Kwanini Kila anayefanikiwa lazima aitwe Mwizi, atoa Kafara, Free mason, Tapeli

Hakuna utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii Tanzania ndo maana.

Watu hawaoni kwamba kufanya kazi kwa bidii kunalipa.

Kwahiyo wanafuatilia habari za watu kuwa matajiri wakubwa na wanawaza utajiri na Range Rover huku hata mfukoni hana senti.
 
Lakini hizo pesa za ufreemason utapeli pia zipo tusikatae japo sio matajiri wote!

Pia hata ukiwa na pesa za njia hizo zilizotajwa kwenye uzi, inahitaji uendelee kujituma na sio uvivu
Pesa za Freemason hazipo ni uongo.

Jaribu kupitia threads humu utajifunza.

Kuna moja inaitwa “Freemasons inside out”

Freemason ni jamii ya watu siyo wachovu. Na hakuna miujiza zaidi ya wao kusaidiana na wanachaguana. Huwezi ingia tu kama unavyoona matapeli wanaweka namba za simu huko mtaani eti kujiunga freemason.
 
Hata hao freemasons, waganga majini wanataka mtu mwenye nyota yake
Sio nyota yako ya kinyesi hupati pesa ng'oo

Hivyo kama utapeli, ufreemason, majini ni rahisi waende na wao tuwaone.
Hakika Ila sasa wasione kila aliyefanikiwa wakadhani ni wa namna Hiyo
 
Exactly and Masonic movement started in 1970’s
 
Sijajua kwanini Nimetajwa katika huu Uzi.
 
Africa tutakuita mchawi ila ulaya watasema ni mchapa kazi
 
asilimia kubwa ya utajiri si halali
hata akina ronaldo utasikia wamekwepa kodi
 
MKuu kupata Kila mtu anapata utajiri au maisha fulani Kwa juhudi binafsi!

Ishu inakuja baada ya kupata Nini kinakupata!!

Bila kukwepa kodi vizuri au kuwa mjanja mjanja kibongo bongo hutoboi coz mifumo ya kodi imekaa kinyonyaji sana kuliko uhalisia was kipato husika!!
Ndio maana mkwepa Kodi huitwa mwizi!

Matajiri wanajipendenkeza Kwa wanasiasa Ili kukwepa panga la Kodi na kupata favor!!

Lakini kumbuka kupata jiwe la kweli lazima upandishe viwango vya kujitolea binafsi au kivingine,au magendo!huwezi tajirika kihalali kimfumo ni ngumu sana labda uwe na connection!!!

Kama unabisha wewe ni mtu wa mfumo hebu fuatilia ishu ya yule "Rama was kariakoo alijipiga risasi"utajua hujui!

Juhudi bila baraka za Dola na mfumo inakula kwako peupe kabisa Wala sio utani!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…