Kwanini Magufuli anachukiwa na CCM, Chadema, ACT, CUF na wasomi wengi ila anapendwa na wanyonge?

Kwanini Magufuli anachukiwa na CCM, Chadema, ACT, CUF na wasomi wengi ila anapendwa na wanyonge?

Magufuli alipendwa na mazezeta na watu dizaini kama misukule isiyojua kufatilia vitu! Ndio maana wenye akili kama Tundu lissu walipigwa shaba mchana kweupe!
@sang'udi ni Mfano hai wa Mazezeta yanayompenda Jiwe Mpaka sasa
 
Magufulification of Tanzania ni approach iliyoacha maumivu makubwa kwa Oligarchs wengi wa Tanzania kwa sera zake za kuwabeba watu wa tabaka la chini na msisitizo wake juu ya uzalendo kwa Taifa.
Kuna siku kizazi hiki kitakua kinafundishwa Magufulicism Kama moja ya Development approach.
Watafundishwa wanao wawe ma Zuzu kama wewe
 
Hakuna watu wasiojitambua nchi hii kama hawa wanaitwa wasomi. Nje ya kufanywa watumwa na walamba miguu ya wengine hawana jipya.

Hao CCM wanajulikana kwa unafiki wao kwani wao chama ni njia ya kutengeneza deals badala ya kusimamia dira sahihi ya Taifa. Huoni wanasema chama chao kinapambana na rushwa na wakati wao ndo walezi wa rushwa nchi hii.

Wapinzani wao hawajielewi ndo maana kila siku wana kazi ya kuhama vyama na hata ajenda za maana hawana.

Mwacheni Magufuli apumzike kwa amani mema na mabaya Mungu anajua mwenyewe.
Hawezi kupunzika Kwa Amani yule Mtu
 
Wazee na miaka yote kwenye Chama na serikalini wakijua mbinu zote sasa ilikuwaje wakampa mtu aliesema Wakinichagua watalimia meno

Hapo wanasiasa walafi wakaanza kukenua meno na kufikiri wananchi watakoma na kuwa Vibogoyo jamaa likishika
Hapo wakamnadi na kumpa kijiti ila hawakujua wao pia ni sehemu ya wananchi

Haikuhitaji Rocket science kuling’amua hilo ila wakaingia mkenge
Sasa wananadi Haki na Amani
Ila Kweli aliwaweza
Wanasema you can’t teach an old ... new trick
 
Lipo wazi CCM wengi hawampendi Magufuli, ila wanajitahidi kutomshambulia moja kwa moja sababu alikuwa kiongozi wao waliomuunga mkono alipokuwa kiongozi, CHADEMA ndiyo hawampendi kabisa, ACT ndiyo kabisaa.

Wasomi wengi pia hawamkubali Magufuli, ukiwauliza tu ukiwa nao wengi wanamponda, baadhi walikuwa wakimsifia tu kipindi kile sababu ya woga au kutaka cheo ila wanyonge, kama alivyopenda kuwaita Watanzania wa kawaida, hili ndio kundi kubwa la watu na linamkubali sana, utaona comments zao Facebook na Instagram wakimfagilia, ila hutawaona sana Twitter na hapa JF, hawapendi sana hii mitandao.

Najiuliza ni kwa nini? Magufuli alikuwa akiwaeleza watu Tanzania ni tajiri, miradi mingi tunaifanya kwa fedha zetu, akawaeleza pia yeye siyo miongoni mwa kundi la elites ndani ya CCM walioifisadi nchi.

Pia alisikika akisema mtu katika utawala wa nyuma masikini aliweza kufanywa chochote na tajiri ila katika utawala wake tajiri anaweza kufanyiwa chochote, aliruhusu pia wafanyabishara ndogondogo kufanya biashara popote na kusema yeye ni mkombozi wao.

Alikuwa akiwafokea, kuwatukana na kuwafukuza maafisa wa Serikali waliokuwa wakilalamikiwa na wananchi mbele ya hadhara, na mara nyingi alisimama kusikiliza matatizo binafsi ya wananchi kama vile mirathi.

Haya na mengine mengi yaliwafurahisha sana watu wa tabaka la chini ambalo liliamini shida zao zinatokana na kuonewa na viongozi wa serikali na matajiri

Sasa kwa nini wasomi na wanasiasa wengi wasimpende? Kwa haraka haraka mtu ukitazama uongozi wa Magufuli utaona ni uongozi wa kuleta maendeleo na kuondoa rushwa, kuwapa haki wanyonge dhidi ya matajiri na mabwanyenye na kuipaisha nchi kiuchumi.

