli

Mkuu mbona kuna wengine wametoboa BILA hayo mambo
Mfano Bakhressa au mzee mengi
Britanicca

Ndîo mmoja Kwa Mia Moja Mkûu.

NI Sawa Ile kauli isemayo Hakuna binadamu mkamilifu lakini haimaanishi binadamu wakamilifu hawapo. Ila nadra kuwapata.

Ni Sawa Umwone Mpare Mrefu alafu uje kusema Wapare NI warefu.

Kwa Afrika ukubali au ukatae Huwezi kuwa tajiri Bila dhulma.

Unakuta NI Dokta, uibe vifaa cha hospital na madawa uuze au upeleke kwèñye hospitali yako.

Binafsi tangu kuzaliwa sijawahi kuona Kwa macho yàngu tajiri asiye na sîfa Kati ya moja ulizozitaja
 
Ni roho za kimasikini tu

Hauwezi kukuta hata siku moja tajiri anamsema tajiri mwenzake ana pesa zake za kishirikina

Uliwahi sikia muuza madawa akamtaja muuza madawa Mwenziwe?

Haya kûna ishu ya Malalamiko ya wafanyakazi wa viwandani kulipwa Mishahara ya kitumwa. Uliwahi sikia Wamiliki WA viwanda wakilizungumzia Jambo Hilo?
 
1.UJINGA
2.CHUKI
3.WIVU
4.USHIRIKINA....kutoamini utajiri hutoka kwa Mungu
 
Tunazungumzia utajiri wa kishirikina

Hawawezi kusemana Kwa sababu Lao Moja.

Huwezi msema Maskini mwenzako Kwa uzembe wa kuwa Maskini Wakati hata wewe NI Maskini.
Halikadhalika Huwezi msema tajiri mwenzako kuwa utajiri wake ni wadhulma Wakati na wéwe unamambo yako ya dhulma. Hutokuwa tayari yaanikwe
 
Tuendelee kutafuta hela mkuu. Hizo ni kauli za mtu mwenye njaa
 
Hizo ni mbinu za shetani za kutaka atukuzwe yeye tu,vitu vyote vinavyopatikana kihalali vina mkono wa Mungu,lakini kwa ujanja wa shetani anataka hata kile ulichopewa na Mungu kionekane kuwa kimetokana na shetani kwa njia ya wizi,kafara,dhuruma n.k.
 
Ujinga umetamalaki. Uwezo mdogo wa kufikiri. Ujinga wa njia za kukusanya mali(Wealth Accumulation).
 
wivu akili za kimaskini na kukosa kazi, na kujitetea kwakua hakuna juhudu zimefanyika....... tukiacha hizi mambo za kufuatilia watu tutaenjoy maisha
 
Umasikini mbaya sana mzee tafuta sana hela🤣
 
Ni kwa sababu mazingira ya kibiashara hapa Afrika yanafanya mtu awe mwizi, mchuna ngozi wenziwe, mtoa makafara, muua kina Haji Manara (maalbino), Free mason na tapeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…