Kwanini Marekani wana economic cooperation with China? Dunia ina unafiki sana

Kwanini Marekani wana economic cooperation with China? Dunia ina unafiki sana

Xi
China imewahi kuwekewa vikwazo vingi sana, lbda wewe hujafuatilia tu. Ila tu China vile vile wana leverage. Halafu wanayo 'absorption" capacity kubwa kuliko viinchi kama Tanzania. Absorption nina maana kuwa China ni kubwa, na liuchumi wake ni kubwa, unaweza uka-sacrifice sehemu moja ukashangaa inazidi kupumua kwa nguvu tu. Sawa sawa kwenye ndondi, heavy weight na light weight wakipigana, light weight utapiga heavy weight ngumi kumi lakini atahimili. Light weight ngumi moja tu ya heavy weight anaweza kuzilai.

Leverage- tunahitajiana na tunaongea. Vikao vinavyofanywa kati ya China na Marekani ni vingi mno kama siyo kila wiki basi kila mwezi Na ukisikia wanavyoongea ni kabisa wanaelewana, constructive argument. Kuna wakati wanakaruzana lakini kuna heshima.

China amewahi kuwekewa Vikwazo kwenye mauaji ya Tianamen 1989, amewahi kuwekewa 2019 kuhusu Hong Kong, kwani hamuoni? Lakini Mchina anasimama anaanza kubisha na kujadili na mchina anaogopa sana uchumi wake usihathirike kwa sababu bila ya kuuza nje Ulaya au Marekani hawewezi kutoboa.

Kwa sasa manufacturing duniani wanategemea world factory yaani China, na consumer mkubwa Marekani na Ulaya.

Kuhusu suala la Waislam wa Xinjiang Province wachina walifanya kazi kubwa sana kuongea na UN, USA, Ulaya na kote huko, mara ya Mwisho unakumbuka Mkuu wa UN human righ yule mama wa Chile aliachia ngazi kwa sababu ya suala hili. Baada ya kuzulu China na kuangalia kule Xinnjiang alikataa kutoa report. Ikazikwa akaachia ngazi.

Watu wanaongea, siyo hao vichaa wenu, ati "Who are you" anapigiwa makofi anaona sifa.
Tiananmen square incidence ilikuwa 1989, kwa nini baada ya hapo Marekani na nchi za Magharibi waliendelea kufanya FDI China?
 
Moja ya jambo limeniacha na peace of mind ni kuwa neutral sana kwenye siasa za Tanzania zisizoeleweka.

Nimeona mahali JF mleta mada ameleta document ya Desemba 2025 ambapo bunge la senate la Marekani limepanga kupitisha muswada unaagiza kutathmini ushirikiano wa Tanzania na China kijeshi, kiuchumi na kisiasa.

Wanasubiri tu Trump abariki muswada huo kwa kumwaga wino Tanzania ishughulikiwe.

Kwa miongo kadhaa media na wachambuzi wa Magharibi wakiongozwa na Marekani wamekuwa wakiiaminisha dunia kuwa China haina Demokrasia, uhuru wa maoni, wala uhuru wa vyombo vya habari hakuna.

Na kama haitoshi wanasema kuwa Serikali ya China huwa inawanyanyasa, kuwatesa na kuwaua jamii ya Waislamu iliyopo Xinjiang.

Mbona hao Marekani bado wanafanya biashara za billions of dollars na China?

Nchi ambayo haifuati Demokrasia ya Magharibi na wanadai inaua Waislamu Xinjiang?

Wamuondoe Xi na chama cha CPC basi tuone au waondoe economic cooperation na China.

Lakini ndio kwanza wiki 2 zilizopita Trump alienda kutafuta deals China. Dunia ina unafiki sana, inataka akili sana ku-deal na Marekani na nchi za Magharibi.

By the way hapa ni mahali Watanzania waondoe uCCM, uCHADEMA, uhanarakati, na Pro-U.S mentality panataka akili sana. Kwa sehemu muswada ulisema:
​

Directs the Administration to evaluate the extent of the People’s Republic of China’s military, economic and political engagement in Tanzania, including cooperation that could undermine democratic institutions and U.S. interests in the region.
​
Hizo interests za Marekani ni zipi?​
Chawa wengi humu ndani wataishia kukutukana hutapewa jibu la maana.

Hao wamarekani siku zote wanaangalia maslahi yao yapo vipi, hizi habari za demokrasia ni geresha tu za kuwapatia wanasiasa wao hoja za kuwajibu waandishi wao wa habari.
 
