Kwanini Marekani wana economic cooperation with China? Dunia ina unafiki sana

Marekani si inasema watu wa Xinjiang China wanauawa na wakosoaji nchini China wanafungwa na kuuawa mbona hawaingilii kati

Marekani imekosoa Russia kwa kufungwa kwa wapinzani, uhuru wa vyombo vya habari, na vita vya Ukraine. Lakini imeepuka kuingia vitani moja kwa moja

Marekani imekuwa mkosoaji wa Saudi Arabia kuhusu haki za wanawake, wanaharakati kufungwa,
na kesi ya mwandishi Jamal Khashoggi. Lakini Marekani bado ina uhusiano mkubwa wa kiusalama na mafuta na Saudi Arabia

Marekani imekuwa ikiikosoa North Korea kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, utawala wa kiimla na programu za nyuklia. Lakini haijaingilia moja kwa moja

Marekani imekuwa ikiokosoa Eqypt kuhusu wapinzani kufungwa, uhuru wa habari na uchaguzi. Lakini Marekani inaendelea kushirikiana nayo

Hii inaonyesha kuwa katika siasa za kimataifa, Marekani mara nyingi huamua hatua zake kwa kuchanganya:
​
  • maadili (demokrasia na haki za binadamu)​
  • maslahi ya kiusalama​
  • uchumi​
  • na nguvu ya taifa husika​
Ndiyo maana nchi tofauti hutendewa kwa njia tofauti.​
 
Inahusianaje na economic cooperation na China?
 
Hivi tunacho cha kulinda?
Ndio Uhuru wa Taifa (Sovereignty)

Tanzania ina haki ya kufanya ushirikiano wa kiuchumi na nchi yoyote inayoweza kusaidia maendeleo yake ikiwemo China

Ushirikiano na China haupaswi kutafsiriwa moja kwa moja kama uadui dhidi ya Marekani
 
Toka tunapata Uhuru tumekuwa tunasaidiwa na wazungu Hadi matundu ya choo, pia sio hivyo Tu Hadi budget ya nchi yetu tunasaidiwa Kwa asilimia 50 ....mikataba mingi tumeingia na wazungu hasa ya Haki za kibinadanu na democracy matters.
Mimi kwenye suala la haki za binadamu na Demokrasia sio hoja yangu

Niko kwenye hoja ya kiuchumi: Swali ni Marekani ndiye anayepaswa kuipangia Tanzania nchi za kushirikiana nao kwenye biashara?
 
Unawezaje kuifananisha china na TANZANIA juu ya siasa ya uchumi? Ukitaka kutunisha msuli na wazungu jitegemee Kwanza Kiuchumi
Huyu jamaa anatoa mifano iliyokufa kabisaa!!! China na TANZANIA wapi na wapi..
Hatupo kwenye ulinganisho wa China na Tanzania. Tusikimbie hoja ya msingi

Ninachozungumzia ni Multi-Alignment diplomacy. Tanzania ni nchi huru ina uhuru wa kuchagua washirika wake wa kibiashara kulingana na maslahi yake

Tanzania haichagui upande wa siasa za mataifa makubwa inachagua maendeleo yake. Biashara na China si upinzani kwa Marekani, ni matumizi ya fursa za kimataifa kujenga uchumi wake
 
TZ siyo China wala URUSI. Hatufanani chochote.


China na URUSI wanajua kuwajibishana wao kwa wao. Na kila mwananchi anaona.

Hawahitaji kelele za Marekani.
 
Umesema vyema, China haicheki na majizi na mafisadi na wala hawakuhitaji Demokrasia ya Magharibi kupambana na hilo
China hawahitaji Demokrasia ya magharibu, kwasababu kujiunga CCP kwenyewe ni mziki.

Super MERITOCRAClTIC.

Hawaokoti okoti, wala kutumia CHAWACRACY na NEPOTISM kupata viongozi.

Na Uongozi wa China siyo sehemu ya kupata UTAJIRI au IMPUNITY.
 
Mimi kwenye suala la haki za binadamu na Demokrasia sio hoja yangu

Niko kwenye hoja ya kiuchumi: Swali ni Marekani ndiye anayepaswa kuipangia Tanzania nchi za kushirikiana nao kwenye biashara?
Tunapangiwa ndiyo Hadi marafiki wa kucheza nao.
Sisi kama Tanzania hatuwezi kuingia kufanya biashara na nchi kama china bila kuangalia kama itaumiza umoja wa ulaya na USA, kwenye madini ni mfano mzuri kwasababu hii raslimali ipo chini ya ulaya Kwa hapa TANZANIA , bado hakuna Uhuru wa kuamua mambo wenyewe
 
