DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Kiistoria, kila unapobaki mwaka mmoja au miwili kuelekea uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini, ndani ya chadema kunaibuka minyukano.
Hii ilikuwa kweli mwaka 2008 na 2009, kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010
Na Ikawa kweli 2013 na 2014, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
Na sasa ni kweli pia mwaka huu ukiwa umebaki mwaka mmoja tu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, tunaona minyukano
Mwaka 2008 Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Chadema taifa, na mbunge wa Tarime, marehemu Chacha wangwe anatoa waraka fulani kwenda kwa wanachama wote ndani ya chama chao.
Ndani ya waraka ule, Wangwe anaeleza nia yake ya kugombea uenyekiti wa Chama hicho huku akianisha sababu...
Sababu ya kwanza ya Wangwe ni kuhusu matumizi mabaya ya ruzuku.
Ifahamike kuwa kipindi hicho chama hicho kilikuwa kikipokea ruzuku ya milioni 66 kwa mwezi
Wangwe akaeleza matumizi ya ruzuku ile hayakuwa na uwazi wala baraka za vikao vya chama.
Na Kuwa Mbowe aliwaambia wajumbe wenzake kuwa, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, alikikopesha chama hicho kiasi cha dola za Marekani 181,949 (sawa na mil 218 wakati ule)
Kuwa hadi mwaka 2008, chama kilishamlipa Mbowe milioni 175
Lakini Wangwe akatia mashaka kwenye hili..
Wangwe alihoji akaunti ipi ya chama iliingiziwa pesa hizo?
Kwa hundi ipi? Tarehe gani?
Na Kwa vikao vipi vya chama vilivyotathmini na kuupitisha mkopo ule?
Wangwe akahoji mbona wao huingia gharama majimboni mwao na hawajakidai chama?
Ukiachana na hoja hii, Wangwe alitoa sababu nyingine zilizomsukuma kugombea uenyekiti
Upendeleo kwenye uteuzi wa wabunge wa viti maalumu na ajira za watumishi wa chama, na uongozi wa kibabe.
Baada ya waraka huu, Wangwe akashukiwa kama tai na kamati kuu ya Chadema
Wangwe aliishia kuvuliwa cheo na uanachama wa chama chake kwa tuhuma kuwa anatumiwa na mfumo kuiba siri za chama na kuzivujisha.
Siku chache baadae, Wangwe akafa kwa ajali mbaya maeneo ya Pandamili akitokea Dodoma kwenda Dar Es Salaam
Huku dereva wake Deus Mallya akinusurika..
Huo ukawa ndio mwisho wa ndoto ya Wangwe kuukwaa uenyekiti Chadema.
Mwaka 2009, aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Zuber Kabwe naye akatangaza kutamani "kiti cha enzi"
Ikafata minyukano ndani kwa ndani ambayo ilitulizwa
Ukafanyika uchaguzi mkuu mwaka 2010
Baada ya uchaguzi wa 2010, mambo hayakuwa tena sawa baina na Mwenyekiti Mbowe na Naibu katibu mkuu wa chama hicho (bara) ndugu Zitto Kabwe
Zitto akashutumiwa kuwa ni mtu wa mfumo
Gazeti moja likaandika jinsi Zitto alivyokuwa akiwasiliana sana na afisa usalama taifa Jack Zoka.
Ilidaiwa kuwa wakati wote wa kipindi cha uchaguzi mkuu 2010, Zitto alikuwa akiwasiliana mara nyingi sana na aliyekuwa naibu Mkurugenzi wa Usalama wa taifa Bw. Jack Zoka
Akatuhumiwa kuwa mawasiliano yale yalikuwa ni ya kukiuza chama chake wakati wa uchaguzi..
Zitto aliendelea kuwa kimya bila kujibu tuhuma zozote alizorushuwa.
Nachelea kusema alikuwa kimya huku nyuma ya pazia akiratibu mipango kabambe
Haya yalikuja kuthibitika mwaka 2012 baada ya wanachama vijana wa chama hicho kuanza kuvuana nguo hadharani.
Kwa mujibu wa Ben Saanane Ben Saanane
aliyekuwa msaidizi wa Mbowe, alieleza juu ya kuanzishwa kisiri kwa kundi la PM 7 ndani ya chama hicho
Kundi hili ambalo mwanzoni lilijiita Patriotic Movement liliundwa na watu 7
Tuwajue kwa uchache wao!
Mwenyekiti wa kundi hili alikuwa Juliana Shonza huku makamu akiwa ni Habib Mchange..
Kwa mujibu tena wa Ben Saanane, malengo ya kikundi hiki yakahama kutoka kwenye kuwajengea vijana uwezo kisiasa hadi kugeuka kuwa Pindua Mbowe 7
Kuwa wafadhili wao walikuwa ni David Kafulila, Mwigulu Nchemba, Deo Filikunjombe na Hussein Bashe
Bila kujua Ben Saanane ni pandikizi
Ben Saanane anadai kundi hili lilikuwa likifanya vikao kwa baraka za Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo na wakaamua kujiita majina ya uficho wawasilianapo
INAENDELEA HAPA
www.jamiiforums.com

- Juliana Shonza,makamu mwenyekiti BAVICHA
- Habib Mchange
- Mtela Mwampamba(Jiwe alimtumbua kisa Jokate)
- Festo Sanga (Mbunge wa sasa Njombe)
- Exaud Mamuya
- Gwakisa Burton
- Ben Saanane
Mwenyekiti wa kundi hili alikuwa Juliana Shonza huku makamu akiwa ni Habib Mchange..
Kwa mujibu tena wa Ben Saanane, malengo ya kikundi hiki yakahama kutoka kwenye kuwajengea vijana uwezo kisiasa hadi kugeuka kuwa Pindua Mbowe 7
Kuwa wafadhili wao walikuwa ni David Kafulila, Mwigulu Nchemba, Deo Filikunjombe na Hussein Bashe
Bila kujua Ben Saanane ni pandikizi
Ben Saanane anadai kundi hili lilikuwa likifanya vikao kwa baraka za Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo na wakaamua kujiita majina ya uficho wawasilianapo
- Shonza akajiita Benazir
- Mchange akajiita Mdude
- Mwampamba akajiita Kony
- Sanga akajiita Tuntemeke
- Zitto akajiita Prezzo
INAENDELEA HAPA
Kwanini kila ikifika Mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi Lazima kutokee Mikwaruzano Ya Kisiasa CHADEMA Ya FAM Hii ndo SIRI ILIYOJIFICHA
Kiistoria, kila unapobaki mwaka mmoja au miwili kuelekea uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini, ndani ya chadema kunaibuka minyukano. Hii ilikuwa kweli mwaka 2008 na 2009, kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010 Na Ikawa kweli 2013 na 2014, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Na sasa ni kweli pia...