Kwa hiyo viongozi ndio wanaocooperate kiuchumi na China?
Kwani lazima hao wauaji ndio wawe viongozi??

Unaniuliza kama vile mimi ndio Marekani.

Una watawala ambao wana MAKOVU yenye USAHA, Marekani anatumia hayo MAKOVU kuwatenga, kama wewe unaona kwako hayo makovu hayana shida, wao hawayataki.

Sasa kama.m wewe unaona NCHI=SAMIA na Genge lake (Vimeungana na havitofautiki), hilo siyo la Marekani.

Ni tatizo lako.
 
Tiananmen square incidence ilikuwa 1989, kwa nini baada ya hapo Marekani na nchi za Magharibi waliendelea kufanya FDI China?
Wachina wanaichukuliaje nchi yao?

Hata Nyerere hakuwapa Wazungu wanachotaka, ila walimheshimu kwasababu aliheshimiwa na watu wake. Vita ya Kagera kila mtu alishiriki.

Leo TZ, watawala wako busy kuteka watu na kuua mpaka wajawazito na watoto, kupora haki kupitia mahakama, WIZI, UFISADI.

Hivi unadhani leo nchi ikivamiwa, labda UVCCM na ABDUL ndio wataenda kupigana.
 
Inategemea unamaanisha demokrasia kwa kipimo gani

China haina demokrasia ya vyama vingi na uchaguzi wa ushindani wa kitaifa kama ilivyo kwenye mfumo wa Magharibi.

China ina aina yake ya demokrasia ya mashauriano ambapo kuna uchaguzi wa ngazi za chini (kijiji na mtaa)

Maamuzi hufanywa kupitia mfumo wa chama na taasisi za serikali na maoni ya wananchi hupokelewa kupitia vyombo vya chama, mashauriano na tafiti za kijamii

Kwa tafsiri ya kimataifa ya demokrasia (vyama vingi + uchaguzi huru wa kitaifa), China si demokrasia

Lakini kwa tafsiri yake yenyewe, China ina aina yake ya demokrasia inayolenga utulivu na maendeleo badala ya ushindani wa vyama

Kama demokrasia ya Magharibi ya ushindani wa vyama ndiyo kipimo pekee cha mafanikio, basi kwa nini China imepiga hatua kubwa za maendeleo kuliko nchi nyingi zenye uchaguzi wa vyama vingi?
​
Hakuna demokrasia bila kuwa na mfumo wa vyama vingi, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mihimili ya dola, mahakama huru na uchaguzi huru.

Mfumo wa mashauriano uko hata Saudi Arabia, Qatar, Oman, Kuwait na UAE ambapo wafalme wanafanya maamuzi kwa kushauriana na Baraza la majlis ila huo sio mfumo wa kidemokrasia.

Pia hakuna demokrasia ya Kichina au ya tafsiri ya Kichina, hakuna demokrasia ya tafsiri ya Kitanzania. Demokrasia ni moja tu na tafsiri yake ni moja kote duniani na demokrasia ni zao la Magharibi. Kusema kuna demokrasia ya Kichina ni sawa na kusema Ukristo wa China au Ubudha wa magharibi.

China ina mfumo wake wa kujitawala usio wa demokrasia, kuhusu huo mfumo kuleta au kutoleta maendeleo ni mjadala mwingine.
 
Umeuelewa huo mswada?? Kitu cha Kwanza cha US ni kuhusu Tanzania ni kuundermine democratic institutions, sasa wewe unakubaliana nao au unapingana nao hapo ndio nitakuja kwenye Hilo jingine
Mleta mada sio mgeni hapa jamvini kwa namna alivyo shabiki wa China.
 
Hakuna demokrasia bila kuwa na mfumo wa vyama vingi, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mihimili ya dola, mahakama huru na uchaguzi huru.

Mfumo wa mashauriano uko hata Saudi Arabia, Qatar, Oman, Kuwait na UAE ambapo wafalme wanafanya maamuzi kwa kushauriana na Baraza la majlis ila huo sio mfumo wa kidemokrasia.

Pia hakuna demokrasia ya Kichina au ya tafsiri ya Kichina, hakuna demokrasia ya tafsiri ya Kitanzania. Demokrasia ni moja tu na tafsiri yake ni moja kote duniani na demokrasia ni zao la Magharibi. Kusema kuna demokrasia ya Kichina ni sawa na kusema Ukristo wa China au Ubudha wa magharibi.