Ndio Uhuru wa Taifa (Sovereignty)

Tanzania ina haki ya kufanya ushirikiano wa kiuchumi na nchi yoyote inayoweza kusaidia maendeleo yake ikiwemo China

Ushirikiano na China haupaswi kutafsiriwa moja kwa moja kama uadui dhidi ya Marekani
Deep down Zanzibar inatumia hiyo haki huku Tanganyika ikiwa usingizini.
Tanzania is illusional
 
Raia wa hizo nchi za Kiarabu na China wanaitaka demokrasia kama ambavyo Raia wa Tanzania wanavyoitaka?
Hoja ya demokrasia haiwezi kutazamwa kwa mtazamo mmoja wa dunia nzima

Mataifa hutofautiana kwa historia, utamaduni, mfumo wa dola na vipaumbele vya wananchi wake

Katika baadhi ya nchi za Kiarabu na China, wananchi wengi wamekuwa wakitilia mkazo zaidi uthabiti wa dola, maendeleo ya uchumi na usalama wa kijamii kuliko mfumo mpana wa ushindani wa kisiasa

Kwa hiyo, si sahihi kudai kwamba kila jamii ina uelewa au matarajio sawa kuhusu demokrasia kama ilivyo Tanzania

Mahitaji ya kisiasa ya wananchi hujengwa na mazingira yao ya kihistoria na kijami
 
Demokrasia ya Tanzania ikoje??

Ukiachana na stori za Urusi, China na Marekani, sisi kama sisi tulikubalinaje?

Madaraka yanapatikanaje?
Viongozi wanapatikanaje?
Wakosaji wanafanywaje?
 
Demokrasia ya Tanzania ikoje??

Ukiachana na stori za Urusi, China na Marekani, sisi kama sisi tulikubalinaje?

Madaraka yanapatikanaje?
Viongozi wanapatikanaje?
Wakosaji wanafanywaje?
Makubaliano yanajulikana lakini inahusianaje na Tanzania kutiliwa shaka kuwa na ushirikiano wa kiuchumi na China?
 
Makubaliano yanajulikana lakini inahusianaje na Tanzania kutiliwa shaka kuwa na ushirikiano wa kiuchumi na China?
Hoja inaanza na wewe, kama HUJIELEWI.


Marekani ni MHUNI.

Hizo hoja mbili za WAKRISTO na China zimewekwa kimkakati ili WATUSHONE.

Vyote ni kwasababu za UPUMBAVU wetu wenyewe.
 
Lakini China imewekeza zaidi Tanzania kuliko Marekani. Na Tanzania ni trade partner mkubwa wa China kuliko Marekani

Kwa hiyo hoja yako ya kusema Tanzania haiwezi kuingia kufanya biashara na China bila kuangalia kama itaumiza Marekani si kweli
 
Hapa sasa umeongea, wawajibishane kwenye masuala ya KISIASA lakini kwenye masuala ya KIUCHUMI hapo ni uhuni tu wa Marekani
Kwenye huo MUSWADA hawaweki vikwazo kwa nchi.

Target ya Vikwazo ni kwa Viongozi wa CCM, JESHI na serikali.

Na tulivyo na INCOMPETENT REGIME, haijulikani itakiluwaje, maana uwezo wao wa kutatua matatizo ni mdogo mnoo, nje ya KUUA, KUTEKA na KUHONGA
 
Historia yetu sisi haiwezi kutengewa na demokrasia, Nyerere aliipata hii nchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia uliosamimwa na Wakoloni, Alivikuta vyama vingi akavufuta na baadaye wakavirudisha tena, makubaliano yetu sisi ni uongozi up upatikane kupitia uchaguzi huru na haki, China na Gulf states za Uarabuni wao hawajawahi kuwa na demokrasia, labda pia hawahiitaji lakini sisi tunahiitaji kulingana na historia yetu.

Ni vigumu sana kuwa na udikteta kwenye Taifa lenye Wakristo wengi.
 
Makubaliano yanajulikana lakini inahusianaje na Tanzania kutiliwa shaka kuwa na ushirikiano wa kiuchumi na China?
Mahusiano ni kwamba inaonekana China inapata kirahisi deals za kuvuna rasilimali Africa kwa sababu serikali ya China haidai uwajibikaji wowote kutoka kwa serikali za Africa kuhusiana na raia. Yani kama kuna madini maalumu kijiji fulani serikali ya Africa hata ikiua kijiji kizima ili kuwapa kampuni ya kichina kuchimba serikali ya China haitahoji au kusema chochote na pia hakuna mwanaharakati wa kichina wa kusema chochote tofauti na ilivyo kwa US.
 
Waondoe pia pro-Russia, pro-China na pro-Arab mentality.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…