Mtu huwezi kusema unaondoa rushwa huku ukiua uwazi, unafunga na kuua wanaokosoa, ukifungia na kuvitisha vyombo vya habari, huwezi kusema utakuza uchumi na kipato cha watu huku unakandamiza sekta binafsi kwa kuvuruga biashara, huwezi kusema hubagui watu kwa vyama huku ukiwaambia mmechagua upinzani maendeleo siwapi, huwezi kusema upo against na mabwanyeye huku ukiwajengea mahekalu wastaafu, na kuteua watoto wao na wake zao kwenye vyeo vya kisiasa badala ya watu wa kawaida.

Huwezi kusema umerudisha nidhamu kwa watendaji wa serikali huku wateule wako wakiingia benki na kupora mchana kweupe, kuvamia vituo vya habari na walinzi wa ikulu, Polisi wakiua na kubambikiza watu kesi, watu wenye uelewa hawawezi kukuelewa kamwe.

Samia kwenye moja ya mahojiano yake, alisema anataka legacy yake iwe ni kuwafanya watanzania kujitambua hasa kwenye mambo ya siasa na uraia, nafikiri ameona watanzania wengi hawajui wana uelewa mdogo sana kwenye siasa na ni rahisi sana kuwalaghai.
ACT na CUF vyama vya kidini, CDM chama cha kikabila na CCM ni chama cha wahuni kusema ukweli. JPM alichomoza kutoka chama cha wahuni akiwa mtu clean sana. Na wanapomshambulia ndipo wanapochemka kwani yuko kwenye mioyo ya watu waluo wengi. 2025 itawapa picha. Hawa watoto wa Kambo wakiamka sasa na kuweka mtu sahihi watachukua Nchi. Asiwekwe makengeza wala mwenye buti moja kubwa wala yule tapeli na mdini mkubwa wa ACT.
 
Nachoshangaa watu wanasema Magufuli aliharibu nchi wakati katika miaka 60 ya uhuru yeye katawala miaka mitano tu, je hao wengine wamefikisha taifa wapi ukilinganisha na mataifa mengine.
Chuki aliyoijenga kwenye taifa ya wasionacho kuwachukua walionacho ndicho kitu kibaya sana kuwahi kufanywa kwenye nchi hii. Kabla ya hapo aliye chini alikuwa anamfata aliye juu naye anakuwa juu hamna ugomvi. Hivi sasa wasionacho wanawasingizia walionacho kwa Hali Yao. Hakuna flyover wala ndege 20, wala sgr au sijui bwawa la umeme litakalowaponya watanzania kwa muda mrefu ujao kutoka kwenye chuki iliyojengwa awamu ya tano. Wewe huoni hasara hiyo kwa taifa
 
Hili ni jukwaa la chadema, kwa hiyo kupigwa ban sisi tusioimba pambio za kuisifu chadema ni kawaida, tumezoea.
Kwani wewe unadhani huyo rafa wenu atadumu milele? Kufa atakufa, na atazikwa pia, tena bila mikunjo!
Hapa hatuna mtu wetu, vyama vyote CCM, Chadema, ACT, CUF na wengineo tunasherehekea kufukia lile gaidi kule Chato
 
ACT na CUF vyama vya kidini, CDM chama cha kikabila na CCM ni chama cha wahuni kusema ukweli. JPM alichomoza kutoka chama cha wahuni akiwa mtu clean sana. Na wanapomshambulia ndipo wanapochemka kwani yuko kwenye mioyo ya watu waluo wengi. 2025 itawapa picha. Hawa watoto wa Kambo wakiamka sasa na kuweka mtu sahihi watachukua Nchi. Asiwekwe makengeza wala mwenye buti moja kubwa wala yule tapeli na mdini mkubwa wa ACT.
Watoto wa kambo akina nani? Na wamuweke mtu gani kupitia chama gani?
 
Wapigaji hawanaga akili kabisa, ukishakuwa mdokozi, mnafki, mbinafsi, mchoyo, mwizi, muongo..huwa unakosa hata maarifa ya mambo mengine. Hao wote ni wapigaji na wanafikiri bado Magufuri yupo hai wanajaribu hadi kugombana na kivuri na maiti yake wasijue hata wao kesho ama kesho kutwa nao wanakufa, tena wao watakufa kwa aibu kila mtanzania aliye hai atanena juu yao. Tunayo safari ndefu sana ktk nchini, yaani katika watu milioni 60 wanaozeeka na kustaafu wanaonekana ni wazuri kuliko vijana hadi inafikia hatua ya kurudisha vibabu vilivyostaafu vije madarakani. Nchi iongozwe na vizee vya mawazo ya karne ya 10 vitawale leo hii ni dharau sana. Hovyo sana, wanakuja kulipa visasi au wanakuja wafia ofisini wakifunua mafaili?? . Tubadilike kidogo jamani😎😎
 
Back
Top Bottom