China ina mfumo wake wa kujitawala usio wa demokrasia, kuhusu huo mfumo kuleta au kutoleta maendeleo ni mjadala mwingine.
Demokrasia siyo lazima vyama vingi.

Demokrasia lazima iambatane na UWAJIBIKAJI KWA WATU, WATU KUCHAGUANA WENYEWE, MSINGI WA HAKI na MERITOCRACY
 
Mpaka sasa swali langu halijajibiwa, inasemwa kuwa Tanzania inaundermine demokrasia

Basi kwa nini Marekani iingilie economic cooperation kati ya Tanzania na China?

Kuna uhusiano gani kati ya mambo hayo mawili?
Kwa sababu China ndio mnufaika mkubwa wa utawala usio wa kidemokrasia wa Tanzania.
 
China haiendi Afrika kama mlezi wa kisiasa bali kama mshirika wa biashara

Sera yake ya kutokuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine inamaanisha inaheshimu mamlaka ya serikali za Afrika kufanya maamuzi yao wenyewe

Ikiwa kuna ukandamizaji au ufisadi, jukumu la kwanza ni la viongozi wa nchi husika, si la China

Kulaumu China kwa kila tatizo la Afrika ni kuondoa uwajibikaji kwa wale wanaotawala Afrika

China inanunua rasilimali haiendeshi serikali za Afrika. Tatizo la viongozi wabovu ni la Afrika, si la China
Kama ambavyo China haingilii mataifa mengine wakati watawala wa nchi hizo wanaua watu wake, ndivyo hivyo hivyo hawataingilia matatizo yako, siku MABEBERU wakianza kukushona.
 
Kwa sababu China ndio mnufaika mkubwa wa utawala usio wa kidemokrasia wa Tanzania.
Wao Marekani hawajawekeza Tanzania?

Mbona hapo Tanzania wapo na mnafanya nao economic cooperation na wananufaika

Basi Marekani ilitakiwa iweke mfano kwa kuwa mstari wa mbele kuondoa ushirikiano wa kiuchumi na Tanzania
 
Hakuna demokrasia bila kuwa na mfumo wa vyama vingi, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mihimili ya dola, mahakama huru na uchaguzi huru.

Mfumo wa mashauriano uko hata Saudi Arabia, Qatar, Oman, Kuwait na UAE ambapo wafalme wanafanya maamuzi kwa kushauriana na Baraza la majlis ila huo sio mfumo wa kidemokrasia.

Pia hakuna demokrasia ya Kichina au ya tafsiri ya Kichina, hakuna demokrasia ya tafsiri ya Kitanzania. Demokrasia ni moja tu na tafsiri yake ni moja kote duniani na demokrasia ni zao la Magharibi. Kusema kuna demokrasia ya Kichina ni sawa na kusema Ukristo wa China au Ubudha wa magharibi.

China ina mfumo wake wa kujitawala usio wa demokrasia, kuhusu huo mfumo kuleta au kutoleta maendeleo ni mjadala mwingine.
Swali: Ni lazima mataifa yote duniani yafuate mfumo wa Demokrasia ya Magharibi?

Kila taifa lina haki ya kufuata mfumo wake wa kisiasa na utawala

Mwisho wa siku kinachoamua ni mfumo upi unaleta maendeleo, amani na prosperity

China wamejipata kwenye socialism with Chinese characteristics
 
Demokrasia yetu ikoje?

Mbona unakwepa UKWELI?

Utaratibu wetu wenyewe, tumekubaliana vipi?

Tunaheshimu utaratibu huo?

Huu upumbavu wa kushindwa kutoa majibu, na kutafuta watu wa kulaumu haujawahi kutatua tatizo lolote
 
Swali: Ni lazima mataifa yote duniani yafuate mfumo wa Demokrasia ya Magharibi?

Kila taifa lina haki ya kufuata mfumo wake wa kisiasa na utawala

Mwisho wa siku kinachoamua ni mfumo upi unaleta maendeleo, amani na prosperity

China wamejipata kwenye socialism with Chinese characteristics
Mfumo wetu wa kisiasa na utawala Tanzania ni upi?
 
Wachina wanaichukuliaje nchi yao?

Hata Nyerere hakuwapa Wazungu wanachotaka, ila walimheshimu kwasababu aliheshimiwa na watu wake. Vita ya Kagera kila mtu alishiriki.

