Kwanini Magufuli aliwaogopa sana Nape na January Makamba?

Kwanini Magufuli aliwaogopa sana Nape na January Makamba?

Wote waliohusika kumsema Magufuli kwenye zile sauti zilizovuja, wote walipotezwa kisiasa kasoro Nape na Makamba

Ngelejea japo hakuwa mshiriki mkubwa na kuwa wa kwanza kuomba msamaha lakini alipotezwa kwenye ubunge baada ya Magufuli kumfadhili mshindani wake

Membe alifukuzwa, Kinana nae akawa suspended kwenye chama(hata hivyo baadae Magufuli alimrudisha licha ya Kinana kutoomba msamaha rasmi),

Lakini Nape na Makamba japo ndio walikuwa viongozi wakuu wa uasi ule, Magufuli aliwaacha wakapita kwenye kura za maoni ndani CCM na majina yao hakuyakata na wakarudi bungeni na sasa ni mawaziri wenye nguvu kwenye serikali ya Samia

Sasa nauliza kwa nini Magufuli alikuwa anaogopa kuwaadhibu hawa watu?

Leo hii wafuasi wa Magufuli wanateseka sana wakiona Nape na Makamba wanavyotesa na kuvimba huku wakiwatupia vijembe
Ni kawaida kwa mtu muoga na mjinga kutokupenda changamoto.Hakuna la zaidi.
 
Kwa jinsi tunavyoelezwa alivyokuwa Magufuli basi nilitegemea kuona akiagiza Makamba na January wauliwe au watekwe.
Kwa alichokifanya kwa Lissu nilidhani hawa wangefukuzwa chama, ila sijui kwanini aliwaogopa hivi
 
Nape na Makmba hawakuwa na wapinzani wa maana ndani ya CCM huko majimboni mwao; iwapo wangekuwa na wapinzani wa maana, huenda nao wangepotea. Magufuli alikuwa haogopi mtu!
Magufuli alikuwa na uwezo wa kumfanya yoyote kuwa mbunge refer kwa Katambi, Kimei, Ndalichako, etc ambao hawakua na mizizi CCM lakini akawabeba
 
We jamaa mkongwe hapa ila mindset zako km muuza magazeti wa kule sumbawanga.
Hao unaowataja Magu anahusiana nao vipi.
Yaani kweli katika hali ilivyo hiyo nchi kabisa kiongozi mwenye dhamana kubwa hivyo akaangaishane na viroboto sijui kwa lipi.
Yani kuna muda hata mimi huwa nashangaa hawa watu kimewapata nini? Yani mtu anaamini kabisa Magufuli alimteka hadi Roma mkatoliki?
 
Kwa alichokifanya kwa Lissu nilidhani hawa wangefukuzwa chama, ila sijui kwanini aliwaogopa hivi
Kipi kinakufanya ufikirie aliogopa ikiwa kweli hakuogopa kumshambulia Lissu mchana kweupe katika eneo kama lile na huku inajulikana hawaivi?

Mimi nadhani mlimkuza sana huyo Magufuli katika ubaya kiasi cha kumwita hadi Shetani ila et kumbe slikuwa anamugopa Nape na January!
 
Wote waliohusika kumsema Magufuli kwenye zile sauti zilizovuja, wote walipotezwa kisiasa kasoro Nape na Makamba.

Ngelejea japo hakuwa mshiriki mkubwa na kuwa wa kwanza kuomba msamaha lakini alipotezwa kwenye ubunge baada ya Magufuli kumfadhili mshindani wake.

Membe alifukuzwa, Kinana nae akawa suspended kwenye chama(hata hivyo baadae Magufuli alimrudisha licha ya Kinana kutoomba msamaha rasmi).

Lakini Nape na Makamba japo ndio walikuwa viongozi wakuu wa uasi ule, Magufuli aliwaacha wakapita kwenye kura za maoni ndani CCM na majina yao hakuyakata na wakarudi bungeni na sasa ni mawaziri wenye nguvu kwenye serikali ya Samia.

Sasa nauliza kwa nini Magufuli alikuwa anaogopa kuwaadhibu hawa watu?

Leo hii wafuasi wa Magufuli wanateseka sana wakiona Nape na Makamba wanavyotesa na kuvimba huku wakiwatupia vijembe.
Alijua hao ndio wenye akili ya wizi wa kura. Na yeye alikuwa muumini wa wizi wa kura.
 
Kipi kinakufanya ufikirie aliogopa ikiwa kweli hakuogopa kumshambulia Lissu mchana kweupe katika eneo kama lile na huku inajulikana hawaivi?

Mimi nadhani mlimkuza sana huyo Magufuli katika ubaya kiasi cha kumwita hadi Shetani ila et kumbe slikuwa anamugopa Nape na January!
Inashangaza ila haishangazi sana maana wanasema kila mbabe ana mbabe wake, hata simba jike huwa anazaa
 
Hivi kile chuma ni cha kuogopa hawa wadudu kweli jamani!
Nape alikwenda ikulu kwa magoti ambayo ni ishara ya woga uliopindukia!
Makamba wote 2 walitafuta hadi mashimo ya kuingia kumkimbia 🗝️🔑🤣
 
Inashangaza ila haishangazi sana maana wanasema kila mbabe ana mbabe wake, hata simba jike huwa anazaa
Sasa Nape na January walikuwa na nini cha kumtisha Rais wa nchi ambaye tunaambiwa alikuwa dikteta tena mwenye kuuwa sana watu? Hebu niambie kwa mfano angewafukuza tu kule ccm nini unadhani kingetokea ambacho pengine ndio alichoogopa rais wa nchi ambaye ni dikteta?

Mimi narudi kusema kwamba Magufuli mlikuwa mnakuza tu kwenye huo ubaya, dikteta muuwaji wa mamia ya watu bila kuogopa ndio aje kuzidiwa ubabe na Nape na Makamba?
 
Hivi kile chuma ni cha kuogopa hawa wadudu kweli jamani!
Nape alikwenda ikulu kwa magoti ambayo ni ishara ya woga uliopindukia!
Makamba wote 2 walitafuta hadi mashimo ya kuingia kumkimbia 🗝️🔑🤣
Aisee hata mimi nashangaa.
 
Aliwaogopa au wao ndo walimuogopa?,alisubiri kuja kuwatumia Kisiasa
 
Kwamba ccm nzima wenye akili ya wizi wa kura ni Nape na Makamba tu?

Kuna kitu kinafanywa na wote, wenye uthubutu wa kufanya hivyo ndio huonekana wa kwanza hata kama wako wengi.
 
Back
Top Bottom