Kwanini kujenga nyumba imekuwa ni fashion kwa Watanzania?

Kwanini kujenga nyumba imekuwa ni fashion kwa Watanzania?

Mleta mada sawa unaweza kuwa umefikria nje ya box au kuangalia maisha ya wenzet nje ya nchi
Ila kwa muktadha wa kitanzania ni adha kubwa sana kwa wababa wenye nyumba ndio mana unaona mtu anapambana ajenge aondokane na adha za wenye nyumba
 
Imekuwa ni jambo la kushangaza kwa watanzania wengi kuamua kujenga na kuendelea kuishi maisha yale yale

Unakutana fundi fenicha aliyefanya kazi miaka 15 anakuambia anamalizia ujenzi ukiangalia ufanyaji kazi bado wa kusubiri hela advance kwa mteja hafikirii kabisa kuwa na store kubwa utakayotoa faida kubwa zaidi kwa haraka zaidi kutokana na uzoefu wake.

Unakutana na dereva yeye miaka na miaka anaendesha gari za watu anakuja na habari njema amejenga ni vyema lakini kwanini asikilie kumiliki gari yake.

Unakutana na kijana kinyozi ana uzoefu wa miaka saba anakuambia nimejenga vyumba vitatu nataka nihamie kwangu ni jambo jema lakini hafikirii kama pesa hizo kama angetumia kufungua barbershop kubwa ambayo ingempa faida maradufu
Nyumba ni asset kwa maisha ya baadae, mfumo wetu umekaa kizushi sana in the sense kwamba ukisema urisk hela uweke kwenye biashara instead of asset inawezapotea na ukakosa vyote. Mtu anaona ni bora ajenge akae kwake kwanza halafu ndio atafute namna ya kufanya biashara. Somo la kuinvest and reinvest pamoja na ujasiriamali hatujafundishwa mashuleni toka tukiwa watoto. Sisi tumekuwa tukiwaona wazazi wakiajiriwa na wakijenga sasa sisi ni nani tusijenge tupanue biashara, leo nikizeeka na biashara ikadoda ntaenda kukaa kwa nani na kodi siwezi lipa tena- haya ndio maswali watu wengi wanakuwa wakijiuliza mtu unakuta anaona wacha ajenge halafu akishakaa kwakwe atatafuta kabiashara kakumsukuma mdogo mdogo mpaka azeeke.
 
Katika mahitaji matatu ya binadamu unayosema hayapo ila nyumba ipo. Nyumba ni makazi ya kudumu yabinadanu, kujenga ni muhimu.
 
Halafu unakuta uliyeandika huu uzi upo ndani kwenye nyumba/chumba cha kupanga...

Unawaza utampaje hela yako mwanadamu mwingine (landlord)
 
Ndio mfumo wa maisha kwa sisi watanzania, serikali haiwezi kujenga kwa ajili ya watu wake, tupo na serikali masikini kama sisi. Hivyo the best option ni kujiwekea assets kama nyumba na viwanja kwa ajili ya baadae.

Kwa nchi zilizoendelea hali ni tofauti kidogo, tusijilinganishe.
 
Mtoa mada upo sahihi sana, nikiri hata mimi nimezika pesa nyingi sana kwenye nyumba, pesa ambazo pengine ningewekeza kwenye biashara ningekua mbali sana
Ungefika mbali au ungerudi mbali yote yanawezekana kwenye biashara mkuu
 
Shukuru kukuta wazazi wako wamejenga ndio maana kujenga unaona kupoteza pesa, ungezaliwa ukakuta wazazi wamepanga, arafu mpo jinsis tofauti mzee kapanga vyumba viwili tu, chumba na sebule, kitanda kipo sebuleni wanalala dada zako, wewe mtoto wa kiume umeombewa kulala kwa jirani kwa mzee abas maana yeye ana watoto wa kiume, kwaiyo unaenda kulala uko aisee ungejua thamani ya kujenga nini

Ngoja nishie hapa maana naweza kulia nakumbuka machungu
 
Nyumba ya kukaa wewe kwenye economics ni asset ila in real sense nyumba ya kukaa si aset, sababu in real sense anything that puts money in your pocket ndio asset kama it takes money out of your pocket sio asset... Frame za biashara nyumba za kupangisha ndio asset hizi za kukaa unalipa kodi ya jengo, ardhi, umeme na maji wakati yenyewe haizalish kitu hapa ni tatizo tu na lenyewe
Kwani ukipanga hulipi maji na umeme
 
Unalipa mkuu ila nyumba ya kuishi sio asset
Ni asset.

Ngoja nielezee kwa nini?

Asset(Mali)
Ni kitu chochote kinachokuingizia faida(Cash inflow) au kinapunguza deni(Cash outflow)

Hivyo mtu aliyekuwa amepanga Nyumba halafu analipa rent ya 150,000/= kwa mwezi na umeme na maji tuassume 20,000/=

Akafanikiwa kujenga Nyumba yake hivyo rent halipi lakini umeme na maji(fixed overheads)

Hivyo kujikuta anaokoa 150,000 kwa mwezi mara mwaka itakuwa almost 1.8M
ambazo atazielekeza kwenye kwingine

Siku hizi property tax ni inclusive maana imeingizwa kwa Luku hivyo ukae Nyumba ya kupanga au kwako utalipa.

Utabakia na Kodi ya ardhi.

Hivyo kwa hapo Nyumba itakuwa imepunguza Cash outflow hivyo msikalili.

Lakini ipo namna ya kuielezea kwa kutumia statement of financial performance na position kuliko cash flow ikiwa sijaeleweka.

Sawa mzee wa ICT.
 
Ahahaha hii statement ya mwisho "Sawa mzee wa ICT" its like you know me au labda umesoma sehemu ahahaha nimecheka sana ngoja nikubaliane na wewe lakin nifanye research pia... Haya bana...
 
Ukiwa na familia nyumba ni muhimu sana ni asset nzuri asikudanganye mtu ukiwa kwako unaweza hata kuuza chips kiepe nje kwako ukala na familia ya kufunga kuku ila nyumba za kupanga ni matatizo kweli.
Kweli kabisa kwako ni kwako Tena ukiwa uwezo unajenga hata sita na ardhi haishuki thamni
 
Imekuwa ni jambo la kushangaza kwa watanzania wengi kuamua kujenga na kuendelea kuishi maisha yale yale

Unakutana fundi fenicha aliyefanya kazi miaka 15 anakuambia anamalizia ujenzi ukiangalia ufanyaji kazi bado wa kusubiri hela advance kwa mteja hafikirii kabisa kuwa na store kubwa utakayotoa faida kubwa zaidi kwa haraka zaidi kutokana na uzoefu wake.

Unakutana na dereva yeye miaka na miaka anaendesha gari za watu anakuja na habari njema amejenga ni vyema lakini kwanini asikilie kumiliki gari yake.

Unakutana na kijana kinyozi ana uzoefu wa miaka saba anakuambia nimejenga vyumba vitatu nataka nihamie kwangu ni jambo jema lakini hafikirii kama pesa hizo kama angetumia kufungua barbershop kubwa ambayo ingempa faida maradufu
Kuna biashara yoyote unayofanya? Na km unabiashara mpaka sahizi umefikia wapi? Je unakiwanja,umejenga? Je una gari? Ukinijibu hili nitakuja ku comment
 
Back
Top Bottom