Leo TZ, watawala wako busy kuteka watu na kuua mpaka wajawazito na watoto, kupora haki kupitia mahakama, WIZI, UFISADI.

Hivi unadhani leo nchi ikivamiwa, labda UVCCM na ABDUL ndio wataenda kupigana.
Sio kila anayetekwa serikali inahusika. Kijana kakatwa kichwa mwezi uliopita, serikali inahusika?.

Propaganda zinaichafua sana nchi hii kwa pesa zinazolipwa kwa waandishi wa habari, wanafanya ufisadi halafu kinafiki wanauandika kwenye vyombo vyao vya habari.
 
Sio kila anayetekwa serikali inahusika. Kijana kakatwa kichwa mwezi uliopita, serikali inahusika?.
Kama hawahusiki, wanafanya nini sasa?

Kama kuna genge linakuja nchini linateka watu na kuwaua, maana yake wanaosema serikali ya CCM ni zero wako.m SAHIHI kwa 600%.
Propaganda zinaichafua sana nchi hii kwa pesa zinazolipwa kwa waandishi wa habari, wanafanya ufisadi halafu kinafiki wanauandika kwenye vyombo vyao vya habari.
Propaganda wana fanya CCM ndio maana haziendi.mbali.

Ukweli unaishi MILELE.

Waandishi gani wa Habari, hao wa TZ ambao Mhariri mkuu ni TCRA na BASHITE???
 
Kama hawahusiki, wanafanya nini sasa?

Kama kuna genge linakuja nchini linateka watu na kuwaua, maana yake wanaosema serikali ya CCM ni zero wako.m SAHIHI kwa 600%.

Propaganda wana fanya CCM ndio maana haziendi.mbali.

Ukweli unaishi MILELE.

Waandishi gani wa Habari, hao wa TZ ambao Mhariri mkuu ni TCRA na BASHITE???
Mnajazana ujinga humu mitandani hata mnapokwenda kufanya vurugu huko mtaani halafu mkapigwa shaba vifo vyenu vinakuwa na msingi wa ujinga mwingi.

Hakuna genge lolote linalotoka nje ya nchi kuja kufanya uharamia hapa Tanzania. Hakuna huo ushahidi kwamba wanajeshi walituliza ghasia tarehe 29 October ni raia wa kigeni, vijana wa hapa hapa bongo walimaliza ule upuuzi.

Watu wanauana wao wenyewe kwa sababu zao wenyewe unataka serikali iziue wasiuane?. Kivipi wakati kuuana kwao hutokana na sababu zao binafsi?
 
Mnajazana ujinga humu mitandani hata mnapokwenda kufanya vurugu huko mtaani halafu mkapigwa shaba vifo vyenu vinakuwa na msingi wa ujinga mwingi.
Bahati nzuri wote mnakiri kuwa nyie ndio MMEUA watu, mpaka wanawake wenye MIMBA.

Tutajua mtokeo yake siku chache zijqzo.
Hakuna genge lolote linalotoka nje ya nchi kuja kufanya uharamia hapa Tanzania. Hakuna huo ushahidi kwamba wanajeshi walituliza ghasia tarehe 29 October ni raia wa kigeni, vijana wa hapa hapa bongo walimaliza ule upuuzi.
Ushahidi huwezi kuutoa wewe. Itafamika tu, hata miaka 50 ijayo.
Watu wanauana wao wenyewe kwa sababu zao wenyewe unataka serikali iziue wasiuane?. Kivipi wakati kuuana kwao hutokana na sababu zao binafsi?
Huu ni uthibitiaho mwingine, tuna zigo la mavi ya nguruwe Ikulu
 
Bahati nzuri wote mnakiri kuwa nyie ndio MMEUA watu, mpaka wanawake wenye MIMBA.

Tutajua mtokeo yake siku chache zijqzo.

Ushahidi huwezi kuutoa wewe. Itafamika tu, hata miaka 50 ijayo.

Huu ni uthibitiaho mwingine, tuna zigo la mavi ya nguruwe Ikulu
Kulalamika ni jadi na asili ya mtanzania, akipewa yeye nafasi vichekesho vitupu.

Hao waliouliwa wangeingia ikulu tungekuwa tunajiliza kwa kina ICC kuhusiana na vifo vyao?.

Mlitaka kufanya mapinduzi ya kihuni mkadhibitiwa kihuni pia.
 
Back
Top Bottom