Kwanini Kituo cha mafuta 'Rupeez Oil' kimejengwa kwenye hifadhi ya barabara Kimara Stop Over?

huu uzi hauna picha, na ule uliorudiwa hauna picha pia
 
Hii sijawahi kuisikia kabla
 
Majibu ya kindezi haya.. wizara ya mazingira ipo wapi? Wizara ya ujenzi ipo wapi?
 
Hiyo pesa hata haiendi tanroad.. kuna jamaa huko mbeya nimeambiwa ametumia mil 24 kupata kibali cha kujenga sheli ambacho hutolewa kwa tsh laki 240
Yule amepanga eneo la Tanroad kwa muda fulani, anawalipa Tanroad hela, siku wakitaka tumia eneo anapewa notice anaondoka bila kudai chochote
 
Eneo lile halitakiwi kuwa na kituo cha mafuta
 
Enyi vigogo mnapoamua kufanya jambo fulani tumieni hekima msitumie mabavu fuateni sheria msijiweke juu ya sheria msifanye ndivyosivyo upenuni mwa umma, msiwe wavunja sheria namba moja.
 
Hiyo pesa hata haiendi tanroad.. kuna jamaa huko mbeya nimeambiwa ametumia mil 24 kupata kibali cha kujenga sheli ambacho hutolewa kwa tsh laki 240
Anajua itarudi
 
Apostle Kuna muujiza
 
Mtu wa brela humu atusaidie kujua jina la mmliki wa kituo. Unaweza kukuta shamba la bwana heri.

Tatizo sheria iliyotumika kubomoa nyumba za wakazi wa kimara ni sheria ya TANZANIA HIGHWAY ORDINANCE OF 1945.

Mpangaji hana kosa Mkurugenzi wa TANROADS hana analolijua. Ila wanasisa wetu na wanaharakati wao hili hawalioni isipokuwa maridhiano ya kuzuia tumbo lisitetemeshwe na mwili. Sufuria hata likiwa safi kiasi gani hata liwe jipya, likiwekwa kitandani ni uchafu.
 
Kipindi kimefika sasa barabara zipishe sheli na makazi ya watu sio makazi ya watu, sheli zipishe bara bara... mambo yanabadilika jamani
 
Hatimaye kamati ya kudumu ya bunge imeamrisha kituo kivunjwe, je ni sahihi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…